Leo nafanya interview Ubalozi wa Marekani kwa ajili ya viza

Leo nafanya interview Ubalozi wa Marekani kwa ajili ya viza

Mungu akutangulie usisahau kusaidia na wengine, sio lazima mpaka mtu umjuwe.
Wewe tumepeana moyo tu hapa mtandaoni lakini wapo tulioshikana mkono Leo wametobowa wameaota maoembe, ila Mungu ni mwema na Mimi si haba siko vibaya.
Shukrani sana, nitafanya hivyo, na daima nimekuwa nafanya hivyo mkuu
 
Hongera sana mkuu, Mungu akutangulie.
Siku nikikwama nitakutafuta unipe hint za taarifa nitakazo hitaji. All the best mkuu!
 
Huu uzi unaonyesha jinsi gani watanzania ni wanafiki na wenye roho mbaya, yaani mtu hata humjui lakini unaanza kuonyesha chuki za wazi kisa safari ya hapo marekani?
Mtu aliyefanikiwa kukuzidi hutakiwi kumponda bali unatakiwa kujifunza kutoka kwake.

Ndio maana watanzania wengi ni masikini sababu ya chuki na roho mbaya.
Hivyo vitu viko ndani kabisa ya DNA za watanzania wengi.
 
Salamu wakuu,

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, nikihangaikia suala la kutoka huku nchini kwetu kwenda Marekani, hatimaye leo ndio siku yenyewe ya kujua mbivu na mbichi. Nitakuwa ubalozini kwa ajili ya visa interview saa tatu na dakika 45 asubuhi hii.

Namuomba sana Mwenyezi Mungu anifanikishe katika jambo hili, niombeni pia rafiki zangu, nitaleta mrejesho.

Wasalaam.
Mm Nina lottery yangu imbayo inanidirect interview JANUARY .ulivyopata ujuui tu umenitia nguvu mno...nawezaje kwenda kwenye interview bila ya kuwa na consent ya mzazi mmoja juu ya watoto kuruhusu kuondoka bila yeye kujua
 
All the best Bro
Usijali hivi vibwengo vinavyotapatapa, sijui utumwa sijui kuna hela bongo wakati venyewe ukiviangalia ni choka mbaya mbovu... kutwa kushinda humu JF...
Na kuna kimoja kinaoneka ni kizee `kweli kipo humuJF toka 19kweusi kina wanga kwenye kila siredi...
Vita mbele, ushawaacha wala vumbi....
 
Kila la kheri mkuu usisikilize negative comments, chukua zile positive tu alafu zifanyie kazi. Simamia lengo kuu linalokupeleka USA, kuwa na nidhamu katika mambo yote (socially, economically n.k). Pia usisahau ulipotoka, iogope kesho yako na mshirikishe Mungu katika mambo yako.
 
Moja ya kinachofurahisha Jf ni ukianzisha uzi kuhusu nchi yoyote na wachangiaji watajidai wako huko huko hata kama wengi sio kweli.

Utasikia, karibu sana huku Marekani. Mara mwingine atasema, kwa kweli kwa sisi tunaoishi hapa Landani Uingereza hilo suala tunalikubali. Na hata wapo watakaokwambia huko Bongo mnateseka sana, karibuni huku falme za kiarabu.
 
Salamu wakuu,

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, nikihangaikia suala la kutoka huku nchini kwetu kwenda Marekani, hatimaye leo ndio siku yenyewe ya kujua mbivu na mbichi. Nitakuwa ubalozini kwa ajili ya visa interview saa tatu na dakika 45 asubuhi hii.

Namuomba sana Mwenyezi Mungu anifanikishe katika jambo hili, niombeni pia rafiki zangu, nitaleta mrejesho.

Wasalaam.

Mzee baba kwanza hongera kwa uthubutu! Sema umeenda muda mbaya sana! Pale kuna consolar mmoja tu dirishani ambaye ni mdada black america. Ana roho mbaya sijawahi pata kuona yaani sijui kama utatoboa. Kulikuwa na mama wa kizungu pale sema karudi kwao yule ndo alikuwa poa sana wengi walikuwa wanapewa tu Visa. Ila yule dada wa kimatumbi ana roho ya mwendazake! Walah ukipata wewe kidume. Ukuje utuletee mrejesho hapa.
 
Ukitaka kumpatia mzungu akupe viza yake ki rahisi,wwe cheza na documents tu, angalia ni documents gani wanazitaka kwa ajili ya safari yako kwenye web zao zinakuwepo! Mtalii ana documents zake, mfanyabiashara pia na Wanafunzi nao kuna aina ya documents zao za kiwanafunzi! Sababu ya safari yako ndiyo itakuelekeza ni documents gani ukusanye!!
 
Back
Top Bottom