Leo mjanja nimekamatika, naona kama nimetapeliwa Tsh. Milioni 1

Wewe subiri Jumatatu uone kama watafungua. Ukienda polisi sasa hivi utapoteza muda bure.
Hata CRDB wameshauri hivyo, hiyo Kesho naisubiri Kwa hamu, ikifika sa4 hajafungua naenda kwenye Tawi la CRDB kuripoti tena, nikiona hakuna Masada naenda polisi
 
"Auna unjanja oote" mkuu kabla ya yote nenda bank u print bank statement inayoonyesha huo muamala kwanza utaweza kusaidia baadae wakianza kukupiga dana dana
 
Kutoa hela kwa wakala si salama sana japo Kuna mazingira yanakulazimu kufanya ivo!

Mimi Kuna wakala, brother fulani maeneo ya njia panda ya segerea niliwahi kwenda kwake kutoa hela!

Nikatoa mara ya kwanza mtandao ukagoma!

Nikarudia kutoa mara ya pili ikakubali ilikuwa ni laki 4 na 50

Zikapita wiki mbili .. Nikaenda ATM kutoa hela naambiwa hakuna hela!

Kuwapigia simu watu wa NMB wakaniambia siku Ile nilifanya miamala 2 kwa wakati mmoja!

Nilivyorudi kwa jamaa kumuelezea na kumtajia na tarehe akaona ni kweli akanirudishia hiyo fedha

Tola siku hiyo, nikiwa na miamala wa kufanya naenda kwake!
 
"Auna unjanja oote" mkuu kabla ya yote nenda bank u print bank statement inayoonyesha huo muamala kwanza utaweza kusaidia baadae wakianza kukupiga dana danau

"Auna unjanja oote" mkuu kabla ya yote nenda bank u print bank statement inayoonyesha huo muamala kwanza utaweza kusaidia baadae wakianza kukupiga dana dana
Unaongea nini wewe? Nimeshapiga simu customer care na wamethibitisha pesa imetoka Kwa wakala japo ilichelewa Kwa sababu za mtandao, wamesema nisubiri afungue nichukue pesa yangu, kama asiponipa Niwapigie niwape simu waongee nae, sasa wewe unaongelea nini hapa
 
Muaminifu huyo
 
Download simbanking uwe unatoa pesa bila kadi
ya bank.
 
Pole sana mkuu subiri afungue uchukue pesa yako
 
Simbanking app sio lazima namba ya simu uliyosajilia bank iwepo ukiwa na internet tu pesa inatoka
Nakuelewa, Yani Meseji baada ya kutoa pesa Kwa wakala inakuja Kwa sms sio kwenye app
 
Never, Tembea na RB mkuu akileta ujanja ujanja hio Kesho ita polisi kwa utaratibu weka mtu korokoroni...

Ushauri wangu ulishaokoa wengi na wanitumia sadaka kwa uaminifu mkubwa
 
Usipende kumpa wakala kadi yako, toa pesa kwa Token kwenye simu yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…