Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Sabaya amehukumiwa miaka 30 jela. Mahakama ya hakimu mkazi Arusha imemuhukumu kwenda jela kwa miaka 30 aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai ole sabaya na wenzake kwa kosa la unyang'anyi kwa kutumia siraha

----
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo amesema kuwa ameridhika mashtaka dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake na kuwatia hatiani kosa unyang’anyi wa kutumia silaha .

Baada ya kuwatia hatiani wakili wa Serikali amesema hakuna kumbukumbu ya makosa ya zamani ya washtakiwa wote watatu, na kuiomba Mahakama iwape adhabu ya miaka isiyopungiua 30 jela na viboko.
 
Wanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.

=======

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo Oktoba Mosi, 2021 baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.

Agosti 24 mwaka huu, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walikamilisha kujitetea mahakamani hapo baada ya Jamhuri kukamilisha mashahidi 11 na vielelezo vinane.

Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Mwananchi

UPDATE: SABAYA NA WENZAKE MIAKA 30 JELA


Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamehukumia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.
Aisee
 
Huyu dogo alijisahau Sana akajiona anord shwaziniga....sasa ndo hivyo afwilwe munu asigale munu
 
Siasa ni mchezo wa kuigiza kwani huonagi kila wanapokwenda wanasiasa kuna kuwa na ma camera ! Hata wakiwa ofisini kwenye kikao kuna kua na ma camera!

Hiyo ni tamthilia mkuu utakuja kustuka baadae sanaa
Rudia tena kusema
 
Tushangilia hukumu hii, lakini pia ni maandalizi ya hukumu nyingine kwa mtu fulani na shahidi akiwa huyuhuyu....hapa tunaamini mahakama imetenda haki maana kwingine tutailaumu mahakama..
Sabaya unyama wake hata kipofu aliuona, Mbowe hana kosa hata mtoto mdogo anajua, kosa lake ni kudai Katiba Mpya pekee sijui kavunja sheria ipi kwa kosa hilo?
 
Back
Top Bottom