Leo nafanya interview Ubalozi wa Marekani kwa ajili ya viza

Watu wamejikatia tamaa wanatakakuwakatisha tamaa na wenzao,maisha popote.
 
Mkuu hapa JF kuna watu wa kila aina,wapo waliopo Bongo na wapo waliopo nje ya Bongo,kwa Dunia ya leo ni rahisi sana kwenda nchi yeyote ile na kutafuta riziki,

So,mtu akikwambia sijui yupo nchi fulani usichukulie kua ni jambo kubwa sana,ni kawaida tu,

Karibu hapa kwa Malkia tukomae na box.
 
Ishi na watu vizuri VISA haina interview
 
Unadhani wote ambao huwa wanaokoswa huwa hawamshawishi consular officer? wakati mwingine jitahida haizidi kudra Mkuu, ndio maana namuomba Mungu.
Mkuu umetumia gharama kiasi gani Hadi hapo ulipofika? Kwenye interview uliulizwa maswali gani? Na Ni visa ipo umepata.? Kama vip tusaidie njia ulizopita na sisi wengine wenye Nia tujue pa kuanzia ...
 
Mkuu umetumia gharama kiasi gani Hadi hapo ulipofika? Kwenye interview uliulizwa maswali gani? Na Ni visa ipo umepata.? Kama vip tusaidie njia ulizopita na sisi wengine wenye Nia tujue pa kuanzia ...
Mkuu OllaChuga Oc, ahsante kwa swali.

  • Visa niliyopata ni F1 - student Visa.
  • Hii ina gharama kubwa kuliko B1 na B2 ( Tourist & Business Visa).
Jumla ya gharama zote ni ngumu ku analyse
Maana si rahisi kukumbuka gharama ndogo ndogo kama, stationery, usafiri wa hapa na pale, kuandaa documents, internet nk.

Lakini gharama kubwa ambazo ni rahisi kuwa noted ni,

  • Application fee dollars 300 (kwa vyuo vitano nilivyoomba)
  • Visa Fee - Tsh 384000
  • Sevis Fee - Tsh 873000
  • Visa Insurance - 696000
  • WES - Dollars 220
  • English Proficiency Test ( Duolingo) - Dollar 45.

Maswali.

  • Kwanini ukasome USA sio Tanzania au nchi nyingine?
  • Nani atakulipia gharama za masomo na kwanini akulipie wewe na sio mwingine?
  • Sponsor wako anajishughulisha na nini?
  • Umekijuaje hicho chuo?.
  • Unatuhakikishiaje kuwa utarudi baada ya masomo?
  • Ni course gani ulizojisajili kwa ajili ya Program uliyoomba?

Baada ya hapo, YOUR VISA HAVE BEEN APPROVED.

Unapewa card ya rangi ya kijani hivi, yenye namba (namba imezungushiwa star [emoji93] nyekundu, karatasi ya kulipia visa insurance, (hapo hapo ndani kama una cash)

Cash points ni dirisha namba 4, (karibu na sehemu ya kukaa watoto).
 
Uko positive sana Mkuu.
 
Watu wamejikatia tamaa wanatakakuwakatisha tamaa na wenzao,maisha popote.
Yaani kuna jamaa alianza kuniambia mambo ambayo hadi sasa hivi najiuliza kama hiyo roho anayo mtu anayekujua vizuri anakuua kabisa.

Nilichojifunza tu ni kuwa sitakuwa naweka masuala binafsi mtandaoni, ni kukaribisha roho za kishetani tu maishani.

Niliweka ili tu niweze kupata usaidizi na ushauri kutoka kwa wajuzi wa mambo, ili kupata insight ya kupambana,ila matokeo yake mtu anakuandikia.

  • UNAENDA UTUMWANI UNAONA SIFA.
  • UTAKUFA NJAA HUKO
  • UTARUDI NA MAKOBAZI HUTAFANIKIWA
  • UTARUDI KAMA ULIVYOKWENDA.
  • UNATUANDIKIA MAREKANI UNADHANI NI MBINGUNI.
  • UNATAKA SIFA, NK.
  • CHUKUA MIFAGIO YA KUZOLEA MAVI YA WAZUNGU.

Ina discourage sana, anyway tuishi.
 
Point[emoji1666]
 
Huyo huyo ndio kaa approve mkuu,anapenda kuwa window 3, black sura nzuri kiasi nyembamba, mwembamba pia, kama mnyarwanda hivi, namshukuru Mungu.

Window 2 alikuwa, Mzungu wa kiume, mrefu, mwenye upara mtu wa makamo.

Window 1, nilifanya fingerprint, kuna mdada mswahili,mnene kiasi, maji ya kunde,na ku submit passport na Ds 160 printed page, na picha moja yenye white background.

Window 4, nikalipia cash ( Visa Insurance) karibu na screen mwisho wa ukumbi, (Sehemu ya kukaa na kucheza watoto).
 
Kwanza mi nikupongeze kwa hatua uliyofikia na Mungu azidi kukuongoza na kukupa hitaji la moyo wako. Kingine achana na hao roho nyeusi na mbaya wapo kwa ajili ya kukatisha watu tamaa na kutopenda wengine wapige hatua. Kila la kheri Mkuu.
 
Ahsante kwa ushauri bora kabisa, Mungu akubariki sana.
 
Siwazingatii mkuu, nashukuru sana.
 
Hongera Sana chief Mungu azidi kukupigania
 
Allah akujaalie kheri,



Jf kuna wachawi wengi makonkodi,

Rana yao kuona umeleta uzi wa kuomba msaada,halafu wao wanajivisha ngozi ya kondoo na Kufariji/pole nyingi za kinafiki.
Jana nimeamini humu ndani kuna watu wa ajabu mno, jambo la kuomba visa na kupata ni jambo la kawaida kabisa, me sio wa kwanza kupata wala sitakuwa wa mwisho.
Me kupata sitaziba ridhiki aliyoandikiwa mja kwa namna yoyote ile, ila jana nimeshangaa watu wananitolea hadi MATUSI na maneno ya LAANA,sijui kosa ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…