Leo ndio nimejua kwanini wanawake wanajiingiza katika tabia za udangaji

Leo ndio nimejua kwanini wanawake wanajiingiza katika tabia za udangaji

Hapa nilipo nina majonzi, roho imeniuma sana kwa kuzaliwa kwenye familia maskini

Ipo hivi mimi kwetu ndio wa mwisho msichana peke yangu kati ya watoto 6.. Mzee wangu alitangulia mbele za haki hivyo tumebaki na mama tu.. hao ndugu zangu wote hawana maisha ya kueleweka isipokuwa mmoja tu angalau yeye ameajiliwa serikalini ndio kidogo anaibeba familia, yeye ameshaoa ana familia yake

Mimi nimeshahitimu chuo nina kama Miaka miwili nyumbani.. nimepata sehemu ya kujishikiza wananilipa 250000.. Kwetu ni bunju nafanyia kazi magomeni kila siku natumia 5000 yaani 3000 nauli 2000 nakula mchana hapo Ndio najibana mno..

Sasa kwasasa Hivi nyumbani Hakuna mtu nipo peke yangu mama ameenda kijijini kwao bibi anaumwa, mama yangu hana kazi ile ya kumtegemea anauza chupa za maji hivyo siwezi kumsumbua kwa chochote, amesafiri hajaniachia hata shilingi 100.. Hakuna chakula ndani Hakuna chochote, nachofanya nikitoka kazini nashukia kwa brother nakuta wamepika nakula naondoka

Leo nimeumia sana sijaenda kazini Nina siku 2 sina nauli hela niliokuwa nayo akiba imeisha nimemuomba bro kasema yeye hana hela hawezi kuwa anatoa hela mara mbili mbili kwa familia yake na kwangu, Kama niliweza kutafuta kazi basi nijitegemee nauli nikitaka kula nije nyumbani,, nikamuuliza sasa nitatoa wapi na Ndio naanza kazi akanijibu nitajua mwenyewe

Hiyo kauli imeniuma yaani anamaana gani kusema nipambane nitafute nauli yaani naitafutia wapi ..

Leo nimeacha kuwa judge Watu na maisha wanayoishi Kama ndugu yangu wa damu ananiambia maneno haya hao wa nnje watanijibu vipi


Ni hayo tu wakuu
Ila wanawake sijui mkoje yaani ukikumbwa na changamoto kidogo unachowaza ni kuuza kei. Sio fair naamini hapo hapo ofisini kwako kuna wafanya usafi na walinzi huenda wanalipwa 150,000 ila hawajawaza kujiuza. Kama una uhakika wa chakula kwa kaka yako huoni ni sapport kubwa sana aisee!
 
Ila wanawake sijui mkoje yaani ukikumbwa na changamoto kidogo unachowaza ni kuuza kei. Sio fair naamini hapo hapo ofisini kwako kuna wafanya usafi na walinzi huenda wanalipwa 150,000 ila hawajawaza kujiuza. Kama una uhakika wa chakula kwa kaka yako huoni ni sapport kubwa sana aisee!

Boss nauli ndio changamoto
 
Wako wadada hawapokei hata hiyo 250k na wanatembeza mihogo na karanga na wana watoto na familia na maisha yanasonga! Kudanga siyo na haijawahi kuwa excuse!

Sijasema kuwa nitadanga wakati mwinginee kila kitu kuna yumba pia nyuma ya biashara ya mtu kuna mengi yanaendelea mimi nina marafiki wanauza chakula ila bado wana danga
 
Shida ni kuwa unafikiri watu wote wenye changamoto basi wanazichukulia changamoto zao Kama wewe unavozichukulia

Mkuu dunia ina watu wengi na tupo tofauti katika kukabiliana na changamoto… shida nimepitia nyingi sana ila hii imenifanya kuomba ushaurii

Kuwa positive sio kila nyuzi unaona ni chai
Hizo scamming method za kutumia public sympathy nimezishuhudia sana kwa watu wengi. Wewe utawapiga wajinga wenzako, ila wengi huwapati.
 
Kwa nn huyu dada swali la amesomea nn analikwepa, tafadhali watu sitisheni hiyo miamala mpaka aseme nn kasomea isije kuwa watu tunapigwa hapa........akisema kasomea nn pengine wadau twaweza mpatia hata ofa ya kazi nzuri zaidi.
Kazi zingine sio mpaka uwe umesomea boya wewe! Labda atakuwa muhudumu wa gesti au yupo kiwandani, nk.
 
Niwakumbushe tu ndugu wajumbe huyu mleta mada alishwah kuja na uzi wa kusema amechoka kuwa SIDE CHICK anataka kuwa MAIN CHICK
ephen_ nimekaa kwenye matumizi ya internet kwa muda mrefu kidogo kuliko wewe, niamini mimi huyu mtu ni scammer. Kama unafatiliaga visa vyake ambavyo vingi kashavifuta na hata hiki i know atakifuta, you will just land yourself to the same conclusion.
 
Sijasema kuwa nitadanga wakati mwinginee kila kitu kuna yumba pia nyuma ya biashara ya mtu kuna mengi yanaendelea mimi nina marafiki wanauza chakula ila bado wana danga
Kikubwa ni kutambua kwamba changamoto ni sehemu ya maisha, ili ufanikiwe changamoto haziepukiki. Namna unavyochagua kukabiliana na changamoto hizo ndizo zitatoa uelekeo wa maisha yako.
 
Back
Top Bottom