Ndiyo maana kuna mdau nilimjibu kuwa kuacha mwanamke siyo sawa na kuacha takamwili chooni, kwa mujibu wa hoja yako ni kweli kuwa kuna wanaosamehewa na kuacha pamoja na kujutia lakini kuna wengine ukimsamehe yeye anahisi dawa zake (ushirikina) ndio zimefanya kazi, hivyo atakudharau na kuendelea, pia kuna mwingine atakwambia ameacha kumbe wamebadilisha mbinu na mazingira ya kukusaliti.
Kuhusu kuwekeza kwenye "K" au watoto ni jambo zuri lakini una uhakika gani kama hao watoto waliokuja kupitia hiyo "K" ni damu yako (wanaume inatudhuru sana) Unaweza kuhangaika na watoto wakishafika ngazi ya chuo Baba yao mzazi anajitokeza halafu hana mbele wala nyuma na mke anakuambia ukweli kuwa huyo ndiyo Baba yao mzazi (maana wakati huo hana cha kupoteza) na hatimaye unagundua kuwa ulifanywa mjinga kipindi kirefu cha maisha yako.
Kuhusu kusamehe ni jambo zuri lakini unaposema "umesamehe ila kidonda hakiponi" jua wazi kuwa hujasamehe na hivyo unajidanganya na kujiumiza mwenyewe maana Msamaha wa kweli unaambatana na kuachilia pia. Unaposamehe halafu ukashindwa kuachilia matokeo yake ni kufa kwa sonona (hivyo ndiyo mke mzinzi anapenda ili apate mali kiurahisi)
Sasa naomba unijibu. Kwa usumbufu na madhila yanayopatikana katika sakata la fumanizi je, adhabu ya faini inatosha?