Leo nafanya interview Ubalozi wa Marekani kwa ajili ya viza

Leo nafanya interview Ubalozi wa Marekani kwa ajili ya viza

Mkuu ahsante sana kwa moyo wako mwema, umenisaidia sana tangu mwanzo hadi hapa nilipofikia, ubarikiwe maradufu, natambua msaada wako kwangu.
Mungu akutangulie usisahau kusaidia na wengine, sio lazima mpaka mtu umjuwe.
Wewe tumepeana moyo tu hapa mtandaoni lakini wapo tulioshikana mkono Leo wametobowa wameaota maoembe, ila Mungu ni mwema na Mimi si haba siko vibaya.
 
Salamu wakuu,

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, nikihangaikia suala la kutoka huku nchini kwetu kwenda Marekani, hatimaye leo ndio siku yenyewe ya kujua mbivu na mbichi. Nitakuwa ubalozini kwa ajili ya visa interview saa tatu na dakika 45 asubuhi hii.

Namuomba sana Mwenyezi Mungu anifanikishe katika jambo hili, niombeni pia rafiki zangu, nitaleta mrejesho.

Wasalaam.
Allah kakubariki kwenda Amerikiya siyo Jeddah, Mecca au Riyadh.
 
Salamu kwenu nyote.

Awali ya yote napenda kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha tangu naanza hizi harakati hadi leo nimefika mwisho wake na kufanikiwa.

Pili, nawashukuru wachangiaji wote hapa JF walionipa support (kwa njia ya ushauri) kuhusu jinsi gani naweza kufanikisha adhma yangu, Mungu awabariki sana (kwenu nyote mnaoamini uwepo wake na utendaji kazi wake).

Binafsi nina furaha ya pekee sana, nimefanya interview na visa yangu ime be approved, kesho saa nane kamili mchana nitakwenda kuchukua tayari kwa kuanza maandalizi ya safari hivi karibuni.

Mwisho kabisa, nawashukuruni nyote mlioniombea, mlionikejeri na kunikatisha tamaa, mmenipa nguvu kwa namna moja ama nyingine.

Nimelizie kwa kuwakaribisha nyote mlio na mlengo kama wangu, kwa ushauri namna gani mnaweza fanikiwa pia.

Wabillah tawfiq.
Takbir! Allah amekujalia kuingia Amerikiya. Baada ya hapo ni ahera na bikra 72. Mecca, Jeddah, na Riyadh Allah hataki uende.
 
Salamu kwenu nyote.

Awali ya yote napenda kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha tangu naanza hizi harakati hadi leo nimefika mwisho wake na kufanikiwa.

Pili, nawashukuru wachangiaji wote hapa JF walionipa support (kwa njia ya ushauri) kuhusu jinsi gani naweza kufanikisha adhma yangu, Mungu awabariki sana (kwenu nyote mnaoamini uwepo wake na utendaji kazi wake).

Binafsi nina furaha ya pekee sana, nimefanya interview na visa yangu ime be approved, kesho saa nane kamili mchana nitakwenda kuchukua tayari kwa kuanza maandalizi ya safari hivi karibuni.

Mwisho kabisa, nawashukuruni nyote mlioniombea, mlionikejeri na kunikatisha tamaa, mmenipa nguvu kwa namna moja ama nyingine.

Nimelizie kwa kuwakaribisha nyote mlio na mlengo kama wangu, kwa ushauri namna gani mnaweza fanikiwa pia.

Wabillah tawfiq.
Barikiwa sana nilikuwa na imani utapata Maana Mungu yupo pamoja na wewe karibu siku moja moja Canada.
 
Mkuu ulipitia hatua zipi maana mimi mpaka nimechoka, VISA ni ngumu kuliko mashart ya kuiona pepo
Mkuu angalia post zangu zinafuatana Kaka, wazo, colleges application , admission, visa application, sevis fee, interview, visa.
 
Back
Top Bottom