Leo ni kumbukumbu ya kifo cha Nyerere au Magufuli?

Hili taifa halina uongozi kabisa

Sijui hata vyombo vya ulinzi na usalama wa taifa vinafanya Nini !!

Hizi aibu Nani anabeba?
Hawa watu wamechanganyikiwa. Nafikiri kuna siri kubwa(password) kafa nayo bila kuwaachia sasa wanahaha Kila Kona. Kuna Sanduku la shaba liko pale jengo jeupe wakuu wameshindwa kulifungua. Password yake aliyekuwa anafahamu ni Jiwe pekee.[emoji2960][emoji2960]
 
Unashangazwaje kwa ufafanuzi ambao umekwisha kutolewa?!!!

Wameamua kuuzima mwenge Chato kwa ajili ya pia kumkumbuka hayati JPM....

HASTA LA VICTORIA EL COMANDANTE JKN🙏
Akili zako hazina akili au makusudi tu..?!
 
Nyerere Day inahusiana vipi na vyombo vya ulinzi na usalama?
Ndio maana mlivyo wapumbavu sherehe za Uhuru uwa zinaharishwa mnashangilia !!

Huwezi kunielewa Kama umeona kilichofanyika Leo na TISS wapo ni sawa!!
 
mkuu kama kutoa maoni yako hadi ulipwe, basi kuna shida mahali

sisi wengine tuko huru kidogo.
Upo Ukweli watu wanaolipwa humu kutetea UOZO wewe ni mmoja wapo. Hii mada inatia simanzi sana jinsi Mwalimu Nyerere alivyokosewa adabu leo. Siku ya Magufuli ni March 17. Inakuwaje CCM wamkosee adabu Mwalimu?
 
Mtateseka sana, heshima ya JPM ni kubwa!
Baada ya Nyerere ni JPM Tanzania!
Hawa akina Kikwete hata wakifa leo, kumbukumbu yake ilishafutika
Ni kweli mmemtesa mama Maria Nyerere, anajisikia vibaya kwa haya yaliyotokea leo. Rais Samia ana washauri wa hovyo kabisa, hata hivyo, na yeye amepokeaje USHAURI wa KIPUUZI kama huu wa kudhalilisha siku ya Mwalimu? Magufuli ana yake March 17, siyo hii ya leo ambayo imetumika kudhalilisha Mwalimu.
 
Usikufuru! Magufuli alikuwa mbadala wa Nyerere!! Ulimfahamu Nyerere? Mambo mengi aliyoyafanya marehememu Magufuli, ni yale ambayo Mwalimu aliyakaripia vikali.

Mwalimu alisisitiza sana kuheshimu katiba na sheria. Alisisitiza watu, na hasa vijana, kuwa jeuri na kukemea viongozi wanapopotoka. Alilaani sana udikteta. Na alisisitiza maamuzi kufanywa na vikao na siyo mtu mmoja kwa utashi wake binafsi. Haya yote ni kinyume kabisa na matendo ya marehemu Magufuli.
 
Usiendeleze UJINGA. Kama ni mwenge ungezimwa Butiama. CCM wamekosa adabu kwa Baba wa Taifa kumpora siku yake kumpa Magufuli, ni ukosefu wa adabu kwa Mwalimu.
mwenge huzimwa butiama kila mwaka?

kwahiyo kwa mujibu wako leo ilikua siku ya magufuri?
 
Nyerere mdogo wake Magufuli! Kumbe wote walifariki leo!
 
mwenge huzimwa butiama kila mwaka?

kwahiyo kwa mujibu wako leo ilikua siku ya magufuri?
Kama mwenge siyo lazima uzimwe Butiama, basi ungezimwa Chato ,lakini viongozi kuanzia Rais wangekuwa Butiama kuweka mashada, Kama ishara ya kuheshimu Nyerere day. Wamemwacha mama Maria peke yake mashada wanaweka kwa Magufuli! Mwalimu amekosewa adabu.
 
Kama mwenge siyo lazima uzimwe Butiama, basi ungezimwa Chato ,lakini viongozi kuanzia Rais wangekuwa Butiama kuweka mashada, Kama ishara ya kuheshimu Nyerere day. Wamemwacha mama Maria peke yake mashada wanaweka kwa Magufuli! Mwalimu amekosewa adabu.
hueleweki.
 
Sidhani kama kuna mtu atakayeweza kumfanya Magufuli asikumbukwe. Imepita miaka mingapi tangu Hitler atoweke, lakini Wajerumani, kwa uovu ule alioufanya, bado wanamkumbuka.

Mtu aliyeteka watu, kuwapoteza, kuua, kuwashambulia watu kwa risasi, kuwabambikia watu kesi za uhujumu uchumi, kuwatenga na kuwapendelea watu kwa misingi ya ukabila na kanda, atawezaje kusahaulika kiurahisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…