Leo nimejisikia vibaya sana wakuu!

Leo nimejisikia vibaya sana wakuu!

Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!

Siku ya leo kwangu imekuwa siku mbaya sana kwasababu mimi huwa nina huruma sana na huwa naguswa na matatizo ya watu wengine wanayopitia!.

Leo nilikuwa nimeenda Hospitali moja pale Sinza,nilimpelekea Dada mmoja hivyo ikabidi nipaki nje kumsubiri!,Sasa wakati nikiwa pale nje kuna dada mmoja alitoka ndani ya hospitali mwanaye akiwa analia kweli!

Alipofika kwangu akawa ameniomba nimsaidie nauli ya kumfikisha kwake,ikabidi nimuulize maswali kadhaa,baada ya kujiridhisha kutokana na majibu yake kiukweli niliumia sana!.

Yeye " Kaka mambo"

Mimi " Poa,Kwema"

Yeye "Samahani kaka,naomba unisaidie!"

Mimi " Nikusaidie nini Sister?"

Yeye " Kaka pesa yote niliyokuwa nayo nimefanya vipimo vya mwanangu na nyingine nimechukulia dawa!"

Aliendelea " Naomba tu unisaidie nauli ya kunifikisha nyumbani kaka"

Mimi "Pole sana,Unaishi wapi?"

Yeye " Nakaa Banana"

Mimi "Umemtaarifu Mumeo kwamba umeishiwa nauli?"

Yeye "Wee acha tu kaka,ni kama huyu mtoto hana Baba"

Mimi "Kwanini?,Baba yake yuko wapi?:

Yeye " Baba yake alimkataa mwanaye!"

Mimi "Usione kama nakuuliza maswali dada,nisamehe kama nitakuudhi lakini nataka kujiridhisha maana matapeli huu mji ni wengi mno!"

Yeye "Mimi si tapeli kaka naomba unisaidie tu nauli"

Mimi "Hapana sister,sijasema wewe ni tapeli,nilikuwa nakuelewesha tu!:

Yeye "Basi ngoja nkutolee kadi la kriniki uone"

Kweli,alinitolea kadi la kriniki pamoja na dawa ambazo aliandikiwa akanunue kwa ajili ya mwanaye!

Sikutaka kumchimba sana maana pengine niliona isingekuwa vema kumpeleleza,mimi niliamua tu kujiongeza!

Sasa ni kwamba,kwa maelezo yake ni kuwa jamaa aliyempa mimba alimkimbia akiwa mjamzito na jamaa anafanya kazi Tanesco Mkoa wa Kitanseco wa Ilala!.

Kiukweli mwanamke ni mzuri na amezaa mtoto wa kike mzuri sana kama mama yake!.Nilijaribu kumuuliza sababu za yeye kuachana na huyo mshikaji akadai ni wivu wa kimapenzi!.

Leo nimenikuta natoa Tsh 50,000/= namsaidia yule dada,Kiukweli sijawahi kutoa kiasi hicho cha pesa kusaidia kutokana na nature ya kazi yangu (Hayo mambo niliyafanya zamani nilipokuwa Don kabla sijarudi kuanza moja).

Kiukweli baada ya kumpa hiyo hela huyo Dada nimejihisi amani sana na nimekuwa na furaha ya moyo ingawa nimehuzunika sana!

USHAURI:

Wanaume wenzangu,hata kama utakuwa umekosana na mwanamke ambaye amekubebea mimba yako kiasi gani, tafadhali usimtelekeze,kiukweli huwa wanapitia mateso makubwa mnooo!,nawaomba sana msije mkafanya hivyo!.

Hata kama huyo mwanamke awe ameekuudhi kiasi gani,tafadhali jifanye mjinga tu ili umnusuru mtoto kwasababu dogo anakuwa hana tatizo,tatizo linakuwa kwenu,hivyo mtoto mpeni haki yake ya matunzo na malezi!.

