Leo nimefurahi sana kumsikia Tundu Lissu akisema yale ambayo nimekuwa nikiyasema kwa miaka mingi!

Endeleeni kumpa moyo kwenye hizo harakati zake za kukimaliza chama chake. Wazee wenye umri kama wa Mbowe na Wasira anawataka wapumzike nyumbani kulea wajukuu. Lakini hapo hapo amemwomba Mzee Warioba agombee uraisi kupitia chama cha chadema 2025 ili yeye akagombee ubunge huko Singida aweze kuwa KUB
 
Mass mobilization halafu nini kinafuata baada ya hapo?

Kuwashawishi wananchi wengi kutokushiriki uchaguzi kwa sababu A, B, C, n.k, hiyo si sehemu ya mass mobilization?
 
Umeongea ukweli mchungu sana
 
Ungejiita tu Dr. Kilaza. Nani kakwambia Lissu alienda kumuomba Warioba agombee urais? Hivi huko CCM mnafuga funza vichwani mwenu?
 
Mass mobilization halafu nini kinafuata baada ya hapo?

Kuwashawishi wananchi wengi kutokushiriki uchaguzi kwa sababu A, B, C, n.k, hiyo si sehemu ya mass mobilization?
Sawa. Lakini hivi kuna quorum ya uchaguzi? Kuwa wakipiga kura watu pungufu ya hapa uchaguzi utakuwa batili? Ma utawashawishi vipi wanachama, mashabiki, watumishi wa umma kutoshiriki uchaguzi?
Mimi nadhani ni kuwashawishi wananchi kupigania uamuzi wao uheshimiwe. Nchi zote za jirani mabadiliko yalitokea baada ya wananchi kuchoka kudhulumiwa. Kama hawajachoka itakuwa kama kumpigia gigaa mbuzi. Hali haitabadilika.

Amandla...
 
hawezi kuhadaa watu kwama ana mkutano nao, kumbe anataka kuomba kuchangiwa pesa tu,

afanye kazi, ataomba kuchangiwa mpaka lini kibaraka asie na aibu huyo?
Kuna sheria iliyotungwa kama mtu asichangiwe ewe mtafiti???
 
Ungejiita tu Dr. Kilaza. Nani kakwambia Lissu alienda kumuomba Warioba agombee urais? Hivi huko CCM mnafuga funza vichwani mwenu?
Wewe usiye na funza kichwani mwako, unadhani alienda kumuona Mzee Warioba kwa jambo gani? Warioba ni mzee kuliko Wasira na Tundu Lissu alishasema hadharani kuwa wazee wa aina hii hawana cho chote kipya cha maana hapa duniani cha kujifunza toka kwao. Kwamba wanapaswa kutulia tu nyumbani kulea vijukuu na vitukuu wakisubiri kifo chao ambacho kimeshafika mlangoni.

Alishasema hata wazee wa umri kama wa Mbowe (63 years sawa na wa Samia) nao wameshapitwa na wakati, wanapaswa kutulia nyumbani kulea vijukuu. Yaani kwake (Tundu Lissu) jukumu la kulea watoto siyo la baba wala mama bali ni jukumu la babu na bibi. Bila shaka yeye alilelewa na babu na bibi, ndiyo maana akili yake iko hivyo ya kifyatufyatu. Baadhi ya wafuasi wake wenye funza vichwani mwao wanamwamini anachokisema na hivyo wakampumzisha Mbowe kwa sababu ya uzee. Akili zao haziwezi kuona kwamba, 'There will be no reform but election is a must. Hence after the election there will be no chadema and peace shall prevail'.

Akili zao haziwaelekezi kuwa reform zinafanywa bungeni na wabunge wetu ambao ndiyo wawakilishi wetu tuliowachagua kupitia uchaguzi mkuu. Hakuna mtu mwingine yo yote wa kufanya reforms hizo za sheria, ni wabunge wetu pekee. Hata rais wetu au spika wa bunge letu hana mamlaka hayo.

Akili zao zenye funza hazioni kuwa ili hzo reforms wanazozitaka ziweze kufanyika, hatua ya kwanza ni chama chao kipate wabunge wengi zaidi ya wale wa ccm ili hoja yao iweze kufanikiwa huko bungeni. Kwani huko bungeni maamuzi hufanyika kura. Ni maamuzi ya wengi wape. The winner takes it all. Hakuna cha nusu mkate. This is what is meant by the word democracy. It is the rule of the majority through their representatives in the Parliament.

Akili zao zenye funza zinaamini kuwa democracy is the rule of the minority through maandamano, matusi, harakati na sarakati mitaani. After the 2025 general elections, hakitakuwa na muwakilishi hata mmoja bungeni huku wakitegemea wabunge wa ccm wawafanyie hayo mabadiliko ya sheria wanayotaka. Eti watatumia nguvu kama zile za M23 wakisaidiwa na hivyo vikundi wanavyovitumikia kutoka baadhi ya nchi za ulaya magharbi hususani Ubelgiji na Ujerumani kwa akina Robertson.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…