Mahakamani leo tena kesi inaendelea kwa Upande wa Mawakili wa Serikali kumuuliza Mswali ya Dodoso Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika
Pia soma: Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kutoa Ushahidi kumtetea Tundu Lissu Mahakamani leo Agosti 31, 2026. Kesi imeahirishwa hadi Kesho
Leo September 1, 2026
Last time tuliishia Sehemu ya 317, leo tunaendelea na 318
Sehemu ya 318
Maombi yalishafanyika asubuhi hii na Majaji wameingia na Mheshimiwa Lissu akiwa na Kombati nyeusi pia ameingia tayari Mahakamani.
Anasimama Ajuaje niko na Katuga, Mrema, Ignas Mwinuka, Thawabu Issa, Cathbert Mbiringe na Winiwa Kasawa. Wote tunaiwakilisha Jamhuri na tuko tayari.
Mhe. Lissu nae anasema yuko tayari na Shahidi anapanda kizimbani.
Jaji Ndunguru: Shahidi nakukumbusha bado uko chini ya kiapo.
Katuga: Habari ya asubuhi Shahidi?
Mnyika: Salama.
Katuga: Wewe ulikiwakilisha Chama kwenye Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria?
Mnyika: Ndio
Katuga: Wakurugenzi ulipendekeza wasishiriki zoezi la uchaguzi?
Mnyika: Wakurugenzi na watumishi wa Serikali wengine?
Katuga: Ulipelekea sheria ya uchaguzi kubadilika na wakurugenzi waliondolewa kwa mujibu wa kifungu cha 6?
Mnyika: Uliondoa Wakurugenzi na kuweka utaratibu mbovu zaidi wa maafisa waliopo chini ya Mkurugenzi.
Katuga: Mlipata nafasi kutoa maoni au hamkupata?
Mnyika: Nilizimiwa kipaza sauti
Katuga: Mabadiliko ya Kikatiba ulitoa maoni yake au hukutoa?
Mnyika: Nilizuiliwa sikutoa.
Katuga: Ni maoni gani ulitoa maoni gani hukutoa?
Mnyika: Nilisema maoni yote ya kuhusu Katiba yalikataliwa.
Katuga: Baada ya kusema Kamati ya Bunge kukataa maoni yenu ulirudisha mpango mkakati kuwa tukazuie uchaguzi?
Mnyika: Hauko sahihi
Katuga: Mkakati wa kuzuia uchaguzi haukuwa mpango wa Chama?
Mnyika: Ulishapitishwa Tar. 02/12/2024 na Kamati Kuu katika azimio la No Reforms: No Election. Hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi.
Katuga: Mtandao wa Jambo TV ni nini?
Mnyika: Nilisema niliambiwa mtandao wa Jambo TV ndio ulichapisha hayo.
Katuga: Ulisema Mkutano wa Tar. 03/04 haukuwa na Mwenyekiti wa Mkutano?
Mnyika: Nilikujibu hivyo jana. Ni Majibu yangu.
Katuga: Ni Mikutano ya Chadema haina Mwenyekiti?
Mnyika: Sio mikutano yote haina Mwenyekiti.
Katuga: Chama chetu kina mikutano ambayo haina Mwenyekiti wambie Majaji?
Mnyika: Mikutano yetu ipo yenye Mwenyekiti na Mingine haina Mwenyekiti.
Katuga: Hiyo Mikutano ina minutes?
Mnyika: Haiwezi kuwa nazoKatuga: Ina agenda au haina?
Mnyika: Ipo yenye agenda na ambayo haina.
Katuga: Huo Mkutano wa Tar. 03/04 ulikuwa na agenda au hauna?
Mnyika: Ulikuwa na Mada sio agenda.
Katuga: Tofauti ya Mada na Agenda ni kwa mujibu wa Kamusi? Tusomeee agenda ni nini kwenye hii Kamusi?
Mnyika: Ni orodha ya mada zitakazojadiliwa. Soma sasa maana ya Mada hapo?
Katuga: Soma mada hapo
Mnyika: Ni jambo linalojadiliwa au kuzungumzwa. Umeona sasa nilikuwa sahihi anamrudishia Kamusi lake.
Katuga: Utofauti ni nini?
Mnyika: Huoni ni maneno mawili tofauti hapo na maana zake zinatofautiana nyingine ni orodha ya mada na nyingine ni jambo mahsusi. Hujaelewa nini? Sisi tulikuwa na mada.
Katuga: Kwahiyo kama hakukuwa na agenda mzungumzaji alikjwa huru kuzungumza chochote?
Mnyika: Nimesema kulikuwa na mada mahsusi.
Katuga: Ulisema uasi sio kosa kisheria kwakuwa uliwahi kusikia mwalimu nyerere akisema anataka kuona vijana waasi dhidi ya mifumo kandamizi?
Mnyika: Sahihi Katuga: Mbona una sana?
Mnyika: Inawezekana akili inafikiri haraka zaidi najua unachotaka. Kwahiyo ni suala la kupunguza uwezo wa kufikiri. Uliza maswali nitakujibu.
Katuga: Uelewa wako wa kisiasa ni nini?
