Leo nimefurahi sana kumsikia Tundu Lissu akisema yale ambayo nimekuwa nikiyasema kwa miaka mingi!

Leo nimefurahi sana kumsikia Tundu Lissu akisema yale ambayo nimekuwa nikiyasema kwa miaka mingi!

Endeleeni kumpa moyo kwenye hizo harakati zake za kukimaliza chama chake. Wazee wenye umri kama wa Mbowe na Wasira anawataka wapumzike nyumbani kulea wajukuu. Lakini hapo hapo amemwomba Mzee Warioba agombee uraisi kupitia chama cha chadema 2025 ili yeye akagombee ubunge huko Singida aweze kuwa KUB
 
Hivi kuna nchi ambayo ilileta mabadiliko kwa kuzuia chaguzi kufanyika? Tatizo kubwa sio kuwa taratibu ni mbaya. Tatizo kubwa ni kuwa hata hizo taratibu mbaya zilizokuwepo hazifuatwi. Mfano hai ni wa wakina Halima. Pamoja na kuwa Katiba kusema kuwa mbunge ni lazima awe mwanachama wa chama cha siasa, wakina Halima wanamaliza miaka yao mitano pamojq na kuwa waliishafukuzwa kutoka kwenye Chama chao na chama hicho kusema hakiwatambui. Hii ni pamoja na precedent za Spika kuwanyang'anya ubunge wale waliotumuliwa na vyama vingine. Tamko la kuwafukuza lilipotoka, nafasi zao zikatangazwa kuwa wazi. Kwa mantik hii sitashangaa kuona wagombea wa Chadema wakipitishwa kugombea bila ridhaa ya Chama chao. Hapo bado vyama vingine ambavyo vitaona kuwa ni fursa ya kuchukua nafasi ya CDM.

Na kutegemea mataifa ya nje kuweka presha ni kujidanganya hasa katika enzi hizi za Trump na nchi za Ulaya kuongozwa na far right parties. Hawa watu hawana mpango na Tanzania na watakuwa comfortable kutambua utawala wowote utakaokuja.
Njia inayoweza kufanikiwa ni ya mass mobilization. Mimi ningewashauri wasahau uchaguzi wa 2025 walenge zile za 2029 na 2030. Hakuna Rais ambae atakubali kuwa wa kwanza wa mukula mmoja. Hakuna.

Kwa sasa waweke nguvu katika kuhamasisha watu na ku identify wagombea. wanaokubalika na wenye moyo wa kupambania haki zao. Watu kama Aisha wa Dodoma, yule dada wa Chato, mbunge wa Nkasi, yule dada wa Njombe, Susan Kiwanga, Catherine Ruge n.k.

Wa identify maeneo ambayo wana uhakika wa ushindi na wawekeze katika kuhakikisha kuwa hujuma hazifanyiki katika maeneo hayo. Hao wabunge wachache watakaopatikana watawapa nafasi ya kupiga kelele bungeni na kura watakazopata zitawapa ruzuku ambayo wataitumia kujitayarisha kwa ajili ya 2029 na 2030.

Amandla...
Mass mobilization halafu nini kinafuata baada ya hapo?

Kuwashawishi wananchi wengi kutokushiriki uchaguzi kwa sababu A, B, C, n.k, hiyo si sehemu ya mass mobilization?
 
Mkuu usimamizi wa dhati ndio upi labda?

Hivi kiuhalisia mpinzani akipata kura 50,000 na CCM akipata kura 10,000 halafu msimamizi akitangaza CCM imepata 50,000 na CDM 10,000 na mawakala wa CDM wakagoma kusaini fomu itabadilisha nini?

Masanduku ya kura wanatunza wao mahakama za kwao hata ukienda huko hamna kitu

Mkuu hizi suggestions zenu ni kwasababu hampo field kujionea umafya unaofanywa na ccm

Hapo sijazingumzia wagombea kenguliwa, kununuliwa, kutekwa, kuporwa fomu, fomu kuongezwa makosa na tume nk nk

Just imagine Mtu wa upinzani kakaa jela miezi 6 kafutiwa kesi na kuachiwa huru bila hakimu usiku wa saa 2 Singida na kesho yake Asubuhi yupo Bungeni anaapishwa ubunge wa Viti maalumu wa upinzani 😳
Yaani wapinzani wenyewe wanajishangaa😂
Umeongea ukweli mchungu sana
 
Endeleeni kumpa moyo kwenye hizo harakati zake za kukimaliza chama chake. Wazee wenye umri kama wa Mbowe na Wasira anawataka wapumzike nyumbani kulea wajukuu. Lakini hapo hapo amemwomba Mzee Warioba agombee uraisi kupitia chama cha chadema 2025 ili yeye akagombee ubunge huko Singida aweze kuwa KUB
Ungejiita tu Dr. Kilaza. Nani kakwambia Lissu alienda kumuomba Warioba agombee urais? Hivi huko CCM mnafuga funza vichwani mwenu?
 
