Leo nimefurahi sana kumsikia Tundu Lissu akisema yale ambayo nimekuwa nikiyasema kwa miaka mingi!

Leo nimefurahi sana kumsikia Tundu Lissu akisema yale ambayo nimekuwa nikiyasema kwa miaka mingi!

Utafika wakati Chadema itasimama kama chama imara na hapo ni pale chama hichi kitapoweza kusimama imara kwa uwezo kifedha.

Licha ya ruzuku chama pia hupaswa kuwa na uwezo wa kuwa na vyanzo vyake imara vya mapato ikiwemo michango wa wahisani na ada ya uanachama.

Hili la vyanzo vya mapato ni eneo jingine ambalo chama tawala lalitumia kujichotea fedha za umma ili zitumike kufanya mambo mengi kama takrima kununua mapikipiki na madubwasha mengine.

Mambo ni mengi ya kuishughulikia nchi hii ikiwemo Katiba mpya, mfumo wa Kleptokrasia , ruzuku kwa vyama vya siasa, matumizi mabaya ya kodi za wananchi na kila ina ya michezo ya ajabu.

Jambo la msingi kwa sasa ni kwa Chadema kuendelea kuwaelimisa wapiga kura namna ya kufikiri kwa umakini pale wanapokwenda kupiga kura kutoka kwenye kupiga kura kwa mazoea kuwa kupiga kura kwa umakini na malengo maalum huku wakiwa na ulinzi wa kutosha wa tume huru ya uchaguzi.
 
Umeishiwa kabisa hoja umebaki kutoa viroja tu!
sasa kibaraka anatumia masaa ma3 kupotosha wadau halafu kumbe agenda ilikua kuomba kuchangiwa pesa za kujikimu na kuongoza chama?

that's useless and completely nonsense, au nasema uongo ndrugu zango? 🐒
 
May be a passive strategy but it wont work at least significantly.

CCM ina vyama vingi sana vya kuiunga mkono and they can do anything to remain in power.

CDM wakisusa anapewa ACT, na wote wawili wakisusa CUF will be back on it gain...

then CUF kinaitwa chama kikuu cha upinzani.

Tusubir mapambano.

..hila zote hizo za nini?

..kwanini wasiunde Tume Huru na kila chama kifurahie ushindani wa kisiasa?
 
..hila zote hizo za nini?

..kwanini wasiunde Tume Huru na kila chama kifurahie ushindani wa kisiasa?
Haitakaa itoke, angalao sio kwa kizazi chetu...

Wengi washakubali matokeo haya, na wapambanaji wengi waliliona hilo wakaamua kujiunga nayo..

Katika historia ya nchi hii hakuna mpambanaji wa kweli wa opposition anaileishi au aileishi vizur ..

Anzia kina Kambona mpaka kina James Mbatia...

Mabere marando ni mfano mzur pia.

Madaraka yanapatikana kwa hila, ghilibu na wizi nchi karibu zote za Africa...
 
..sisi tunaweza kujitofautisha na nchi nyingine za Kiafrika.

..Tume Huru na uchaguzi wa HAKI una faida kubwa kwa nchi yetu.

..Watawala wanapaswa kuliona hilo.
 
Uchaguzi Mkuu wa 2025 uko palepale bila kujali chama gani kinashiriki ama la. Chadema kususa ni jadi yao. Wakitaka kujifanya M23 waambieni hii ni Tanzania. They'll perish!!!!
Huo ubabe wa kishamba chawa acheni kuwavimbisha kichwa ccm ili mnufaike, Dunia imebadilika mkileta ubabe misaada yote toka nje itafutwa na pia vikwazo vya uchumi vitakuja
 
sasa kibaraka anatumia masaa ma3 kupotosha wadau halafu kumbe agenda ilikua kuomba kuchangiwa pesa za kujikimu na kuongoza chama?

that's useless and completely nonsense, au nasema uongo ndrugu zango? 🐒
Wewe ndiyo kibaraka wa uovu kuiba kura kubaka demokrasia mpaka vyama kukosa wabunge na pesa, wewe ndiyo mchawi ndiyo ulimpiga risasi bila wewe mda huu asingekuwa akiomba msaada
 
Kasema " kama CCM haitakubali kufanya marekebisho MUHIMU ya matakwa ya uchaguzi, basi hakutakuwa na uchaguzi" Lakini pia akasema " hatutasusia uchaguzi, bali tutakwenda kwa wananchi na tutawaambia, pia jumuiya za kimataifa kuwaambia ccm na serikali yake inafanya nini hivyo tutataka uchaguzi usifanyike".

