Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Kwani wana kesi zinazofanana? Ama makosa yao ni sawa. Hii naona kama kauli ya kujifariji ya wakereketwa wa Sabaya. Ushahidi wa wizi na udhalimu wa sabaya nani asiyeujua ama kuusikia?
Kubalansi wote Kuachiwa imeshindikana hivyo balansi inayofanyika sasa ni Wote kwenda Jela ili Jumuiya ya Kimataifa ione kuna Haki na hakuna anayeonewa Tanzania.
 
... unajua ikoje? Iko hivi, ugaidi wa Mbowe ni kutaka kuwadhuru "viongozi" wa serkali; na kiongozi wa serikali anayetajwa kutaka kudhuriwa na "gaidi" Mbowe ni Ole Sabaya ambaye mahakama leo imeuthibitishia ulimwengu kwamba ni JAMBAZI LILILOKUBUHU na limekatiwa miaka 30 jela!

Sasa najiuliza, ugaidi wa Mbowe ulikuwa kulifanyia ugaidi jambazi tena jambazi lililotumia zana za moto? Jambazi lililojificha kwenye mwamvuli wa ukuu wa wilaya aka DC? Mbowe sio gaidi!
 
Sasa tusisikie mahakama haitendi haki kwa gaidi
Alikugaidia mamayo?

Au nani tutajie?

Ninani nchi aliyekaa na kusema mbowe anaudhuluma huu na huu kwa kufanya ugaidi?

Mbona kwa sabaya watu wengi Walton ushidi wa aliyoyatenda kuwa alikuwa nijambazi lillilojifisha nyuma ya uongozi wake.

Madai ya kudai katiba mpya ndio ugaidi unaousema?

Mbona mnakuwa hamna hoja bali mnafuata mikumbo ya policcm inayotumia madaraka yake vibaya hata ukisikia policcm akisema nilimfinya mke wako utaamini kwasababu amesema policcm wakati hakuna ushahidi unaothibitisha.

Wacha ujuha wewe kenge.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Mbowe pia ajipange...usisahau hili
Mimi kama mwana ccm, Sabaya tulishamuonya sana hapa JF,

Siasa sio uadui, Mimi ni ccm lakini mtu wangu wa karibu hana chama kabisa

Yeye anapenda mpira sana na ni shabiki wa Timu ambayo Mimi Siipendi kabisa hapa Tanzania

Siku wakishinda Yeye na watoto wanashangilia na kunizomea week nzima mpaka pale watoto watakapo sahau ndio pona yangu

Hata ccm tukishinda wananicheka sana, Wanaona nina mawazo ya kizamani kisa kuwa ccm

Sabaya aligeuza siasa vita na ubaguzi

Sasa kama nina ndugu wengi Chadema, Act na CUF na CCM na tunaishi kwa Amani na kushirikiana

Sabaya Yeye nani?
 
Hivi ni kweli Magufuli alikuwa hajui chochote kuhusu uovu wa Sabaya?
 
Wanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.

=======

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo Oktoba Mosi, 2021 baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.

Agosti 24 mwaka huu, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walikamilisha kujitetea mahakamani hapo baada ya Jamhuri kukamilisha mashahidi 11 na vielelezo vinane.

Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Mwananchi

UPDATE: MAHAKAMA YAMKUTA NA HATIA OLE SABAYA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imemkuta na hatia Lengai Ole Sabaya na wenzake katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha.

Mahakama ilimpatia nafasi Ole Sabaya ajitetee(Shufaa) kwanini asipewe adhabu kali naye aliiomba Mahakama imuonee huruma kwani si yeye bali alikuwa anatekeleza amri ya mamlaka ya uteuzi, pia ameomba mahakama imuonee huruma kwani ana mchumba anayetegemea kufunga naye ndoa na mahari ameshalipa.

UPDATE: SABAYA NA WENZAKE MIAKA 30 JELA

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamehukumia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

WASIFU WA OLE SABAYA

Lengai Ole Sabaya amezaliwa 26/12/1986 mkoani Arusha. Amesoma Shahada ya Sayansi katika Elimu Chuo Kikuu cha Mtakatifu John Dodoma (St. John University).

Ole Sabaya aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha na pia aliwahi kushika wadhifa wa Udiwani katika kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha Mjini mwaka 2015.

Ole Sabaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro tarehe 28 Julai 2018 ya aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli.

Sabaya alitenguliwa nafasi hiyo ya ukuu wa Wilaya ya Hai tarehe 13 Mei 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan ili kupisha uchunguzi wa makosa yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha. Tarehe 15 Oktoba 2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha imemhukumu Sabaya na wenzake kifungo cha miaka 30 jela.
Vile navyomuona Lengai Ole Sabaya na Daudi Albert Bashite
images (2).jpeg
 
SASA TAASIS ZIKO HURU KUTOA HUKUMU KWA HAKI, TUNASHUKULU.. ILA PIA KAMA ZIKIFANYA HAKI NA KWA YULE JAMAA BASI TUSIONE NONGWA
 
Hivi ni kweli Magufuli alikuwa hajui chochote kuhusu uovu wa Sabaya?
Kwa utawala uliojinadi Kila kitu kinaenda saw na sifa zote zili na Chelsea kuamini kama haya yalitokea Kwa bahati mbaya.
 
Baaada ya miezi/miaka kadhaa, utashangaa Mahakama kuu/ya rufaa imetengua hukumu yake kwa sababu ya bla bla gani sijui za hapa na pale zilizo kiukwa!

Dah! Ila Dogo naye alijisahau sana. Na hapo bado ana kesi nyingine ya uhujumu uchumi! Idugunde wapi ulipo mkuu! Pole sana. Hatimaye yametimia.
 
Back
Top Bottom