Mnyika: Kupinga au kukataa kwa nguvu kubwa sana jambo fulani. Katuga: Uhasi dhidi ya Uchaguzi tafsiri yake ni nini?
Mnyika: Unasema ni Uhasi au Uasi? Katuga: Huo huo. Maana yake ni nini?
Mnyika: Kupinga au kukataa uchaguzi kwa njia mbalimbali za kidemokrasia ikiwemo boycot, maandamano.
Katuga: Neno demokrasia umeliweka kwenye maana ya uasi?
Mnyika: Neno Demokrasia nimelitumia mara nyingi. Katuga: Kazi yangu kukuonesha ulivyo Muongo?
Mnyika: Kazi yangu mimi ni kusema ukweli na Haki. Kila mmoja afanye kazi yake.
Sehemu ya 319
Katuga: Kama Katibu Mkuu wa Chama chama chako kilishiriki uchaguzi?
Mnyika: Kilizuiwa Kushiriki?
Katuga: Kwenye hotuba ya Mwenyekiti ya Tar. 03/04 je ulisikia akisema kama unategemea kuwa mbunge sahau?
Mnyika: Aliwaambia uchaguzi utaahirishwa.
Katuga: Hotuba ya Mwenyekiti alisema na mimi nina nia ya kugombea katika kacheo fulani sahau?
Mnyika: Toa neno sahau weka neno utaahirishwa.
Katuga: Kama Chama cha siasa kama mlijiandaa kushiriki uchaguzi wa mwaka 2025.
Mnyika: Tulijiandaa vizuri sana.
Katuga: Mlijiandaa kushiriki uchaguzi kwa mujibu wa Katiba?
Mnyika: Kwa mujibu wa Katiba iliyopo na marekebisho ya Katiba tuliyohitaji.
Katuga: Kwa haki hiyo hiyo ambayo Chadema alikuwa nayo na Vyama vingine vilikuwa na haki hiyo hiyo?
Mnyika: Haki ya kushiriki uchaguzi huru, wa haki na halali kila mtu anayo.
Katuga: Mwenyekiti alisema tutazuia uchaguzi kwa njia ya kidemokrasia ulisema hivyo?
Mnyika: Sikutumia exactly maneno hayo Sikumbuki kama nilisema kama unavyotamka hapo. Mimi nilisema njia zilizotumika.
Katuga: Je hizo njia za kuzuia uchaguzi zilikuwa ni zipi?
Mnyika: Nilisema.
Katuga: Kuhamasisha uasi ni njia ya kidemokrasia.
Mnyika: Ndio
Katuga: Kuzuia uchaguzi usifanyike ni njia ya kidemokrasia kwa nguvu zote?
Mnyika: Kwa nguvu zote za kidemokrasia ni njia ya kidemokrasia.
Katuga: Kwahiyo ni maneno yako kuwa vyama vingine havikupaswa kushiriki?
Mnyika: Unasema wewe sio mimi.
Katuga: Uchaguzi huru, haki na halali je wa mwaka jana vyama vilikuwa na haki hiyo au havina?
Mnyika: Ni suala lao wenyewe kuitumia hiyo haki au la? Sijasema kama uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa huru na haki na halali.
Katuga: Kama Chama kimoja kinaenda kushiriki Uchaguzi ni demokrasia gani kwenda kuzuia?
Mnyika: Demokrasia ya kupinga na kuzuia uchaguzi au kuahirisha uchaguzi
Katuga: Njia gani itakayotumika ya kidemokrasia itakayotumika kumzuia mtu?
Mnyika: Ukienda kupiga kura peke yako wenzako wasiende hakutakuwa na uchaguzi hapo.
Katuga: Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema kila mtu anapaswa kuamini chochote ili mradi havunji sheria.
Mnyika: Inaruhusu.
Katuga: Je inaheshimu imani ya mtu ilimradi asivunje sheria?
Mnyika: InaruhusuKatuga: Je inaelekeza kumzuia mtu asiyeamini kitu fulani?
Mnyika: Inaelekeza kumueleimisha mtu.
Katuga: Sikiliza maswali kama mtu mwenye akili timamu.
Mnyika: Sikiliza Majibu yangu kama mtu mwenye akili timamu. Itakusaidia.
Katuga: Mwenyekiti kusema tutakinukisha, tutaenda kuzuia uchaguzi alilenga kunishikiza Serikali kufanyike mabadiliko ya sheria na Katiba?
Mnyika: Hapana. Hatukulenga Serikali. Maneno yetu tuliyaelekeza kwa umma na wananchi kwa ujumla.
Katuga: Huo msimamo wa No reforms No Election ulitekelezwa na nani?
Mnyika: Kamati Kuu. Katuga: makamu mwenyekiti nae aliendeleza nia ya no reforms: No election?
Mnyika: Yupi huyo? Wako wawili.
Katuga: Bara?
Mnyika: Chama kilifungiwa kwa siku 309 kutokufanya hiyo mikutano.
Katuga: Viongozi waliendelea kuhamasisha umma kuhusu nia hiyo?
Mnyika: 09th June 2025 Chama kilifungiwa kufanya shughuli zake.
