#COVID19 Leo ndo nimeamini COVID-19 ni hatari

#COVID19 Leo ndo nimeamini COVID-19 ni hatari

Ili uamini zaidi, kuwa COVID-19 ipo na inauwa fika mortuary za KCMC na Mawenzi hospital Mkoa wa Kilimanjaro.
Kuna tatizo la suspects wa corona kuwaita moja kwa moja kuwa ni wagonjwa wa corona, hili nimeliona kwenye ile clip ya Mama Samia alipoogopa kuingia kwenye wodi ya wagonjwa wenye matatizo ya kupumua ambapo kuna suspect ila sisi huku tukapitisha kuwa ni wodi ya wagonjwa wa corona.
 
Nilikuwa nachukulia poa hii kitu. Yaani kuvaa barakoa na kunawa sijui mikono ilikuwa ni mpaka nione kuna ulazima au kulazimishwa.

Mfano nikienda hospital ni mpaka nione watu hawaruhusiwi kuingia bila barakoa ndo na mimi nitanunua na kuvaa. Ila sasa yaliyotokea leo ndugu zangu nimenyoosha mikono juu. Yaani nimepigiwa simu jana saa nne usiku naambiwa mama yako mkubwa anaumwa kifua kimembana na vichomi tunampeleka hospitali, nikachukulia kawaida tu. Kufika saa saba na nusu usiku watu wanapiga simu wanalia amefariki.

Nimefika msibani tena naambiwa watoto wake wawili wamelazwa hospitali wapo hoi kwa tatizo hilo hilo la vifua kubana na vichomi. Aise ikabidi nitoke kimya kimya kwanza kwenda kununua barakoa za kutosha na groves kabisa maana ni hatari.

Covid ipo ndugu zangu ni hatari na inaua ghafla ghafla kabla hata hujatubu dhambi zako.

Take care chukua tahadhari.
Nani kakuambia ni covid? Mbona mnakuza mambo nyie mtaimba nyimbo za mabeberu mpaka lini
 
Kwa kweli ugonjwa huu unatisha. Nina mtu wa karibu ameuumwa anakaribia kupona lakini dah ilikua changamoto kufika kumuona alivyoteseka. Babati tuna facilities nyingi za hospitali Kama oxygen na daktari. Pia tumechanganya Tiba ya dawa asilia, chakula na vidonge vya hospitali. Tuchukue tahadhari Ila tule vyakula Kama mbigamboga na matundaa kwa wingi
 
Back
Top Bottom