Kaomba nguvu ya makundi yote.
 
Wenye mamlaka ya kumiliki na kutoa taarifa kutoka kwenye BVR za kupigia kura ni CCM pekee, Wao ndio wenye idadi na umiliki wa daftari la kupigia kura, wao ndio hutoa vitambulisho vya kupigia kura.

Hivyo vitu vikimilikiwa na ujumuishi wa vyama vyote vya kisiasa tunaweza kupata kiongozi halali hata kwa katiba iliyopo, vinginevyo kushiriki uchaguzi wa aina tunayoshiriki siku zote ni kujidanganya.
 
Ambacho CCM hawana ni udhibiti wa fikra, nia, ari, na nguvu za wananchi.

Tukiamua kwa umoja, ndani ya siku chache tu CCM inasalimu amri.
Mimi tatizo langu kwa miaka mingi hili la CDM kila siku kuomba CCM ijikaange yenyewe. Tatizo ni kuwa CCM isipofanya hayo mabadiliko ni kweli CHADEMA wana nguvu ya kufanya lolote? Yaani, watafanya nini?
 
Bila kuwa na kitu kama M23 unakosa turufu ya kuitwa kwenye vikao vya maamuzi. Wanapaswa watafute turufu ya kuitwa kushiriki kufanya maamuzi.
 
Mimi tatizo langu kwa miaka mingi hili la CDM kila siku kuomba CCM ijikaange yenyewe. Tatizo ni kuwa CCM isipofanya hayo mabadiliko ni kweli CHADEMA wana nguvu ya kufanya lolote? Yaani, watafanya nini?
Yaweza pia kutokea yalotokea Zambia, Malawi na Botswana ambayo yalitikisa.

Lakini kama Chadema hawatajiandaa vilivyo basi yatatokea tena yale yalotokea Namibia ambako Swapo ilifanya maarifa na kupata asilimia 57 ya kura za ushindi dhidi ya asilimia 26 za upinzani.

Tume ya uchaguzi ya Namibia ECN yajisifu kuwa yazingatia mambo matatu makubwa Uwajibikaji (Accountability), Ushirikishwaji (Inclusiveness) Utaalam (Professionalism).

Lakini hapohapo:

1. Ni wananchi wenye haki ya kupiga kura walikosa nafasi ya kufanya hivyo,

2. Matangazo ya matokeo ya kura kufanyiwa kwenye makao makuu ya polisi.

3. Kutokuwepo kwa masanduku ya kutosha kwa ajili ya kukusanya kura.

4. Mashine za kuhesabia kura (scanners kuharibika kwenye vituo vingi vya kupigia kura.

Haya masuala yasemwa ni "typical" kwa mfumo wa demokrasia za Afrika kwasaabu zadidimiza harakati na michakato yote ya kuhakikisha chaguzi zawa huru na zenye kutoa haki kwa pande zote.
 
Mimi tatizo langu kwa miaka mingi hili la CDM kila siku kuomba CCM ijikaange yenyewe. Tatizo ni kuwa CCM isipofanya hayo mabadiliko ni kweli CHADEMA wana nguvu ya kufanya lolote? Yaani, watafanya nini?
Very good question.

Tusubiri tuone mwenyekiti mpya atakuja na mbinu/ mikakati gani.

Leo/ jana alipokuwa anazungumza, alinipa matumaini kiasi.
 
Kumbe yule aliyelamba asali na ambaye alikuwa kibaraka wa CCM ndie alianzisha mpango mzima wa " No Reform No Elections"? Au ndio namna ya kumbebesha lawama kama mkakati mzima ukisuasua?

Amandla...
 
CDM imekuja na mkakati mzuri nadhani kilichobaki ni kuzidi kuwaelimisha wananchi wafunguke watoe support ya kutosha!
 
Kumbe yule aliyelamba asali na ambaye alikuwa kibaraka wa CCM ndie alianzisha mpango mzima wa " No Reform No Elections"? Au ndio namna ya kumbebesha lawama kama mkakati mzima ukisuasua?

Amandla...
Kwa mtazamo wangu, Mbowe hakuwa consistent.

Kuna nyakati alikuwa anayumba. Leo anasema hakuna uchaguzi bila mabadiliko, baadaye anasikika akisema CHADEMA ijiandae na uchaguzi mkuu.
 
Back
Top Bottom