Sehemu ya 320
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Katibu Mkuu wa Chadema John
Mnyika.Katuga: Je huyu Heche katika kueneza hiyo nia alikuwa anaongea na waandishi wa habari?
Mnyika: Nimekwambia Tarehe 10/04 Chama kilifungiwa.
Katuga: Katuga una akili kweli?
Mnyika: Wewe unajiona una akili kweli?
Mhe. Lissu: Mheshimiwa haya maswali kila saa ya kwamba shahidi ana akili au vipi? Sheria inakataza. Kama hana maswali akae tu.
Katuga: Unajua au hujui Heche aliwahi kuongea East Africa radio kuhusu nia ya kuzuia uchaguzi?
Mnyika: Sijui Katuga: Alitangaza kwamba uchaguzi wa 2025 hautakuwepo?
Mnyika: Sijui.
Katuga: Unajua au hujui kwamba katika uchaguzi wa 2025 kulikuwa na jaribio la kuuzuia huo uchaguzi, kufanya fujo.
Mnyika: Ninachojua kuna Mauaji yalifanyika.
Katuga: Je kulikuwa na jaribio la kuzuia uchaguzi kwa kuchoma vituo vya kura?
Mnyika: Sijui ndio maana tulitaka uchaguzi huru sisi.
Katuga: Ulikuwa nchini au haukuwa nchini?
Mnyika: Nilikuwa nchini?
Katuga: Ulijitokeza au hukujitokeza kwenye zoezi la uchaguzi?
Mnyika: Sikujitokeza kwasababu hakukuwa na uchaguzi.
Katuga: Kwa Msimamo wenu hakukuwa na uchaguzi?
Mnyika: Hakukuwa na uchaguzi huru, haki na halali.
Katuga: Ila nia ya kuzuia uchaguzi inadhihirika kwa maneno hayo?
Mnyika: Sio sahihi.
Katuga: Uchaguzi ule kuna mali za watu zilichomwa moto.
Mnyika: Nilijua kupitia hotuba ya Chande. Katuga: Vilichomwa havikuchomwa?
Mnyika: Najua viliungua moto. Mambo ya kuchomwa sijui aliyechoma.
Katuga: Vituo vya mwendokasi je?
Mnyika: Nilipita na kuona vimeungua. Simjui aliyechoma.
Katuga: Maneno ya Mwenyekiti ya Tar. 03/04 kuwa tutakinukisha, tutazuia uchaguzi ni haki ya umma kutafsiri na kufanyia kazi?
Mnyika: Ni haki.
Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema ni haki pia umma kuchocheka na kukata wapiga kura vidole.
Mnyika: Sio haki.
Katuga: Mwenyekiti aliwaambia umma kuzuia uchaguzi zoezi hilo lifanyike lini?
Mnyika: Hakuwaambia.
Katuga: Ni haki au sio haki kuzuia uchaguzi sio ya kupiga kura?
Mnyika: Sio haki.
Katuga: Ulisema wewe ni accounting officer? Una elimu yoyote ya hesabu?
Mnyika: Nina elimu ya miaka 3 Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuhusu Bussiness Administration and Accounting sina Award yoyote.
Katuga: Ulisikiliza taarifa ya Chande yote au kipande?
Mnyika: Sio taarifa ni hotuba. Nilisikia yote.
Katuga: Ulisikia Chande akisema matukio ya Otober yalitokana kwasababu ya ushawishi wa wanasiasa kufanya machafuko?
Mnyika: Kwenye hotuba kuna vyanzo na viashiria
Katuga: una akili timamu kweli?
Mnyika: Nina akili timamu kuliko wewe na Maboss zako wote.
Katuga: Mimi ndio nimekuuliza una akili timamu?
Mnyika: Watu wasio na akili timamu mara nyingi huwa wanapenda kudhani wenye akili hawana akili. Sasa nina akili kuliko wewe.
Katuga: Mwenyekiti alikuwa anataka mabadiliko ya kisheria na kikatiba kwa njia zipi?
Mnyika: Alisema njia za kidemokrasia.
Katuga: Utofauti wa Chande na aliyosema mwenyekiti ni upi?
Mnyika: Chande alisema wakati Mwenyekiti yuko jela na Mwenyekiti alisema wakati Chande hajafanya kazi zote.
Katuga: Kwamba Kauli mbiu ni tumteteee kwa nguvu zote?
Mnyika: Kwamba Kauli Mbiu yenu huko Serikalini ni Tumfunge kwa Nguvu zote? Si ndio?
Katuga: Ulisema ulikuwa mbunge wa wapi na wapi?
Mnyika: Ubungo na Kibamba.
Katuga: Kwahiyo unauelewa kidogo wa masuala ya Sheria?
Mnyika: Nimetunga sheria nafahamu
Sehemu ya 321
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika.
Katuga: Tanzania ni nchi huru na ina katiba yake?
Mnyika: Yes ina katiba yake na haiongozwi na Katiba pekee ipo Mikataba ya Kimataifa na Sheria zingine.
Katuga: Mahakama ndio chombo cha Mwisho kutamka mtu ana hatia au hana hatia?
Mnyika: Mahakama za Tanzania na Kimataifa.