Mwanamke hata akiwa amekosea kiasi gani lakini machozi na maumivu yake ni laaana tosha!,huwezi kutoboa kamwe kama akiwa anamuangalia mwanaye anateseka na wakati Baba yake yupo kazi kulewa tu na kubadili wanawake,hakika huto toboa!.

Hebu wanaume wenzangu tubadilike ndugu zangu,kiukweli inaumiza sana kukutana na mwanamke anaomba nauli wakati Baba yake yupo!

Chanzo cha watoto wetu kuaribika tatizo huanzia pia kwa Wanaume wanaowatelekeza wanawake wao!,Tusiishie kuwalaumu Marekani na Nchi zilizoendelea kwa kutuleta Ushoga bila kubadilika sisi wenyewe na kutatua matatizo yetu!.

Wewe unamuacha mwanao wa kiume analelewa na mama yake,unategemea nini?!.

Hebu naomba tubadilike!,Tuache Upuuzi!
CHAI
 
Sisemi vibaya ila Wanawake sio watu wa kawaida kbs, umesikia upande mmoja ila ungesikia upande wa pili huenda ungetoa laki umpe huyo mwanaume. Hawa viumbe Mungu ndio anajua alipowakosea ktk uumbaji wake ndio maana alisema tuishi nao kwa akili Mungu sio fara.
 
UMUGHAKA umepigwa. MTU atoke banana aje Sinza Palestina wakati Buguruni Kuna kituo Cha afya na Amana Ni gari moja toka Banana, hata angekwenda Temeke bado Ni gari moja na hakuna foleni.
Unakumbuka ule usemi kwamba MTU akizaliwa Dar tayari Ni fomfoo?
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣bwege mtozeni.
 
[/QUOTE]
Sisemi vibaya ila Wanawake sio watu wa kawaida kbs, umesikia upande mmoja ila ungesikia upande wa pili huenda ungetoa laki umpe huyo mwanaume. Hawa viumbe Mungu ndio anajua alipowakosea ktk uumbaji wake ndio maana alisema tuishi nao kwa akili Mungu sio fara.

Mkuu timiza wajibu wako achana na mambo ya kusikiliza upande wa pili!
 
UMUGHAKA umepigwa. MTU atoke banana aje Sinza Palestina wakati Buguruni Kuna kituo Cha afya na Amana Ni gari moja toka Banana, hata angekwenda Temeke bado Ni gari moja na hakuna foleni.
Unakumbuka ule usemi kwamba MTU akizaliwa Dar tayari Ni fomfoo?

Mkuu umeandika ili kumckesha na kumfurahisha Shoga Hance Mtanashati au umeandika ukiwa na akili zako timamu?
 
Hapo umesikiliza ya upande mmoja ukatoa 50k, je unayafahamu ya upande wa pili wa mwanaume...jitahidi ujue kabla ya kutoa hukumu!
Yeye amesikiliza upande mmoja na ndio upande aliokutana nao,ulitaka aanze kuutafuta na upande wa pili? Kwani yeye ni Mahakama na anataka kutoa hukumu?

Huo upande wa pili kausikilize wewe,yeye ametoa msaada na Mungu ameona that's more tha enough.
 
Vizuri kama umejiridhisha ..tatizo MATAPELI wengi sana hilo eneo ambao wanaharibu sifa ya watu wenye uhitaji kweli...miaka ya nyuma kama 10 imepita nilikuwa hilo eneo la Palestina lilijaa matapeli sana...yaani mama anakuja na vyeti kabisa na analia anahitaji msaada...ukisema twende nkakunulie dawa etc wanakimbia hawataki...
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!

Siku ya leo kwangu imekuwa siku mbaya sana kwasababu mimi huwa nina huruma sana na huwa naguswa na matatizo ya watu wengine wanayopitia!.

