Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakati anafanya ujinga hakujua ana mtoto?Katika hao wenzake kuna mmoja kaacha katoto kachanga mtaani.
AiseeWanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.
=======
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo Oktoba Mosi, 2021 baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.
Agosti 24 mwaka huu, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walikamilisha kujitetea mahakamani hapo baada ya Jamhuri kukamilisha mashahidi 11 na vielelezo vinane.
Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Chanzo: Mwananchi
UPDATE: SABAYA NA WENZAKE MIAKA 30 JELA
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamehukumia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.
Rudia tena kusemaSiasa ni mchezo wa kuigiza kwani huonagi kila wanapokwenda wanasiasa kuna kuwa na ma camera ! Hata wakiwa ofisini kwenye kikao kuna kua na ma camera!
Hiyo ni tamthilia mkuu utakuja kustuka baadae sanaa
Yeye mwenyewe anashukuru Mungu kumuwahisha otherwise yangemkuta tena makubwa zaidi ya haya mwogope Mungu.Miaka 30 jela? JPM huko alipo atakuwa anaumia sana vijana wake kutendewa hivi
Mtoa matunzo.Kwani yeye ndio anae nyonyesha?
Sabaya unyama wake hata kipofu aliuona, Mbowe hana kosa hata mtoto mdogo anajua, kosa lake ni kudai Katiba Mpya pekee sijui kavunja sheria ipi kwa kosa hilo?Tushangilia hukumu hii, lakini pia ni maandalizi ya hukumu nyingine kwa mtu fulani na shahidi akiwa huyuhuyu....hapa tunaamini mahakama imetenda haki maana kwingine tutailaumu mahakama..
Atapata baba mwingine mwenye tabia nzuri kuliko baba mzazi, kuna watoto hawana baba wala mama na wamekuwa vizuri tuKatika hao wenzake kuna mmoja kaacha katoto kachanga mtaani.
Kesi ya Mbowe inafutwa. Copy ya hukumu tayari ninayo.MBOWE AJIANDAE KWA MVUA YA MAANA.