Leo ijumaa SAA SITA mchana mitaa ya AMANI KILIMAHEWA BONDENI chini ya msikiti, vibaka wamemtolea mtu VISU nakuchukua hela na kuondoka

Leo ijumaa SAA SITA mchana mitaa ya AMANI KILIMAHEWA BONDENI chini ya msikiti, vibaka wamemtolea mtu VISU nakuchukua hela na kuondoka

zachariano alexido

Senior Member
Joined
Mar 10, 2026
Posts
178
Reaction score
460
Kwa macho yangu Leo ijumaa SAA SITA mchana mitaa ya AMANI KILIMAHEWA BONDENI chini ya msikiti, vibaka wamemtolea mtu VISU nakuchukua hela na kuondoka.

Nina muomba kiongozi mwenye dhamana ya USALAMA ZANZIBAR awajibike ziende fenda za polisi kukamata wale vijana WOTE wenye tattoo na wanao vuta bangi KILIMAHEWA BONDENI, HUKO tuendako watalii watajuta kwa nilicho kiona.

Hii SI mara ya KWANZA vibaka kufanya fujo mchana kweupe peeee, WAKIWA na silaha na bangi, mpaka niliuliza kazi ya sheha wa huku ni ipi au ni vijana wao? Je taarifa zilishaga fika polisi? Makundi ya vijana wenye silaha ni mengi sana sana
 
Wasalimie huko Jamuhuri ya kiislamu Ya Zanzibar.

Tambueni kuwa mlinikera sana mlipipoga marufuku ya uuzwaji wa pombe kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.
Mkuu pole sana naona ni utaratibu tu japo siamini kuwa POMBE haiuzwi mwezi ramadhan, ila haifai kuuzwa hadharani sana au ovyo, watalii MBONA wanapombeka tu kama kawa
 
Kule wanasema kila mtu ana mtu wake serikalini,ukimfunga mtoto wa fulani inapigwa simu moja tu tu kutoka majuu,madogo wanaendelea kutamba
Kaka hapo KILIMAHEWA BONDENI hutembei hatua kumi hija kita kundi la vijana wakivuta bangi mchana jua Kali, wakina mama wanachungulia tu masikini, nimeumia sana au huku HAMNA VIONGOZI WA ulinzi? Asee ukiishia stone town na DARAJANI UNAEZA SEMA pako shwari sogea huku kwengineko sasa
 
Mkuu pole sana naona ni utaratibu tu japo siamini kuwa POMBE haiuzwi mwezi ramadhan, ila haifai kuuzwa hadharani sana au ovyo, watalii MBONA wanapombeka tu kama kawa
Yule waziri alipiga marufuku huku akitoa kejeli kwa wasio waislamu.

Jamuhuri ya kiislamu Ya Zanzibar ni katili kuliko Jamuhuri ya kiislamu Ya Iran.
 
Hii ndio kazi tunayoiweza Wabongo, mtu akipata shida unakaa pembeni kupiga picha na kuja kuleta habari mtandaoni na sio kumsaidia
Kaka mi ni mgeni, juhudi nilizo onesha hujui tu, why Mimi mgeni unataka nifanye mkubwa? ilihali Kuna wazawa wapo hapo na wanaangalia, hakuna sheha? NASIKIA ni WATOTO wao hivo huleta UGUMU kumchukulia hatua, ila hawa vibaka mmoja alikua na tattoo usoni ana dreads rasi ana vaaga pensi na mlegezo, unafikiri kaka ninge fanya nini
 
Kaka hapo KILIMAHEWA BONDENI hutembei hatua kumi hija kita kundi la vijana wakivuta bangi mchana jua Kali, wakina mama wanachungulia tu masikini, nimeumia sana au huku HAMNA VIONGOZI WA ulinzi? Asee ukiishia stone town na DARAJANI UNAEZA SEMA pako shwari sogea huku kwengineko sasa
Kuna dada mmoja wa Arusha walimvamia hao vijana wa darajani,
Uyo dada akaleta uchuga chuga kwamba aiseh chalii yangu hapa hupati kitu.

Walichana chana mapanga ya kichwa.
Lakini wakazi wa eneo hilo waliitambua hao vijana na raia wakakausha,sababu yule dada ni mbongo labda

Lakini alipona na anafanya kazi uko uko Zenji uyo dada,hana furaha na wa zanzibar ni vile tu utafutaji umemuweka uko.

Stella laizer
 
Kaka huku kama huwezi jipambania MWENYEWE, sahau polisi kukulinda sahau, HUKO uswahilini watu wananyanganywa vitu hasa zanzibar isikie tu forodhani, DARAJANI kwisha huku kwingine kuwa MAKINI haswa
 
Uyo dada akaleta uchuga chuga kwamba aiseh chalii yangu hapa hupati kitu.

Walichana chana mapanga ya kichwa.
Lakini wakazi wa eneo hilo waliitambua hao vijana na raia wakakausha,sababu yule dada ni mbongo ata sijui kwanini.
Mkuu, kwa Maelezo haya ☝️ nikisema wewe ni miongoni mwa hao waliomchana chana huyo binti wa kichuga nitakuwa nimekuonea?

Maana unajua details zote kuhusu kilimchompata bibie huyo.
 
Back
Top Bottom