Leo nimemfukuza mpangaji wangu kwa tatizo lake la kuleta wanawake tofauti nyumbani kwangu na kusababisha usumbufu kwa wapangaji wengine

Leo nimemfukuza mpangaji wangu kwa tatizo lake la kuleta wanawake tofauti nyumbani kwangu na kusababisha usumbufu kwa wapangaji wengine

Tatizo hili utakutana nalo zaidi kwa wamiliki wa nyumba za kurithi haswa mikoa ya pwani na wengi wao ni wenyeji wa mikoa ya kusini Mtwara na LIndi. Unakuta anaishi around kwenye hio nyumba ya wapangaji na kula yake inategemea hizo kodi.

Mtu mwenye uwezo wa kumiliki kijiji cha apartments huwezi kukuta ana michongo ya kufuatilia wapangaji.
MKuu sina shida kabisa na wapangaji hawa maana siishi nao sehemu moja, nyumba nimejenga mwenyewe sio za kurithi jambo jambo lililonifanya kufikia uamuzi huu ni mpangaji huyu kuwa kero kwa wenzake licha ya wenzake kuzungumza naye mara kwa mara na yeye kukataa kuenenda kwa ustaraabu wa mahali hapo sijawahi fika kwenye hizo toka mwaka huu unaanza tunawasiliana tu kwa simu na kusoma miamala ya benki.
 
Mada ni ni kwamba anamiliki Uniti saba sehemu moja! Hayo mengine ni blah blah tuu,, ukichukulia huyo mtu ndio kwanza umepewa kesi moja, hujawah kumuita na kuongea nae kuhusu mazuri na mabaya yake, huyo aliyeleta ushahidi unauhakika Hawana ugomvi wowote? Uliruhusu vipi kumpangisha mtu nyumba yako na ukijua fika ni single na maisha ya mtu single unayajua? Hukutakiwa kukurupuka kwakuwa hujatoa historia ya huyo mtu kwamba umelalamikiwa anatembea na wake za watu, hrf umesha Sema saa nane za usiku? Are you serious Mr faza house? Punguzeni uswahili mliofanikiwa kujenga nyumba za biashara huyo mtu ulipaswa kumuita na kuongeanao ili kumpatia nafasi ya kuangalia mabadiriko yake! Anyway faza house go a heads ni haki yako!
 
Mpangaji mstaarabu sana huyo analeta wanawake usiku wa manane kulinda faragha yake na asipoonyeshe picha mbaya kwa wapangaji wenzake.

Huyo mpangaji mwenye audio ni mbeya na alijuaje kama analeta wanawake tofauti wakati ni usiku wa manane, alafu issue ya kelele hata akiwa na demu mmoja kelele zipo pale pale kila akigegeda. Btw wewe mwenye nyumba ndio tatizo na huo mradi wako wa hizo unit zako kwa kujenga bila kufanya Environmental Impact Assessment (EAA) ambapo wataalam wangekuambia nini cha kufanya kuzuia madhara ya kelele kwa wengine.

Namshawishi mpangaji wako mmoja na huyo uliemfukuza akushitaki kwa kutozingatia kanuni za ujenzi na kusababisha madhara ya kelele
 
Kodi haitoshi kukuachia uhuru ufanye Kila unaloona kwako linafaa, nyumba sijaijenga kwa ajili ya kufanyia uzinifu, maadili yazingatiwe
Ww inawezekana nyuma umepata hela kwenye zinaa acha mzunguko ukamilike
 
Wahuni siwataki nyumbani kwangu kama hutaki kuoa baki single au ishi na mwanamke mmoja kwa uadilifu. Wahuni
Acha ujinga We kenge ...Issue ni kuoa ama ishu ni audio wakati wa tendo?..What if kama kaoa ila wakati wa tendo wana vibe kali la kutoa sauti utasemaje tena..naomba nikushauri haya yafuatayo wewe na hao maboya wenzako(wapangaji)..