Katuga: Mahakama ni Chombo cha Mwisho kwa mujibu wa Katiba kuamua kama mtu ana hatia au hana hatia? Mnyika: Sahihi.
Katuga: Je ni kweli ni Mahakama itakayotamka ushahidi huu unatosha au hautoshi kumtia mtu hatiani?
Mnyika: Sahihi.
Katuga: Uliposema mshitakiwa aliposema kuwa mshitakiwa ameshitakiwa kuwa ni kesi ya uongo kwa majibu yako yaliyopita wambie Majaji kwamba kwenye hizo kesi ulizosema ni za uongo ni kesi gani uliitaja?
Mnyika: Zilifutwa zote kwasababu zilikuwa za uongo.
Katuga: DPP akifuta kesi anaweza kuirudisha au hawezi kuirudisha?
Mnyika: Anaweza kuirudisha. Katuga: DPP akifuta kesi anasema kwa maslahi mapana ya Jamhuri?
Mnyika: Sio sababu pekee.
Katuga: Mihimili ya dola ya Tanzania unaijua?
Mnyika: Mitatu ipo, naijua
Katuga: Kwenye mambo ya kisheria unajua muhimili gani unahusika?
Mnyika: Ndio.
Katuga: Ni Bunge pekee lenye mamlaka ya kutunga sheria?
Mnyika: Sio Bunge pekeee.
Katuga: Mahakama ina jukumu la kutafsiri sheria?
Mnyika: Sio jukumu pekeee.
Katuga: Serikali kazi yake ni kusimamia sheria?
Mnyika: Sio kazi pekeee
Katuga: Hata Bunge linaweza kusimamia sheria pia. Wanaisimamia serikali pia.
Katuga: Vyombo vinavyotumika kulinda amani?
Mnyika: Vyombo vya serikali kama Polisi na pia mihimili yote pia.
Katuga: Vyombo ulivyotaja vyenye jukumu la kulinda Amani viko chini ya nani?
Mnyika: Vyombo gani?
Katuga: Polisi na Jeshi?
Mnyika: Chini ya Rais.
Katuga: Unapotishia kuvunja amani ni tishio la Rais na Vyombo vyake?
Mnyika: Sio kweli, sio kila tishio la Amani ni tishio kwa Rais na vyombo vyake.
Katuga: Siku ya Tarehe 29/10 Amani ilikuwepo au haikuwepo?
Mnyika: Kulikuwa na vurugu lakini Amani ilikuwepo si Serikali yenyewe imesema kulikuwa na Amani.
Katuga: IGP si alitangaza kukaa ndani tarehe 29/10?
Mnyika: Ndio Katuga: Alisema IGP kuwa msitoke?
Mnyika: Hatuwezi kumuamini hata kama alisema.
Katuga: Kule Goba hukusikia mitutu ya Bunduki?
Mnyika: Nani amekwambia nilikuwa Dar es salaam? Nilisema nilikuwa Nchini.
Katuga: Vyombo vya Ulinzi vilikuwa na jukumu la kurudisha amani?
Mnyika: Sifahamu.
Katuga: Kuchoma mali za watu, miundombinu na kukata watjmu vidole ni uvunjifu wa Amani?
Mnyika: Ni uvunjifu wa Sheria. Katuga: Unafahamu au hufahamu kuwa ni uvunjifu wa amani?
Mnyika: Ni uvunjifu wa sheria.
Katuga: Kutishia kuivunja amani ni kuitishia serikali yenye jukumu la kulinda hiyo amani? Unafahamu hilo?
Mnyika: Ndio nasikia kwako sifahamu mimi.
Katuga: Wambie Majaji kama unafahamu au hufahamu kwamba kila baada ya miaka mitano ni lazima kuwe na uchaguzi Mkuu?
Mnyika: Sio lazima.
Katuga: Ibara ya 65 kwamba Bunge litavunjwa kila baada ya miaka mitano.
Mnyika: Zipo ibara nyingi zinazosema extension ya Bunge na masharti mengine kuhusu Bunge.
Katuga: Kila Bunge linapovunjwa ndio ukomo wa Rais si ndio?
Mnyika: Sio kweli Bunge linavunjwa lakini Rais anaendelea kuwa Rais hadi atakapopatikana Rais mwingine.
Katuga: Ukomo wa term ya Urais unaisha Bunge likivunjwa si sahihi ibara ya 38?
Mnyika: Inasema kwa kuzingatia na taratibu zingine. Term inaisha lakini urais anaendelea nao hadi apatikane Rais mwingine ndio maana anaweza kuitisha tena Bunge.
Katuga: Mbona hujibu wewe unamuangalia jamaaa?
Mnyika: Namuangalia Jaji na wewe kati yenu nani ndio jamaaa?
Katuga: Kutishia kuivunja Sheria ni kuitisha Serikali?
Mnyika: Sio lazima.
Katuga: Serikali inaweza kutishika na tishio la kuvunja sheria?
Mnyika: Sio lazima.
Sehemu ya 322

Katuga: Ulisema mlipokamatwa na Sugu wenzako walipelekwa kusikojulikana?
Mnyika: Ndio
Katuga: Kusikojulikana ni wapi?
