Lengo la Lissu ni kuua ndege wawili kwa wakati mmoja. Wenye akili tumemuelewa, ila wasio na akili hawajamuelewa

Haya mambo ya kuzunguka mbuyu umeyarudia na wewe taja majina halisi unayokusudia. Hayo mambo yenu ccm ya uongo na uoga ndo yanaiangamiza nchi tuwe wakweli kama lisu tuiokoe nchi
Mimi nimewataja kwa code, ila Lisu yeye hata code imemshinda kuweka. Kabakia kuzunguka zunguka tu mbuyu bila kufika anapoelekea.
 
Kama hizo ndio unaziita akili bhasi Tanzania tuna janga kubwa sana!!

"Mzanzibari anaeuza ardhi ,bandari ya Tanganyika"hili swala SI hasta TEC waliandika nyaraka!!?kwa hiyo TEC ni Lisu!!?

Muungano !Tume za nyalali,kisanga na warioba hazikuona muungano una shida!!?SI chama chetu ccm wabunge wake walipiga kura mwaka ule tuwe na serikali tati pale Bungeni ndio Nyerere akagoma kwahiyo hao kina nyalali,kisanga na warioba NAO ni Lisu!!?na wale wabunge was 1995 pale Bungeni waliopiga kura ya serikali tatu walikua wabunge was chadema!!?au Lisu alikuwemo!!?

Comrade Lazima ccm tutumie akili mi najua Tumegawanyika sana kwenye Timu nyingi ndani ya chama!

Mimi ni Timu Warioba,Butiku,sokoine na Timu ya 1995 ya wale wabunge!!nawakubali hao!
 
Kumbe unaelewa kuwa kwa Sasa watanzania wana akili na Wapuuzi tunawapuuza na upuuzi wao haya endelea.
Ndio mkuu si unaona porojo zote anaongea Lisu peke yake. Hakuna Mnyika, Lema, Mbowe, Sugu wala Mnyika anaemuunga mkono.

Ingekuwa zamani angeungwa mkono na hao wote niliowataja na aliyoyasema yangepigiwa kelele ktk kila mkutano wao. Ila leo anabwabwaja mwenyewe tu kama garibovu.
 
Hamas walikuwa Shirikani UN na wenyewe vibarua wa kusambaza Vyakula vya Misaada

Ilipofika October 7 wakayabadili Maisha ya Wayahudi hadi Leo hii πŸ˜„πŸ˜„
Hapo kwa Hamas nimekuelewa mkuu πŸ˜‚πŸ˜‚, tuje kwa mkombozi wa Chadema, je ni yule aliefananishwa na Mandela enzi za kesi yake ya uhaini?

Au huyu aliekoswa koswa kurudishwa kwa mwenye dunia yake baada ya kuonekana kusaliti juhudi za baba mwenye nyumba wa enzi zile?
 
Hiyo Political Tactic ...Lissu ni Kifaru anafungua njia ...then wakina Lema Msigwa nk wamalizie KUPONDAPONDA kila square metres ya Tanganyika including Unguja

Hii inahitaji AKILI KUBWA TU

Stay tuned.....
 
Haya maswali na lawama zako zilitakiwa zielekezwe kwa wale waliopokea mamilioni ya kodi zetu kusimamia bunge la katiba ambalo lingesaidia leo hii hao kina Mbarawa kutokuwa katika baraza wala udiwani wa Tanzania bara. Badala yake wakapokea posho na kukimbia bungeni, hali iliyopelekea bunge kuvunjwa na sheria zilizopo kuendelea kutumika mpala leo.
 
Ndo tatizo la vijana ku comment nyuzi kwa sababu ya kupata malipo. Yani unakuta mtu anashindwa hata kusoma alichoandika zaidi ya kuangalia kichwa cha habari ana comment na kuwahi ufipa kuchukua posho.

