Leo msafara una magari 25 hadi 30 kwa Kiongozi mmoja!

Nini tatizo hasa mkuu....

Una details zozote kuhusu usalama wa nchi hii
 
Urais ni taasisi, anafanya na kazi na taasisi na vyombo vingi kwa Wakati mmoja. Usidhani magari yote Yale ni walinzi tuu Kuna wasaidizi wa Rais wa Idara zingine
 
Awamu ya nne ndege ilikuwa inajaa hadi wazamiaji na kwa hiyo usiulize sana kwamba kwa sasa tunaongozwa na awamu ya ngapi mpaka unaona msafara una magari mengi, wanalamba asali huku wakipapaswa.
Hivi Yale mabunduki yote yanakuwa na live ammunitions?Magari ya kumwaga,mafuta ya kumwagika-fulltanks na posho kibao kwa wasindikizaji.Nchi hii inaliwa na wenye meno.
 
Tunawadai mambo mengi sana ndio maana wanajitenga ili tusipate nafasi ya kuwauliza.

Kwa mfano kwenye interview na Tido bado akatumia msafara within the premises za Ikulu.

Yaani ilishangaza mno.
Kuna siku tutaongea lugha moja ...muda utaongea
 
Ni uoga kutokana na dhuluma wanazozifanya dhidi ya wananchi.
 
A show of power before the people. Mkakati muhimu wa viongozi wetu ni "kutisha"; "kuogofya". Instil fear in the ruled. Wanajijengea "aura" ya kuogofya ili wananchi wajue hao sio binadamu wa kawaida kama wao. Unapofikiria kuwahoji inabidi kwanza uutizame msafara wake na kujihoji mara tatu tatu kuhusu huyo unayetaka kumkabili kama mnafanana. In reality wanajulisha umma kwamba hawako "acccessible" to any tom, dick and harry.

Tena hiyo misafara ni jeshi kamili na ulaji mzito kwa wapambe wa watawala. Ndio alama za banana republics hizo. Nenda kwenye nchi za francophone. Hata mawaziri na maCEO wa taasisi za umma wana misafara ya mikubwa ya wapambe yenye jeuri hasa.

Tafsiri ya uhuru kwa nchi za kiafrika ilikuwa kumbadili mkoloni wa kigeni ili Waafrika waliojanjaruka (enlightened) washike hatamu za ulaji na ubwana juu ya waafrika wenzao. Watu kama Nyerere waliokuwa na malengo ya dhati ya kuwakomboa wananchi wao kiuchumi, kielimu na kiafya, walikuwa exception. Walitegemea zaidi karisma kuliko "hofu" ingawa kuna mida walilazimika kutisha kiasi kutimiza malengo yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…