Mnyika: Ndio maana hakujulikani
Katuga: Ni sehemu wewe usiyoijua au wewe usikokujua?
Mnyika: Nisipopajua na hapajulikani.
Katuga: Unajua ama hujui huyu aliyepelekwa kusikojulikana alipelekwa nyumbani kwake?
Mnyika: hata mimi nilisema hapa kuwa nilipelekwa central na baadae nyumbani.
Katuga: Yeye aliiambia Mahakama kuwa alipelekwa Iringa kuna mbu wakubwa
Mhe. Lissu: Mimi sikusema mambo ya Iringa sijui ametoa wapi hili swali. Mimi sikupelekwa iringa na sikusema hivyo.
Jaji Ndunguru: Acha tu sisi tunaandika majibu yake. Maswali hatuna shida nayo.
Katuga: Kuonesha jinsi gani uanaharakati una malipo...
Mnyika: Nilisema Gharama hayo malipo unayatoa wapi?
Katuga: Milioni 350 ulisema hamjarudishiwa?
Mnyika: Hadi leo ndio Jamhuri walipaswa kutulipa hizo pesa.
Katuga: Ulitaja kesi nyingi sijui Nyamongo au wapi je umewatajia namba za hizo kesi?
Mnyika: Namba za nini nitaje? Sijataja.
Katuga: Je hati za mashitaka ulileta?
Mnyika: Sijaleta. Mimi sio shahidi wa Jamhuri.
Katuga: Je Mbowe nae alifunguliwa kesi ya Uongo ya ugaidi?
Mnyika: Sahihi.
Katuga: Ulisema alienda ikulu ilikuuma sana?
Mnyika: Inaniuma kumsingizia mtu ugaidi halafu mawakili wa serikali mmeshindwa kuthibitisha kesi inafutwa halafu gaidi anaenda kupokelewa ikulu. Hiki ndio kinaniuma na ni uongo huu.
Katuga: Unamjua Chura? Nitafute baadae nikusimulie kwanini ana mabaka. Unajua Chura ana mabaka..
Mnyika: Umesema nikutafute baadae. Kwahiyo kama unaendelea kumuhadisia hapa wahadisie majaji mimi nitakutafuta baadae. Sasa hivi sikusikilizi. Watu wanacheka.
Katuga: Sasa Mbowe alishitakiwa na watu wengine ambao walikuwa wanajeshi?
Mnyika: Nilisikia Mahakamani.
Katuga: Wale Walinzi wake hawakuwa wanaharakati wa Katiba Mpya?
Mnyika: Kumlinda Mwenyekiti ni kuwa Mwanaharakati wa Katiba Mpya pia.
Katuga: Ulisema ulikuwa afisa maduhuri
Mnyika: Ni Masuhuli. Hiyo maduhuri kaitumie kwenye ofisini kwenu.
Katuga: Ulihusika kuwalipa posho?
Mnyika: Posho za Safari nilikuwa nawalipa.
Katuga: Je ulikuwa uanatembea nao mnalala pamoja na kula nao kujua yote?
Mnyika: Sikuwa natembea nao ili kujua yote.
Katuga: Ulikuwa pia hujui ushahidi wa tuhuma walizokuwa nazo kwasababu ulikuwa hutembei nao?
Mnyika: Nilisikia mahakamani wanayosema. Kwani mapolisi wakienda kutoa ushahidi walikuwepo?
Katuga: Ulisema kesi hii ni mwendelezo wa serikali kubambikiza kesi?
Mnyika: Ndio kupitia jeshi la polisi lenye wajibu wa kulinda raia na mali zake. Lakini sio kubambikizia watu kesi. Katuga: Ni sheria gani inayompa Mwenyekiti wa Chadema kinga?
Mnyika: Kama amefanya kosa hana kinga lakini hana kosa lolote.
Sehemu ya 323
Wakili wa Serikali Katuga anaendelea na maswali yake ya Kiwaki ila Mnyika anampa za uso.
Katuga: Unasema Msajili aliwaandikia barua kuhusu Kauli za Mwenyekiti?
Mnyika: Ndio
Katuga: Nae alimtuhumu Mwenyekiti?
Mnyika: Tuhuma za kisiasa ndio alituhumiwa nazo.
Katuga: Kuhusu kusaini au kutokusaini sheria hailazimishi?
Mnyika: Hailazimishi. Katuga: Kushiriki uchaguzi ni haki ya Kikatiba?
Mnyika: Ndio ni kweli.
Katuga: Kunyimwa kutoshiriki uchaguzi kwa chama chenu na kuvunjwa kwa haki hiyo sheria inaruhusu kuidai Mahakamani haki hiyo?
Mnyika: Sio lazima uende mahakamani.
Katuga: Mlienda Mahakamani kudai haki yenu ya Kikatiba au hamkwenda?
Mnyika: Sio lazima twende Mahakamani soma kesi ya Kubenea Mahakama ilisema haki za kisiasa zinapaswa kutafutwa kwa njia za kisiasa pia.
Katuga: Wanasiasa wa Chadema ni dhumuni lao kushika nafasi ya uongozi kwenye hili Taifa?
