Leo ni kumbukumbu ya kifo cha Nyerere au Magufuli?

Acheni kujizungusha Nyerere day ni Nyerere day na Magufuli day ni Magufuli day, kusema eti wamekwenda Chato kwa kuwa Magufuli alimuenzi Nyerere ni kutufanya wote wajinga.
 
Nilijua wataenda butiama

Utawajua kwa matendo yao.

Bora wangepeleza hizo sherehe za matambiko yao ya mwenge huko butiama
 
Huna ushahidi wowote ule bali kuropoka Jamii Forum, shukuru kuna watu wameliwezesha hilo la wewe kupayuka.
 
siku ya pasaka hua unaenda kwenye kaburi la yesu?

nijuavyo, nyerere day hua tunasherehekea maisha ya nyerere so inaweza kua popote.
Yesu hakufa, hakuzikwa.
Alishuka kuzimu na kufufuka siku ya tatu baada ya hapo alipaa mbinguni so hakuna kaburi lake hapa Duniani. Kuhusu Nyerere day yes nakuunga mkono tunasherehekea maisha ya Mwalim na siyo lazima iwe Butiama.
 
Mtu aliyeteka watu, kuwapoteza, kuua, kuwashambulia watu kwa risasi, kuwabambikia watu kesi za uhujumu uchumi, kuwatenga na kuwapendelea watu kwa misingi ya ukabila na kanda, atawezaje kusahaulika kiurahisi?
kama wewe ni mtanzania na una akili timamu, naomba unitajie raisi ambae hakufanya ulichoandika hapa.
 
Huna ushahidi wowote ule bali kuropoka Jamii Forum, shukuru kuna watu wameliwezesha hilo la wewe kupayuka.
Je, hayo hayakufanyika? Yalifanyika chini ya utawala wa nani? Kuna hatua zozote uliona zilichukuliwa?

Huna hata logical reasoning?
 
Nimeshangaa sana, wamefanya kitu kizuri lakini sio sehemu sahihi
 
Acha upuuzi hilo dhalimu haliwezi kuwa mbadala wa Nyerere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…