Leo naomba mniulize chochote kuhusu mimi

Leo naomba mniulize chochote kuhusu mimi

Funzadume ni jina nilijipa na ninaitwa Funzadume mwana wa Washawasha. Nilijiita hivyo baada ya mzee wangu kujipa aka ya washawasha ndio mie ili kwenda nae sawa nikajiita funzadume

Mie sijihusishi na siasa kabisa
Shabiki wa Arsenal na Simba
Game ya leo na Wolves nahisi itakua ngumu kutokana na Ramsey na Xhaka kutokuepo.

Unatamani tutumie formation gani kuwazuia Wolves na kujipatia ushindi hapo hapo tuzibe udhaifu wa Guendouz, Mustafi na Elneny?
 
....Inasemekana...1996 hesabu yake ilikuwa tata sana. Kama una Pass ya mwaka huo kwenye hesabu jione mshindi.
Uko sahihi kabisa.

Naikubali sana system ya zamani, hasa kuanzia 1998 kurudi nyuma, pepa zao zilikuwa zimesimama sana, ndio maana waliokuwa wanafaulu walikuwa wanafaulu kweli(yaani walikuwa majembe).

Hata pepa za shule ya msingi zilikuwa imara san miaka hiyo.
 
Kwa mfano ungekua umesomea kozi ambayo haiajiriki halafu hauna namna ya kupata mtaji ungefanyaje ili kujikwamua kiuchumi?
Mimi licha ya kuajiriwa ninafanya shughuli nyingine ambazo zinaingiza kipato Zaidi ya ajira ninafuga kuku wa nyama, nina mabwawa ya samaki na nina mashamba. Ninachoweza kushauri ni kwamba anza kuwa na wazo la biashara au kilimo ndio utafute mtaji wake tena kwa kuanza kidogo kidogo sio lazima uwe na mamilioni cha muhimu ni wazo. Usipokuwa na wazo unaweza kujikuta unanunua simu ya laki nane kumbe hiyo laki 8 ndio ingekufanya kuwa Tajiri kama ungenunua heka mbili za shamba nje ya mji.

Halafu vijana nawashauri mjitume katika kutafuta mitaji haswa kwa kuangalia fursa zilizopo maeneo ya vijijini hii nchi ni Tajiri sana na ni rahisi kutoka. Naomba nikuulize kijana kama unakaa nyumbani huna kazi na mzazi wako ana eneo la medium density kwa nini usisaidie hata kulima mbogamboga katika njia za kisasa kama za kuweka miche kwenye mifuko na ukawakomboa wazazi zidi ya gharama za mboga nyanya nk. Ukienda China unakuta watu wanafanya hivyo mijini ila huku mtu anakaa Kitunda maeneo kibao anashinda insta tu . Tubadilike
 
Back
Top Bottom