Mass mobilization halafu nini kinafuata baada ya hapo?

Kuwashawishi wananchi wengi kutokushiriki uchaguzi kwa sababu A, B, C, n.k, hiyo si sehemu ya mass mobilization?
Sawa. Lakini hivi kuna quorum ya uchaguzi? Kuwa wakipiga kura watu pungufu ya hapa uchaguzi utakuwa batili? Ma utawashawishi vipi wanachama, mashabiki, watumishi wa umma kutoshiriki uchaguzi?
Mimi nadhani ni kuwashawishi wananchi kupigania uamuzi wao uheshimiwe. Nchi zote za jirani mabadiliko yalitokea baada ya wananchi kuchoka kudhulumiwa. Kama hawajachoka itakuwa kama kumpigia gigaa mbuzi. Hali haitabadilika.

Amandla...
 
hawezi kuhadaa watu kwama ana mkutano nao, kumbe anataka kuomba kuchangiwa pesa tu,

afanye kazi, ataomba kuchangiwa mpaka lini kibaraka asie na aibu huyo? :BASED:
Kuna sheria iliyotungwa kama mtu asichangiwe ewe mtafiti???
 
Ungejiita tu Dr. Kilaza. Nani kakwambia Lissu alienda kumuomba Warioba agombee urais? Hivi huko CCM mnafuga funza vichwani mwenu?
Wewe usiye na funza kichwani mwako, unadhani alienda kumuona Mzee Warioba kwa jambo gani? Warioba ni mzee kuliko Wasira na Tundu Lissu alishasema hadharani kuwa wazee wa aina hii hawana cho chote kipya cha maana hapa duniani cha kujifunza toka kwao. Kwamba wanapaswa kutulia tu nyumbani kulea vijukuu na vitukuu wakisubiri kifo chao ambacho kimeshafika mlangoni.

Alishasema hata wazee wa umri kama wa Mbowe (63 years sawa na wa Samia) nao wameshapitwa na wakati, wanapaswa kutulia nyumbani kulea vijukuu. Yaani kwake (Tundu Lissu) jukumu la kulea watoto siyo la baba wala mama bali ni jukumu la babu na bibi. Bila shaka yeye alilelewa na babu na bibi, ndiyo maana akili yake iko hivyo ya kifyatufyatu. Baadhi ya wafuasi wake wenye funza vichwani mwao wanamwamini anachokisema na hivyo wakampumzisha Mbowe kwa sababu ya uzee. Akili zao haziwezi kuona kwamba, 'There will be no reform but election is a must. Hence after the election there will be no chadema and peace shall prevail'.

Akili zao haziwaelekezi kuwa reform zinafanywa bungeni na wabunge wetu ambao ndiyo wawakilishi wetu tuliowachagua kupitia uchaguzi mkuu. Hakuna mtu mwingine yo yote wa kufanya reforms hizo za sheria, ni wabunge wetu pekee. Hata rais wetu au spika wa bunge letu hana mamlaka hayo.

Akili zao zenye funza hazioni kuwa ili hzo reforms wanazozitaka ziweze kufanyika, hatua ya kwanza ni chama chao kipate wabunge wengi zaidi ya wale wa ccm ili hoja yao iweze kufanikiwa huko bungeni. Kwani huko bungeni maamuzi hufanyika kura. Ni maamuzi ya wengi wape. The winner takes it all. Hakuna cha nusu mkate. This is what is meant by the word democracy. It is the rule of the majority through their representatives in the Parliament.

Akili zao zenye funza zinaamini kuwa democracy is the rule of the minority through maandamano, matusi, harakati na sarakati mitaani. After the 2025 general elections, hakitakuwa na muwakilishi hata mmoja bungeni huku wakitegemea wabunge wa ccm wawafanyie hayo mabadiliko ya sheria wanayotaka. Eti watatumia nguvu kama zile za M23 wakisaidiwa na hivyo vikundi wanavyovitumikia kutoka baadhi ya nchi za ulaya magharbi hususani Ubelgiji na Ujerumani kwa akina Robertson.
 
Back
Top Bottom