Leo nilikuwa nimeenda Hospitali moja pale Sinza,nilimpelekea Dada mmoja hivyo ikabidi nipaki nje kumsubiri!,Sasa wakati nikiwa pale nje kuna dada mmoja alitoka ndani ya hospitali mwanaye akiwa analia kweli!

Alipofika kwangu akawa ameniomba nimsaidie nauli ya kumfikisha kwake,ikabidi nimuulize maswali kadhaa,baada ya kujiridhisha kutokana na majibu yake kiukweli niliumia sana!.

Yeye " Kaka mambo"

Mimi " Poa,Kwema"

Yeye "Samahani kaka,naomba unisaidie!"

Mimi " Nikusaidie nini Sister?"

Yeye " Kaka pesa yote niliyokuwa nayo nimefanya vipimo vya mwanangu na nyingine nimechukulia dawa!"

Aliendelea " Naomba tu unisaidie nauli ya kunifikisha nyumbani kaka"

Mimi "Pole sana,Unaishi wapi?"

Yeye " Nakaa Banana"

Mimi "Umemtaarifu Mumeo kwamba umeishiwa nauli?"

Yeye "Wee acha tu kaka,ni kama huyu mtoto hana Baba"

Mimi "Kwanini?,Baba yake yuko wapi?:

Yeye " Baba yake alimkataa mwanaye!"

Mimi "Usione kama nakuuliza maswali dada,nisamehe kama nitakuudhi lakini nataka kujiridhisha maana matapeli huu mji ni wengi mno!"

Yeye "Mimi si tapeli kaka naomba unisaidie tu nauli"

Mimi "Hapana sister,sijasema wewe ni tapeli,nilikuwa nakuelewesha tu!:

Yeye "Basi ngoja nkutolee kadi la kriniki uone"

Kweli,alinitolea kadi la kriniki pamoja na dawa ambazo aliandikiwa akanunue kwa ajili ya mwanaye!

Sikutaka kumchimba sana maana pengine niliona isingekuwa vema kumpeleleza,mimi niliamua tu kujiongeza!

Sasa ni kwamba,kwa maelezo yake ni kuwa jamaa aliyempa mimba alimkimbia akiwa mjamzito na jamaa anafanya kazi Tanesco Mkoa wa Kitanseco wa Ilala!.

Kiukweli mwanamke ni mzuri na amezaa mtoto wa kike mzuri sana kama mama yake!.Nilijaribu kumuuliza sababu za yeye kuachana na huyo mshikaji akadai ni wivu wa kimapenzi!.

Leo nimenikuta natoa Tsh 50,000/= namsaidia yule dada,Kiukweli sijawahi kutoa kiasi hicho cha pesa kusaidia kutokana na nature ya kazi yangu (Hayo mambo niliyafanya zamani nilipokuwa Don kabla sijarudi kuanza moja).

Kiukweli baada ya kumpa hiyo hela huyo Dada nimejihisi amani sana na nimekuwa na furaha ya moyo ingawa nimehuzunika sana!

USHAURI:

Wanaume wenzangu,hata kama utakuwa umekosana na mwanamke ambaye amekubebea mimba yako kiasi gani, tafadhali usimtelekeze,kiukweli huwa wanapitia mateso makubwa mnooo!,nawaomba sana msije mkafanya hivyo!.

Hata kama huyo mwanamke awe ameekuudhi kiasi gani,tafadhali jifanye mjinga tu ili umnusuru mtoto kwasababu dogo anakuwa hana tatizo,tatizo linakuwa kwenu,hivyo mtoto mpeni haki yake ya matunzo na malezi!.

Mwanamke hata akiwa amekosea kiasi gani lakini machozi na maumivu yake ni laaana tosha!,huwezi kutoboa kamwe kama akiwa anamuangalia mwanaye anateseka na wakati Baba yake yupo kazi kulewa tu na kubadili wanawake,hakika huto toboa!.

