Demi
JF-Expert Member
- Nov 22, 2016
- 40,466
- 88,695
Mwanangu unajua kupika? Basi mkwe wangu atafaidi sana...sio kwenye mapishi peke yake na kwenye mambo mengine pia. Hongera sana.naichukua hii
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwanangu unajua kupika? Basi mkwe wangu atafaidi sana...sio kwenye mapishi peke yake na kwenye mambo mengine pia. Hongera sana.naichukua hii
Baba pale kwenye nazi umeniacha Hoi, ulikalia kibao kabisaa ukaikuna kwaaa kwaaaaa kwaaaa.Mkuu soma vizuri hilo bandiko
Umejitahidi ila tuNilikua na hamu ya ndizi nyama hivyo kwa kua nalijua jiko nikapita zangu sokoni nikachukua mazaga kadhaa nikaingia jikoni😆 na nitawaelezea jinsi nilivyopika hatua kwa hatua
MAHITAJI;
Carry powder, paprika powder, black pepper, soya souce, tui la nazi (tui la 1 na tui la 2), ndizi mshale 8, nyama nusu, carrot na pilipili hoho (paprika)
View attachment 3193027
Nikachemsha nyama hadi zikaiva na kulainika kabisa mimi huwa sipendi nyama ngumu
View attachment 3193032
Baada nyama kuiva nikabadilisha sufuria maana ilikua ndogo nikaweka ndizi zilizokatwa vipande vidogo kisha nikachanganya paprika powder, black pepper, carry powder, soya souce na chunvi
View attachment 3193033View attachment 3193034
Baada ya kukoroga na kuhakikisha viungo vimekolea vizuri nikaweka nyama na tui la nazi la pili
View attachment 3193035
Kisha nikaweka mchuzi wa nyama
View attachment 3193037
Baada ya hapo nikafunika ili mchanganyiko wangu uive kwa muda fulani
View attachment 3193039
Baada ya mchanganyiko kuiva nikaongeza hoho, carrot na tui la kwanza (tui zito)
View attachment 3193040
View attachment 3193041
Kisha nikafunika tena kwa dakika kadhaa ili mchanganyiko uive vizuri baada ya dk kama nane chakula chetu kilikua tayari kwa kuliwa
View attachment 3193048
Chkula kilikua chamoto sana na kitamu chenye radha nzuri na kinanukia
View attachment 3193052
Natamani niwaonjeshe utamu wa hiki chakula ila ndo hivyo tena haiwezekani😜 na pia wengi watajiuliza ulikunaje nazi? Jibu nilitumia blender kisha nikaichuja
Wale tulio single bila wapenzi tuwe na mazoea ya kupika tukipata muda vyakula vya mama ntilie vipo kibiashara zaidi na pia vina kasoro nyingi mno
Mimi ni mtu wa pwani napenda sana chakula kilichopikwa kwa mchanganyiko wa nazi juzi nilitoka mafia nikambebea mama nazi za kutosha chache nikabaki nazo
View attachment 3193106
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣lolWanasema kupika ni Sanaa ila kwangu hii Sanaa imenikataa, labda wali wa kwenye rice cooker na wenyewe huwa hadi Leo nabahatisha kwenye swala la kukadiria maji.
Kuna siku yanakua mengi so nakunywa uji, kuna siku yanakua kidogo so natafuna mchele na kuna siku yanakua poa nakula zangu wali😂😂😂😂... Anyway, hongera sana mkuu.
Wanaume wanaojua kupika wapo so sexy yaani
Acha tu mdogo wangu.Mnoo 😭😭
Mbona ghafla Sana mmeamia lini huku kwenye mapishi kama kigezo😃😃Mnoo 😭😭
Mtumishi mbona hamjatoa tangazo twende short course😃😃Acha tu mdogo wangu.
najulia wapi mama?🤣Mwanangu unajua kupika? Basi mkwe wangu atafaidi sana...sio kwenye mapishi peke yake na kwenye mambo mengine pia. Hongera sana.
Ila Fresh mwanangu,imeisha hiyoooMkuu soma vizuri hilo bandiko
Umenichekesha wakati uzi umenipa majonziMbona ghafla Sana mmeamia lini huku kwenye mapishi kama kigezo😃😃
Najifunza madam🙏Umejitahidi ila tu
1. Ndizi nyama haziwekwi viungo zaidi ya karoti, kitunguu, pilipili (kwa wanaopendelea) hoho na nyanya kidogo sana (ni vyema zaidi kuacha kuweka nyanya)
2. Maji ya kwanza kupikia ndizi yanawekwa kidogo, hayatakiwi kuonekana juu ya ndizi.
Kuhusu nazi tayari umeshauriwa huko juu kwa usahihi, otherwise ulipata nyama nzuri sana ndio maana ndizi zimekuwa nzuri.
Ushauri huu wa mapishi ya ndizi ni kutokea kwa wenye ndizi nyama zetu, uchagani.
Kikao cha mwaka jana tulikubaliana mwanaume ukianza kuunga vitu kwa kutumia nazi sahau kuoa
Nadhan mwongozo bado hujabadilika
Ilikua GG hiyo (both Team to score) unakula kisha baadae unaliwaUmenichekesha wakati uzi umenipa majonzi
Mkuu,raha sana kuwa na mwanaume anayejua kupika sana....nakumbuka nilikuwa naenda kwake niko zangu naangalia movie yeye ananipikia chakula kitamuuu 😭😭
Au labda kwasababu mimi sijuagi kupika