Asprin
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 68,223
- 96,083
Mwajuma, jiwe moja tunaweza kupikia chakula (Hapana bibi).
Mwajuma, mawe mawili twaweza kupikia chakula (Hapana bibi).
Mwajuma, Mawe matatu twaweza kupikia chakula ( Ndiyo bibi, chungu kitakaa).
FL1, sasa inabidi uwe na mawe matatu. Moja tayari ni mume wako, la pili ni bwana wa kukupa pesa mkikwama ndani na wa tatu incase mumeo akikuacha, basi jamaa anakudaka haraka sana.
Haya, ngoja Masa na kundi lake wakuchezee ngoma ya kikwao ya CHAGULAGA yaani "Chagulaga mwana Mayu". Itabidi tu uchague wawili ili YAISHE......... Mumeo itabidi tu avumilie maana ndiyo DIGITAL LOVE umeianzisha.......
Mwenye pesa? Pesa hapa ni nyumbani kwake. Na ndicho alichonipendea kama ulikuwa hujajua.