Mnyika: Sio dhumuni pekee.
Katuga: Ulisema una akili nyingi sasa nikuulize swali...
Mnyika: Nilichosema nina akili nyingi kuliko wewe na Maboss zako. Sio nina akili kuliko watu wote Duniani. Ni muhimu ukaelewa ni akili nyingi kuliko wewe Katuga na Maboss zako.
Katuga: Kufanya mapinduzi ni njia mojawapo au sio njia ya kushika dola?
Mnyika: Ni njia lakini sio njia ya kidemokrasia.
Katuga: Uchaguzi wa Tanzania ulisema sio nini?
Mnyika: Sio huru, sio haki na sio halali.
Katuga: Ule uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa wa nini?
Mnyika: Ulikuwa ni uporaji wa mamlaka ya wananchi wa kuchagua viongozi wanaowataka. Hakukuwa na uchaguzi, ni uchafuzi na uharibifu wa rasilimali za Taifa.
Katuga: Mheshimiwa imefika saa saba tumesimama toka asubuhi naomba twende Break kwa lisaa limoja na nusu.
Baada ya Break, Mahakama imerejea.
Tunaendelea sasa. Anasimama Ajuaye anasema tunataka kuendelea.
Jaji Ndunguru anamwambia John Mnyika nakukumbusha uko chini ya kiapo tuendelee sasa.
Katuga: Iambie Mahakama hii uwepo wa Kesi ya Khatib Gandi?
Mnyika: niliwahi kusikia.
Katuga: Kwenye uamuzi wake kesi sio mpira wa miguu inayohitaji Ushabiki?
Mnyika: Sijawahi kusikia.
Katuga: Kesi ya jinai sio hisia na ushabiki?
Mnyika: Najua
Katuga: Kuwa Katibu Mkuu ni muhusika wa kujua idadi au majina ya Chadema?
Mnyika: Sihusiki moja kwa moja. Wapo wasaidizi.
Katuga: Kazi ya kujua idadi ya wanachama ipo kwa nani?
Mnyika: Katibu Mkuu na Kamati Kuu.
Katuga: Kuna malalamiko mitandaoni kuhusu posho za Chama unafahamu?
Mnyika: Sifahamu
Katuga: Unafahamu kuna mwanachama aliyeitisha waandishi wa habari kutangaza kilichopangwa kufanywa Oktoba 2025?
Mnyika: Sifahamu. Mwanachama yupi huyo unayemzungumzia.
Katuga: Unafahamu mwanachadema huyu kwenye taarifa yake kwa umma kuwa kulikuwa na mifumo maalumu ya kuwasiliana ili kutekeleza nia ya kuvuruga Uchaguzi?
Mnyika: Sifahamu
Katuga: Kulikuwa na mipango ya kusimamia vurugu siku tofauti tofauti.
Mnyika: Sifahamu.
Katuga: Je uliwahi kupanga ama kujitokeza kumpinga Mwanachadema anaitwa Ishengoma wa Chadema kwamba matukio ya Tar. 29 chama kilihusika?
Mnyika: Taarifa unaijua wewe mimi sifahamu.
Katuga: Kwa mujibu wa hotuba ya Chande zilikuwa ni vurugu zilizoratibiwa na kupangwa?
Mnyika: Nilisikia Chande alisema hivyo. Kukubaliana nae ni jambo tofauti.
Katuga: Kuna watu walikamatwa kutokana na hizo vurugu za mwaka jana?
Mnyika: Walikamatwa na kuachiwa.
Katuga: Hao waliokamatwa walihojiwa kituo cha Polisi?
Mnyika: Sikuwepo.
Katuga: Waliofanya fujo zilitokana na kauli za kipenzi chao mwenyekiti wa Chama?
Mnyika: Sijaongea nao
Katuga: Uliwahi kuongea na mtu aliyekamatwa kwa kesi za uhaini mwaka jana?
Mnyika: Sijawahi kuongea na mtu wa aina hiyo.
Katuga: Tafsiri isiyo halali ni ipi?
Mnyika: Chochote kinachoweza kutafsirika na mahakama kuwa ni kuvunja sheria.
Katuga: Demokrasia ni nini?
Mnyika: Limeundwa na maneno mawili demo and cracy yaani utawala wa watu kwa ajili ya watu. Lazima uundwe na watu na ufanye kazi kwa ajili ya watu.
Sehemu ya 325
Wakili wa Serikali Katuga anaendelea na maswali yake ya Kiwaki ila Mnyika anaendelea kumshona bila ganzi.
Katuga: Soma maana ya Kamusi hapa?
Mnyika: Ulipofungua hakuna maana ya Demokrasia labda fungua sehemu husika.
Katuga: Huwezi kufungua?
Mnyika: Demokrasia ni mfumo wa utawala ambao unapatikana kwa matakwa ya umma.
Katuga: Hiyo maana na ile yakwako vinafanana?
Mnyika: Vinakaribiana.
Katuga: Ni kweli kwamba Demokrasia inahusiana na utawala?
Mnyika: Inahusiana na mamlaka ya wananchi pia.
