Mpalakugenda
JF-Expert Member
- Jun 2, 2015
- 4,611
- 5,009
Ni sahihi zoezi kama hilo linaendelea. Hata mimi nimefikiwa. Nadhani wanalifanya nchi nzima maana kuna mtu kanda ya ziwa ameniambia pia.Leo asubuhi Mjumbe wa nyumba 10 amekuja kwangu kutaka kuniorodhesha kama nina kadi ya CCM. Mimi nikamuuliza nani kakutuma uorodheshe watu? Unawaorodhesha kwa sababu gani? Yeye kanijibu kuwa ametumwa na Katibu wa CCM kata kuorodhesha watu na kadi zao.
Jibu nililompa ni kuwa mimi sina chama na ni raia mwema hapa mtaani. Nikakataa kuorodheshwa na akaondoka. Nauliza kuna tatizo gani? Mbona CCM inaorodhesha watu karibu na uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Jambo hili linatakiwa likemewe kwa nguvu zote.