Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kuna ukweli kiasi kikubwa katika hili.
Ndio maana kuna mdau juu kasema watu wanaohangaika na mapenzi ni wale masikini. Kiuhalisia anachokiongea huyu jamaa ni kwamba yeye maisha yake yapo mikononi kwa mke wake. Kwamba akimfumania tu, huo ndio unakua mwisho wa maisha ya wote watatu (anaua mke na mgoni na yeye anaenda kufia/kuozea jela!)
Kwa mtu ambae una mipango ya maana,una watu wanaokutegemea, unaheshimika, una miradi ya kusimamia, una hela za kula maisha mjini hapa, unajua unaweza kupata mwanamke yoyote unaemtaka, huwezi kuwa na akili ya kipumbavu kama hiyo kamwe.