Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi Yale mabunduki yote yanakuwa na live ammunitions?Magari ya kumwaga,mafuta ya kumwagika-fulltanks na posho kibao kwa wasindikizaji.Nchi hii inaliwa na wenye meno.Awamu ya nne ndege ilikuwa inajaa hadi wazamiaji na kwa hiyo usiulize sana kwamba kwa sasa tunaongozwa na awamu ya ngapi mpaka unaona msafara una magari mengi, wanalamba asali huku wakipapaswa.
Kuna siku tutaongea lugha moja ...muda utaongeaTunawadai mambo mengi sana ndio maana wanajitenga ili tusipate nafasi ya kuwauliza.
Kwa mfano kwenye interview na Tido bado akatumia msafara within the premises za Ikulu.
Yaani ilishangaza mno.
A show of power before the people. Mkakati muhimu wa viongozi wetu ni "kutisha"; "kuogofya". Instil fear in the ruled. Wanajijengea "aura" ya kuogofya ili wananchi wajue hao sio binadamu wa kawaida kama wao. Unapofikiria kuwahoji inabidi kwanza uutizame msafara wake na kujihoji mara tatu tatu kuhusu huyo unayetaka kumkabili kama mnafanana. In reality wanajulisha umma kwamba hawako "acccessible" to any tom, dick and harry.Ulinz wa Viongozi kwa kweli unatia kinyaa!
Ni kuanzia kwa rais wa Jamhuri ya Muungano hadi kwa rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Huu ulinzi wao umezidi mipaka, unatisha na wala haupo sambamba na hali halisi ya nchi yetu! Kumbuka tu tunasema kuwa nchi yetu ni ya amani na utulivu!
Tukiwa tuaendelea kuzindua hiyo Royal Tour huku viongozi wakiwa kwenye ulinzi mkubwa namna hiyo kushinda hata wa yule wa Ukraine, dunia hii itatuelewa vipi?
Kuna kipindi cha awamu ya kwanza kadhia hii ilipigwa marufuku. Awamu ile msafara ulifikia magari kumi... na ukakemewa hadi kurudi kwa magari matano
Leo msafara una magari 25 hadi 30 kwa Kiongozi mmoja! Tunajenga nchi au tunabomoa? Huu ni ufahari au ni ulimbukeni au ni dalili ya ukosefu wa ajira?
Hili limepigiwa kelele na wengi hapa kijiweni na ni vema tukapata ufafanuzi kwa nini hali hii ipo na inaendelea kukua! Mbona wakiwa nje ya nchi, ulinzi wao ni wakawaida tu!
Tukiwa katika hali ya sasa ya mfumko wa bei ni vema hao viongozi kuonyesha kweli nchi yetu ipo katika hali ngumu na sio hizo anasa wanazotuonyesha!