Katuga: Kama Katibu Mkuu Kuzuia uchaguzi kwa njia ya Demokrasia ukimzuia ni demokrasia kwa tafsiri hiyo? Hayo mamlaka uliyapata lini?
Mnyika: Sina hayo mamlaka Katibu Mkuu
Katuga: Mwenyekiti wako amepata mamlaka wapi ya kuzuia uchaguzi kidemokrasia?
Mnyika: Alipata kutoka kwa azimio la Chama la Mkutano Mkutano la Tar. 21/01/2025.
Katuga: Mkutano Mkuu wa Chadema una watu wangapi?
Mnyika: 1000 na zaidi.
Katuga: Hao watu elfu moja ni asilimia ngapi ya watanzania?
Mnyika: Huo ni mkutano wa uwakilishi kutoka maeneo mengin, ukisema asilimia labda uwe hujielewi.
Katuga: Nimemaliza naomba waendelee wengine.
Ajuaye: Amesimama Cathbert Mbiringe.
Cathbert: Chama chenu ni cha ukweli na uwazi?
Mnyika: Ndio Cathbert: Wewe ni accounting officer?
Mnyika: Ndio
Cathbert: Ni kweli mnakusanya tonetone?
Mnyika: Ni kweli
Cathbert: Na mmeshatoa takwimu za tonetone la Baraza Kuu la Umma.
Mnyika: Milioni 302 hadi mara ya mwisho.
Cathbert: Unafahamu au hufahamu kuna milioni 100 nyingine ilichangwa?
Mnyika: Sifahamu. Cathbert: Mara ya mwisho mmelipa watumishi wa Chama lini?
Mnyika: Mwezi uliopita.
Cathbert: Ikitokea kuna ushahidi kuwa hujalipa mishahara toka mwaka uliopita nani atakuwa muongo?
Mnyika: Wote watakuwa wakweli huwezi kukifungia chama siku 309 halafu ukazuia ruzuku ukategemea wafanyakazi walipwe. Nilichosema ni mara ya mwisho tumewalipa mwezi uliopita hizo posho zao lakini kuna madeni mengine. Mbona linaeleweka.
Cathbert: Viongozi wakuu wa Chama ni akina nani?
Mnyika: Lissu, Heche, Said Mzee, Mnyika, Amani Golugwa, Ali Ibrahim Juma. Hapo ni kuanzia Mwenyekiti hadi Naibu Katibu Mkuu wote wawili.
Cathbert: Ukiachana na Mwenyekiti na wewe kuna mwingine yoyote ambae hadai Posho?
Mnyika: Hata mimi nadai posho.
Cathbert: Kwanini hujatumia tonetone kulipa mishahara?
Mnyika: Tonetone inahusika na shughuli maalumu huwezi kutoa kwa mfano pesa za Baraza Kuu kwenda kulipa mishahara.
Cathbert: Huoni fedha hizo zitatumika kwenye utakatishaji wa fedha?
Mnyika: Mamlaka zipo na hela zetu zinapitia kwenye account zinazojulikana kwahiyo kama kuna shida maana yake hatua zichukuliwe. Huwa tunaweka account hadharani na hatuulizi watu kwamba hizo pesa mmezipata wapi?
Cathbert: Hizo pesa mnalipa kwenye account zao au vipi?
Mnyika: Kwa kutumia account zao huwa tunalipa.
Cathbert: Nimemaliza. Anasimama Ajuaye sasa.
Ajuaye: Ulisema uasi ni nini?
Mnyika: Ni kupinga na kukataa jambo kwa nguvu kubwa kupitia njia za kidemokrasia.
Ajuaye: soma maana ya uasi kwenye Kamusi.
Mnyika: anaisoma. Anasema Mwalimu Nyerere alitumia neno uasi kwasababu lina maana pia kwenye siasa ndio maana halijawahi kuwa kosa.
Ajuaye: Kamusi ya siasa iko wapi?
Mnyika: Hatuna kamusi ni matumizi ya maneno ambayo ipo kwenye siasa.
Ajuaye: Wakati mnapanga kuhamasisha uasi mlipanga kukiuka sheria na kuvunja sheria kwa mujibu wa kamusi hii?
Mnyika: Wakati tunapanga No Reforms: No Election hatukutumia Kamusi. Na hatukupanga uhalifu wowote.
Ajuaye: Kwahiyo unapingana Kamusi hii?
Mnyika: Hiyo kamusi sio nyaraka yenye maneno yote ya Kiswahili na maana zote. Ndio maana zinarekebishwa na maneno yanaongezwa na kupunguzwa pengine.
Hii inaitwa Ajuaye Hajui.
Sehemu ya 326
Ajuaye: Ni ushahidi wako kuwa vyombo vya habari vilirusha?
Mnyika: Ni vikao Vinavyojumuisha watu wanaofahamika sio kama ile mikutano ya hadhara ambayo yeyote anakuja.
Ajuaye: Si ulisema mlitoa taatifa kwa umma.
Mnyika: Uwe unaelewa, hatukualika umma uje kwenye kikao. Tulitoa taarifa kwa umma kuelezea uwepo wa kikao hicho na kualika waandishi wa habari.
Ajuaye: Kikao kilikuwa na sehemu mbili zipi na zipi?
