Kibunango
Platinum Member
- Aug 29, 2006
- 8,468
- 2,349
Ulinz wa Viongozi kwa kweli unatia kinyaa!
Ni kuanzia kwa rais wa Jamhuri ya Muungano hadi kwa rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Huu ulinzi wao umezidi mipaka, unatisha na wala haupo sambamba na hali halisi ya nchi yetu! Kumbuka tu tunasema kuwa nchi yetu ni ya amani na utulivu!
Tukiwa tuaendelea kuzindua hiyo Royal Tour huku viongozi wakiwa kwenye ulinzi mkubwa namna hiyo kushinda hata wa yule wa Ukraine, dunia hii itatuelewa vipi?
Kuna kipindi cha awamu ya kwanza kadhia hii ilipigwa marufuku. Awamu ile msafara ulifikia magari kumi... na ukakemewa hadi kurudi kwa magari matano
Leo msafara una magari 25 hadi 30 kwa Kiongozi mmoja! Tunajenga nchi au tunabomoa? Huu ni ufahari au ni ulimbukeni au ni dalili ya ukosefu wa ajira?
Hili limepigiwa kelele na wengi hapa kijiweni na ni vema tukapata ufafanuzi kwa nini hali hii ipo na inaendelea kukua! Mbona wakiwa nje ya nchi, ulinzi wao ni wakawaida tu!
Tukiwa katika hali ya sasa ya mfumko wa bei ni vema hao viongozi kuonyesha kweli nchi yetu ipo katika hali ngumu na sio hizo anasa wanazotuonyesha!