Leo kila mtu ataje sababu iliyomfanya akaachana na mpenzi wake wa zamani

Leo kila mtu ataje sababu iliyomfanya akaachana na mpenzi wake wa zamani

Mambo vipi watu wa Mungu?
Leo naomba kila mwana MMU ataje sababu iliyopelekea kuachana na mpenzi/wapenzi wake wa zamani.
Tukianza na mimi mleta mada niliachwa coz sikua msabato mwenzie na vile sikua mnyakyusa mwenzake. Na yeye sababu alizonipa kabla ya kanitema ni kwamba wazazi wake walikua wamemwambia wanataka aolewe na mwanaume msabato na vilevile awe mnyakyusa.
Ebu na nyie watu wa Mungu tiririkeni hapa sababu zilizopelekea mahusiano yenu kuvunjika.


Mie sikuachwa bali niliacha maana mwenzangu alizidi uchafu. Akija kunitembelea geto langu analikuta safi na linanukia harufu nzuri nzuri tu ya kumfanya mtu mchafu ajisikie vibaya. Yeye akija wala hashangai, anapangua vitabu vyote mezani na tukila utashangaa mchuzi atauacha unakaukia mezani na sakafuni. Wakati mwingine akija na zege (chips mayai) na kuku wake wa kukaanga, utashangaa atakula na kuacha pale mezani kwa wikendi yote yuko pale nami. Nilikuja kushangaa siku moja baada ya yeye kuondoka, nilifanya usafi wa nguvu nikakuta mifupa ya kuku chini ya kochi na handkerchief ya mafua ambayo ni yake pia. Ukimuona kwa macho ni kweli anavutia kinoma, wigi za kila aina anazo, na yuko smart katika kuji-keep uzuri ila uchafu tu ndiyo shida yake. Yaani yeye anajali kuonekana msafi tu na sijawahi kumuona anafua nguo hata siku moja. Yaani mpaka vitambaa vya kupangusia vumbi nilikuwa nafua mimi, yeye yuko bize kuchafua nyumba yangu bila haibu. Katika suala na kuweka papuchi clean huko ndio balaa, maana alikuwa na harufu ya fujo haswa baada ya tendo la ndoa. Samahani kama kuna anayekwazika na hili, ila nilishindwa ikabidi niongee na mdada mmoja ajifanye kuwa ndiye girl friend wangu mpya....yule mdada mchafu lipokuja nyumnai akakutana na mdada mpya wakakorofishana na akatimuliwa kisailensa mpaka leo anabaki kunitukana wakati mwenzie nina furaha ya kubaki lonely na usafi wangu.
 
Mimi msela alinichukulia alafu ni chalii wangu wa tokea utotoni asee.

Kumuuliza chalii siunajua huyu manzi ni wangu eroo? Akajibu

"Manzi kanikubali mwenyewe chalii"

Ikabidi nijikate tu alolo nikajiona fara ila manzi akaanzanga leta shobo baada ya muda nikaona huyu hajui kama mimi mkora!? nikamkata shavu kwa kumgonga rafiki yake wa karibu sana alipojua mpaka leo sijawahi kusikia pang'ang'a yoyote.
Alikuletea umbwira huyo chaliaraa....temana naye Bablai. [emoji23]
 
Back
Top Bottom