Leo Desemba 9, 2024 ni Kumbukumbu ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika, una ujumbe gani kwa Viongozi na Wananchi wake?

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Leo tunapoadhimisha miaka 63 tangu Tanganyika kupata uhuru wake mnamo Desemba 9, 1961, tunakumbushwa juu ya safari ya kujitawala, mshikamano, na kujenga taifa lenye matumaini.

Ni siku ya kukumbuka juhudi za mashujaa wetu waliopigania uhuru kwa nia ya kuleta haki, usawa, na maendeleo kwa kila Mtanzania. Pia ni fursa ya kutathmini tulipotoka, tulipo, na tunakokwenda kama taifa linalothamini amani, umoja, na uzalendo.

🙌 Tusherehekee kwa kutenda haki, kuchapa kazi kwa bidii, na kusimamia misingi ya uhuru wetu. Pamoja tunaweza kujenga Tanzania tunayoitaka!
 
Ingependeza Muwataje Majina walochaingia kupatikana UHURU ili vizazi vinavokuja Wawajuwe
 
Leo tunapoadhimisha miaka 63 tangu Tanganyika kupata uhuru wake mnamo Desemba 9, 1961, tunakumbushwa juu ya safari ya kujitawala, mshikamano, na kujenga taifa lenye matumaini.

Ni siku ya kukumbuka juhudi za mashujaa wetu waliopigania uhuru kwa nia ya kuleta haki, usawa, na maendeleo kwa kila Mtanzania. Pia ni fursa ya kutathmini tulipotoka, tulipo, na tunakokwenda kama taifa linalothamini amani, umoja, na uzalendo.

🙌 Tusherehekee kwa kutenda haki, kuchapa kazi kwa bidii, na kusimamia misingi ya uhuru wetu. Pamoja tunaweza kujenga Tanzania tunayoitaka!
TANGANYIKA yenyewe tunayoisheherekea haipo, ilikwisha nyakuliwa siyo HURU TENA.
 
Tanganyika inatawaliwa na Mzanzibari! Vituko kweli!
 
Maisha kipindi Cha ukoloni yalikuwa mazuri kuliko haya ya sasa.
 
Leo tunapoadhimisha miaka 63 tangu Tanganyika kupata uhuru wake mnamo Desemba 9, 1961, tunakumbushwa juu ya safari ya kujitawala, mshikamano, na kujenga taifa lenye matumaini.

Ni siku ya kukumbuka juhudi za mashujaa wetu waliopigania uhuru kwa nia ya kuleta haki, usawa, na maendeleo kwa kila Mtanzania. Pia ni fursa ya kutathmini tulipotoka, tulipo, na tunakokwenda kama taifa linalothamini amani, umoja, na uzalendo.

🙌 Tusherehekee kwa kutenda haki, kuchapa kazi kwa bidii, na kusimamia misingi ya uhuru wetu. Pamoja tunaweza kujenga Tanzania tunayoitaka!
Jana ilikuwa ni kumbukumbu ya Pearl of harbour
 
Neno Tanganyika lilizikwa, likaota jina Tanzania. Labda tupige maombi ya kufa mtu lifufuke upya ling'ae kama TANGANYIKA.
 
Ujumbe kwa samia ni kuwa uhuru tulioupata kutoka kwa beberu hauna maana bora beberu lirudi kushika hatamu
 
Back
Top Bottom