Mada inahusu watu waliopokea mshiko kutoka kwa mama Abdul (hapa anazungumziwa yule alietoka jela, na kukimbilia ktk "jumba la taifa" kimya kimya kuonana na mama Abdul) ili kuhakikisha wapambanaji wa kweli wa chama akiwemo yeye mwenyewe Lisu hawashindi katika uchaguzi wa ndani wa chama na kuleta mageuzi ya kweli ndani ya chama na hatimae chama hicho kushinda chaguzi zijazo. Wewe unaleta nyimbo zako za taarabu ambazo zimeshaibwa na wenzako muda mrefu huko nyuma.

Ndomaana nikasema ni watu wenye akili kubwa tu ndo tunaweza kuandika na kuelewa mambo kama haya.
 
Hiyo Political Tactic ...Lissu ni Kifaru anafungua njia ...then wakina Lema Msigwa nk wamalizie KUPONDAPONDA kila square metres ya Tanganyika including Unguja

Hii inahitaji AKILI KUBWA TU

Stay tuned.....
Hakuna cha political tactic hapo. Kitendo cha Lisu kuhusisha uchafu unaoendelea katika uchaguzi wa ndani ya chama na hela za mama Abdul, na pia kuhoji aliemwalika mama Abdul katika sherehe za siku ya wanake katika chama chao kinaonesha fika kuwa analengwa namba 1 wao wa chama ambae ndio aliekuwepo na kuongoza mapokezi yale.

Pia hizo pesa za mama Abdul anazodai kutumika ndan ya chama anamaanisha zimepokelewa na namba 1 huyo ambae alipotoka tu selo alienda kimya kimya ktk jumba jeupe kuonana na huyo ambae Lisu anamwita mama Abdul. So kwa mantiki hiyo hao jamaa hawawezi kumuunga mkono Lisu hata chembe, kwa vile kauli ile inaonekana kumlenga zaidi namba 1 wao ambae ndio anaewafanya hao wengine wawe katika position walizokuwa nazo leo chamani.
 
Wewe unaamini Nyerere alimfuta Kazi kweli Mzee Mtei au alitaka tu kujua yanayoendelea Kule duniani? πŸ˜‚πŸ˜‚

Hao Wawili unaowataja hawajajikuta pomoja kwa bahati Nasibu

JK: Usione Vyaelea Vyaundwa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ”₯
 
Kama aliyeandika huu uzi na hii comment ni akili kubwa,basi sitashangaa tena kwa nini Tanzania haipati maendeleo hata baada ya miaka 60 ya uhuru.
Jibu ni wajinga, mazwazwa na vilaza kujiona wao ndio wenye akili nyingi na kustahili "makuu" na "kutawala" na kuacha wenye akili na uwezo wa kuwa "viongozi" nnje.
 
Huo ni mtazamo wako....

WaTanzania tumechagua kwenda na Lissu iwe jua iwe usiku Huyu Binadamu anasimamia katika UKWELI

NOTE: Hizo pesa zilizo tumwa kuivuruga Chadema ndo zinakwenda KUIPA NGUVU KUBWA SANA

They think money can work ndo maana wako KIMYAA....

Yaani watupie nyama wavurugane....Hii mbinu ilisha tunguliwa long time

Unaweza kufikiri ni jangwa kumbe chini ni tindiga la maji lenye KINA KIREFU

Mbuyu unapoanguka kishindo ni kikubwa sana ...
 
Wewe unaamini Nyerere alimfuta Kazi kweli Mzee Mtei au alitaka tu kujua yanayoendelea Kule duniani? πŸ˜‚πŸ˜‚

Hao Wawili unaowataja hawajajikuta pomoja kwa bahati Nasibu

JK: Usione Vyaelea Vyaundwa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ”₯
Unajisumbua bure kuelewesha "kiazi" ambacho kinapata kula yake kwa propaganda ya "kutoelewana kwa TL na Mbowe" kila uchwao.
 
Wewe unaamini Nyerere alimfuta Kazi kweli Mzee Mtei au alitaka tu kujua yanayoendelea Kule duniani? πŸ˜‚πŸ˜‚

Hao Wawili unaowataja hawajajikuta pomoja kwa bahati Nasibu

JK: Usione Vyaelea Vyaundwa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ”₯
Naam hapa umeandika kikubwa. Yani kwa kiswahili cha kule kusini tunasema huu ni n'tazamo wa waliokwenda jando tayari πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…