1)Acheni kufuatilia faragha za watu..Mnaingilia uhuru binafsi.
2)hayo magofu yako yaboreshe kaisi kwamba mtu akiwa chumbani hata kekele ziwe kali vipi mtu nje hasikii..So ikitokea hajafunga dirisha ama mlango hiyo ni kesi nyingine.
Over
 
Nina units saba kwenye eneo moja vijumba vimekaribiana kiasi sasa huyu mpangaji mmoja yeye ni kuleta wanawake usiku wa manane na kufanya mapenzi kwa fujo na makelele mengi.

Mpangaji wangu mmoja kati yao akanitumia malalamiko na ushahidi wa audio voice jinsi ndugu huyo anavyofanya na hao wanawake usiku wa manane mpaka imekuwa kero kwa wapangaji wengine sasa nimetafakari toka asubuhi nikaona nimuondoe.

Sasa leo nimempigia simu ndugu huyu na kumwambia ujinga wake na kwa msisitizo nimemrudishia kodi yake iliyobaki kesho nisimuone naona ametaka yaishe ila naona si busara kumwacha akae maana atawaharibu na hawa wengine nyumba zangu sijawajengea wahuni.

Somo langu kwa Vijana mnaojitafuta kwenye maisha acheni ujinga wa kuhangaika na wanawake wanaharibu nguvu zenu bure ndio maana wengi mpo Dar na hamna kiwanja wala nyumba kwasababu ya kuendekeza starehe ambazo zinakera hadi wengine yasiyowahusu.

Nazima simu.
Watu wa hivyo hata utunzaji wa nyumba ni matatizo sana.
Kero za mpangaji mmoja zinafukuza wapangaji wengine
 
Umekutana naa mpangaji zoba. Aisee mimi ningekaa bure 6 months.

Kwasababu najua kwenye mkataba ilo sharti halipo.
 
Sasa nani anamuona
Aende akapige kelele huko asisumbue watu Kuna watoto usiku hawalali utashangaa siku vitoto hapo mtaani vinaanza kulia liankimahaba[emoji3]

Mm naheshimu uhuru wangu na watu wengine shughuli zangu na baby wangu tunamalizia maeneo tnayoona nitajiachia sio kwenye nyumba za watu na km ikiwa but Kwa adabu na heshima
Ila shangazi umechangamka mnoo. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo hili utakutana nalo zaidi kwa wamiliki wa nyumba za kurithi haswa mikoa ya pwani na wengi wao ni wenyeji wa mikoa ya kusini Mtwara na LIndi. Unakuta anaishi around kwenye hio nyumba ya wapangaji na kula yake inategemea hizo kodi.

Mtu mwenye uwezo wa kumiliki kijiji cha apartments huwezi kukuta ana michongo ya kufuatilia wapangaji.
Naunga mkono hoja.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Nina units saba kwenye eneo moja vijumba vimekaribiana kiasi sasa huyu mpangaji mmoja yeye ni kuleta wanawake usiku wa manane na kufanya mapenzi kwa fujo na makelele mengi.

Mpangaji wangu mmoja kati yao akanitumia malalamiko na ushahidi wa audio voice jinsi ndugu huyo anavyofanya na hao wanawake usiku wa manane mpaka imekuwa kero kwa wapangaji wengine sasa nimetafakari toka asubuhi nikaona nimuondoe.

Sasa leo nimempigia simu ndugu huyu na kumwambia ujinga wake na kwa msisitizo nimemrudishia kodi yake iliyobaki kesho nisimuone naona ametaka yaishe ila naona si busara kumwacha akae maana atawaharibu na hawa wengine nyumba zangu sijawajengea wahuni.

Somo langu kwa Vijana mnaojitafuta kwenye maisha acheni ujinga wa kuhangaika na wanawake wanaharibu nguvu zenu bure ndio maana wengi mpo Dar na hamna kiwanja wala nyumba kwasababu ya kuendekeza starehe ambazo zinakera hadi wengine yasiyowahusu.

Nazima simu.
Kama wote mabachela hamna tatizo ila kama kuna watoto upo sahihi
 
Back
Top Bottom