Leo nimetongozwa na binti mdogo tu, imenikumbusha sana ujana wangu

Leo nimetongozwa na binti mdogo tu, imenikumbusha sana ujana wangu

Pole sana,tupe story ilikuwaje?[emoji3]
Nilitoka kzn nikasema leo ngoja nipite shivas, nikanywa alaf nikapitiliza jaman, siku hiyo nilitaka tu kufurahi, muda wa kuondoka kumbe kuna lifisi lilikuwa linanimendea lilijoin nilipokuwa nimekaa tukaanza kunywa nalo, nimefika muda wa kuondoka likaniambia nisiondoke nikasema nahitaji kupumzika likaniambia litanipeleka nikanwambia nina gari, basi akasema atanisindikiza nikatoka yaani wewe achaaa ... Story itaendelea wewe fisi
 
Wakuu mmebarikiwa,

Leo katika pitapita zangu mtaani, kuna mabinti walikiwa wamekaa kibarazani wanasukana, nilipita bila kuwasalimia maana walikuwa bize hivi.

Sasa wakati narudi njia ileile nikaona binti mmoja anasimama anakuja barabarani akanisimamisha akanipa hi, nikaitikia fresh tu.

Akaanza kujiumauma ooh kaka samahani unajua nakuonaga unapita nawaambiaga wenzangu yule kaka nampenda sasa leo umepita nimeoana nikusalimie, nikamjibu asante ondoa shaka kwa hiyo bado unanipenda au unawaambiaga tu rafiki zako?

Akajibu ndio hivyo sahamani lakini, wakuu hii haliya kutongozwa na binti huyu imenikumbusha miaka 15 nyuma wakati niko kijana barobaro mabinti walikuwa wananitongoza haipiti mwezi, hapa miaka ya katikati ubize wa maisha na nini nikawa sijijali sana ila sasa binti huyu amenikumbusha ujana wangu.

Kesho ntawapa mrejesho maana nimeshindwa kumkubalia kirahisi ataniona malaya, nimechukua namba zake tu nimemuahidi nitamtafuta.
Kama upo Dar, nakukumbusha biashara imekua ngumu kwaio mbinu zimebadilika za kibiashara.
 
Nashangaa wazee wa "Weka picha" wamezembea wapi leo? 🤣🤣🤣

Msisahau kesho siku ya UKIMWI.
 
Akajibu ndio hivyo sahamani lakini, wakuu hii haliya kutongozwa na binti huyu imenikumbusha miaka 15 nyuma wakati niko kijana barobaro mabinti walikuwa wananitongoza haipiti mwezi, hapa miaka ya katikati ubize wa maisha na nini nikawa sijijali sana ila sasa binti huyu amenikumbusha ujana wangu.
Nachukia sana hii hali angalia tu asije akakupiga madole 🖕🏽🖕🏽🖕🏽
 
Bora we bado unatongozwa na mabinti, wenzako uzee umepiga hodi uhandsam boi umepotea mabinti hatuwavutii tena kama zamani. Hata wakongwe wenzetu hatuwavutii, hatuna bara wa visiwa tupotupo tu ni kama tumestaafishwa mapenzini
 
Back
Top Bottom