Mnyika: Hotuba za viongozi wakuu na baadae tukawaruhusu waaandishi wakaendelee na majukumu yao na sisi tuendelee na mambo mengine na watia nia.
Ajuaye: Nani alifungua hicho Kikao?
Mnyika: Katibu Mkuu baada ya hapo nilimkaribisha Mwenyekiti azungumze na baadae tukaendelea na mambo mengine.
Ajuaye: Kati yako wewe na Tundu Lissu nani alikuwa Msemaji Mkuu?
Mnyika: Mwenyekiti Lissu
Ajuaye: Nani alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano?
Mnyika: Nilishasema hakukuwa na Mwenyekiti
Ajuaye: Tundu Lissu alikuwa ni nani?
Mnyika: Tundu ni Mwenyekiti wa Chama Taifa hakuwa Mwenyekiti wa Kikao wala Mkutano.
Ajuaye: Nani alikuwa muelimishaji?
Mnyika: Viongozi wote wakuu.
Ajuaye: Hayo mafunzo mliyatoa kwenye ufunguzi?
Mnyika: Kwenye Mkutano wetu wote.
Ajuaye: kwa vile wewe ni layman huna utaalamu wowote wa kuchambua hati ya mashitaka yoyote?
Mnyika: Ninao utaalamu wa ki layman huo huo.
Ajuaye: Kama mtu hajakubaliana na msimamo wenu atauona uchaguzi ni wa haki?
Mnyika: Kwa maoni yake yeye na hawezi kufanya msimamo wa Chadema ukabadilike na usiwe wa Haki.
Ajuaye: Naomba niishie hapa nimkaribishe Job Mrema. Job Mrema: Naomba nimpe hii Kamusi na imeandikwaje hapo?
Mnyika: Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya Mwaka 2015. Kwa kifupi ametoka Abdala amekuja Dullah hapa.
Job Mrema: Hebu soma hapo kwenye Dibaji kwenye Kamusi
Mnyika: Kamusi imeandikwa na BAKITA na wapo waliokesha wakifanya utafiti.
Job Mrema: Ni sahihi kwamba kwa mujibu wa mamlaka ya kisheria BAKITA ndio wamepewa mamlaka ya kufanya tafiti hiyo waliyofanya?
Mnyika: BAKITA sio chombo pekee wananaoweza kufanya utafiti
Job Mrema: Kamusi uliyokuwa unapewa usome maana za maneno ndio hiyo au nyingine?
Mnyika: Ndio
Job Mrema: Hiyo Kamusi niliyokupa ndio chombo pekee cha kutoa tafsiri ya maneno?
Mnyika: sio chombo pekeee.
Job Mrema: Ulisema michango imefika milioni 302?
Mnyika: Nilisema.
Job Mrema: Mmeshatumia kiasi gani kwenye hiyo milioni 302?
Mnyika: Nilikwambia hii ni kwa ajili ya Baraza Kuu. Job Mrema: Ulishindwa kutaja majukumu yako?
Mnyika: Sio kweli.
Job Mrema: Ulisema kazi zako ni zipi?
Mnyika: Mwenyekiti wa Sekretarieti, Msimamizi wa shughuli za kila siku za Chama, Msimamizi wa vikao mbalimbali na muandaaji.
Job Mrema: Umeulizwa maswali mwngi umesema hujui ni sahihi?
Mnyika: Nimeulizwa maswali mengi nimeyajibu. Hoja sio sijui hoja nimesema sijui kwenye jambo gani? Siwezi kujua kila kitu kwenye taasisi.
Job Mrema: Ni sahihi kuna Katibu Mkuu wa Chadema hajui anachokifanya?
Mnyika: Hata wewe unajua kuwa najua ninachokifanya.
Job Mrema: Kuna watu wanakusaidia saidia?
Mnyika: Majukumu ya Katibu Mkuu ni ofisi na ina watu wengi wa kuyafanya.
Sehemu ya 327
Job Mrema: Katika Utendaji wako unabebwa na Mwenyekiti?
Mnyika: Nabebwa na Katiba ya Chama.
Job Mrema: Mwenyekiti amekuja kukuelekeza kwasababu umeshindwa kujibu maswali?
Mnyika: Mwenyekiti amekuja hapa kuongea na mimi kama mshitakiwa na sio Mwenyekiti wa Chadema.
Job Mrema: Fujo ni nini shahidi?
Mnyika: Fujo ni fujo.
Job Mrema: Kwa mujibu wa Kamusi je?
Mnyika: Tafuta uniletee sasa.
Job Mrema anatafuta pale. Maana ya fujo kwenye kamusi ameilata Lakini Mheshimiwa muda umeisha. Ninahitaji kuendelea
Jaji Ndunguru: Uliza swali mi nasikia fujo, sokomoko sijui nini sielewi hata hapo swali ni nini?
Naona mnaongea ongea.
Amerudia swali lake.
Mheshimiwa Lissu anasema swali hilo lina shida.
Jaji Ndunguru sasa kwa vile muda umeisha basi tukutane kesho asubuhi na shahidi huyu.
Shahidi tukutane kesho.
Inapigwaa Court....!!