Hebu wanaume wenzangu tubadilike ndugu zangu,kiukweli inaumiza sana kukutana na mwanamke anaomba nauli wakati Baba yake yupo!

Chanzo cha watoto wetu kuaribika tatizo huanzia pia kwa Wanaume wanaowatelekeza wanawake wao!,Tusiishie kuwalaumu Marekani na Nchi zilizoendelea kwa kutuleta Ushoga bila kubadilika sisi wenyewe na kutatua matatizo yetu!.

Wewe unamuacha mwanao wa kiume analelewa na mama yake,unategemea nini?!.

Hebu naomba tubadilike!,Tuache Upuuzi!
Kumbe kupigana ni kapepo tu kanakupitiaga ila una moyo mzuri sana hongera mkuu
 
Yeye amesikiliza upande mmoja na ndio upande aliokutana nao,ulitaka aanze kuutafuta na upande wa pili? Kwani yeye ni Mahakama na anataka kutoa hukumu?

Huo upande wa pili kausikilize wewe,yeye ametoa msaada na Mungu ameona that's more tha enough.

Safi sana,

Mkuu wewe una akili kubwa sana,Hongera sana mkuu!
 
Japo we jamaa me siku kubari wala nini...

Ila kumekuwa na tabia hawa wadada ikifika jioni wana tembea na watoto kuomba nauli hii nme iona pale mawasiliano stand.

ile njia jion wadada wana pishana na watoto wana omba nauli uki pita tu ana jifanya ana enda stand ,afu ana rudi kutafuta mwingine ni upumbavu wa hali ya juu
 
Vizuri kama umejiridhisha ..tatizo MATAPELI wengi sana hilo eneo ambao wanaharibu sifa ya watu wenye uhitaji kweli...miaka ya nyuma kama 10 imepita nilikuwa hilo eneo la Palestina lilijaa matapeli sana...yaani mama anakuja na vyeti kabisa na analia anahitaji msaada...ukisema twende nkakunulie dawa etc wanakimbia hawataki...

Huyu nimejiridhisha mkuu na dawa amendikiwa ila hakuwa na hela,mimi nimewahi kuwa tapeli na Jambazi,hivyo naelewa mtu akiwa tapeli,huyu mama alikuwa na uhitaji maana karibia pesa yote aliyokuwa nayo imeishia kwenye matibabu ya mwanaye!,Halafu mwanaye ni alichubuka usawa wa jicho hivyo alikuwa na Jeraha!

Kuna muda alitaka nisipompa hela nimsaidie kumnunulia mwanaye dawa alizoandikiwa,Aiseee kuna matapeli lakini yule Sister anapitia magumu mno!.

Yaani sielewi hata kesho na kuendelea atakula nini,kibaya zaidi sikuchukua namba yake!

Pesa niliyokuwa nimepanga nifanyie mambo yangu nimeona nimpatie yeye,kwani hata hivyo mkuu huwa tunapoteza kiasi gani kwenye mambo ya ajabu?,Huwezi amini baada ya kumsaidia nina amani kuliko kawaida!
 
Kwani mwanaume kosa lake nini unajua ugomvi wao mpk uje kutuchanganya na wao elimu kubwa kufikiri kidogo duh!
 
Kumbe kupigana ni kapepo tu kanakupitiaga ila una moyo mzuri sana hongera mkuu

Mkuu kupigana huwa ni kwasababu nachokozwa na malaya hawa wa mjini wasio kuwa na kazi ya kufanya,but kiuhalisia mimi ni mtu poa sana !
 
Kwani mwanaume kosa lake nini unajua ugomvi wao mpk uje kutuchanganya na wao elimu kubwa kufikiri kidogo duh!

Elimu kubwa vipi mkuu,timiza wajibu wako achana na mambo ya ugomvi,ina maana ukigombana na Kiswanswadu wako mwanao apate shida kwasababu ya ujinga wenu?
 
Back
Top Bottom