Lengo la uzi ni kuendelea kukumbushana kutenda wema hata kama mtu humjui

Lengo la uzi ni kuendelea kukumbushana kutenda wema hata kama mtu humjui

L
Hey people,

Leo katika pita pita za hapa JF nimekutana na moja ya nyuzi nyingi za marehemu,mwanaJF mwenzetu Mpauko ambazo kwa namna moja ama nyingine alizianzisha kwa lengo la kupata msaada

Binafsi huyu member nilizoeana nae kidogo humu jukwaani na ni moja ya kifo kilichoniumiza japo sikuwahi kumfahamu zaidi ya kutumiwa picha yake moja ambayo hadi sasa ninayo

Ajabu ni kwamba huyu marehemu alishawahi kuniPM kuniomba msaada wa jambo fulani lakini PM yake nilikuja kuisoma baada ya uzi wa kifo chake kuwekwa humu sijajua ni kwa namna gani niliacha kusoma PMs chache nilizokuwa nazo kwa wakati ule na sio kawaida yangu(huwa najitahidi kusoma PMs zote kwa wakati)

Lengo la uzi ni kuendelea kukumbushana kutenda wema hata kama mtu humjui,kiufupi hai-cost chochote kuwa mwema,mimi nitajitahidi

Akiwepo mtu anajiona hana wa kumsikiliza, Joanah nipo kwa ajili ya kila mtu,karibuni aseee

Kwa yoyote anayepitia magumu kiafya,kiuchumi ama kinamna yoyote usikate tamaa,yatapita.....mimi naomba 2025 ikawe ya heri kwa kila mtu

Cheers to 2025 🥂

View: https://youtu.be/ro-8dhLL6IU?feature=shared

ife is too short tuache kupandisha mabega
 
Mie naomba msaada hapa wa kiuchumi.
Man utd vers newcastle nataka weka laki...niweke o2.5 au GG?

Weka GG manake Man U lazima wapate goli na walivyo wapuuzi lazima waruhusu goli,pengine hata wakafungwa
Sema odds za over 2.5 tamu kuliko za GG

Kwa over 2.5 weka hiyo 100K na mbupu 1....zingatia,mbupu weka 1 tu
 
Ms. Joanah Asante kwa kutukumbusha, aisee hata Mimi huo uzi wa Mpauko Leo mchana niliusoma aisee nilisikitika sana kwa Baadhi ya comments za watu.

Ubarikiwe sana na umefanya jambo jema sana kutukumbusha. Sisi binadamu sio kitu kabisa. Afya, kipato na muonekano huwa unatufanya tuwe na kiburi na maringo.

Allah akubariki sana.
 
Amen mkuu....atubariki sote
 
Back
Top Bottom