Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

Ukimfuatilia vizuri Katuga, uulizaji wake wa maswali ni ule wa propaganda za ccm, na sio kesi ya msingi iliyopo mahakamani.
 
Ukihitaji taarifa za mtu za bank unapewa kisheria kwa kificho ama? Maana nataka kujua wakili yoyote akiwa na shaka na miamala ya mtu anaweza kwenda kupewa tu? Kama ni kisheria akina Katuga wamepata hizo taarifa kisheria?
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 21.

KUHOJIWA NA NASSORO KATUGA

Nassoro Katuga: Shahidi, kama nimekupata unasema kwamba hii “No Reform, No Election” ilitangazwa na Mheshimiwa Freeman Mbowe?

Heche: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Shahidi, waambie Waheshimiwa Majaji kama alieleza kwamba tunaenda kuzuia uchaguzi wa 2025.

Heche: Sikueleza.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji hivyo hivyo, kama Freeman Mbowe alisema anaenda kuhamasisha uasi.

Heche: Hakusema.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama Freeman Mbowe wakati anaelezea “No Reform, No Election” alielezea masuala ya kukinukisha.

Heche: Hakusema.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama kwenye msimamo wa chama wa “No Reform, No Election” kuna maneno kwamba tutazuia uchaguzi.

Heche: Hakuna.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama kwenye maneno “Hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi” kuna maneno tunaenda kuhamasisha uasi.

Heche: Hapana.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama kwenye maneno ya “Hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi” kuna maneno tunaenda kukinukisha.

Heche: Hakuna.

Lissu: Muda, Waheshimiwa Majaji. Shahidi wangu amechoka, anahitaji break.

Jaji Ndunguru: Shahidi, hajisema kama amechoka.

Lissu: Mimi mwenyewe nimechoka. We all need a break.

MAHAKAMA: Kicheko.

Jaji Ndunguru: Upande wa mashitaka.

Ajuaye: Hatuna pingamizi, Waheshimiwa. Tunaomba tuhairishe.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, tunaomba kabla hamjaahirisha, mueleze mpaka Ijumaa.

Jaji Ndunguru: Shauri linahairishwa hadi kesho saa 3:00 asubuhi.

Shahidi hajamaliza kutoa ushahidi wake. Kesho ataendelea kutoa ushahidi.

TUKUTANE KESHO ASUBUHI.
 
Lisu ameuliza kuhusu uenguaji wa wagombea wa chadema kwenye chaguzi kadhaa zilizopita huko nyuma...vipi maswali hayo yana uhusiano gani na kesi yake ya uhaini?

..masuala ya uenguaji wa wagombea wa Chadema wakati wa uchaguzi yanajenga msingi wa kauli mbiu na msimamo wa Chadema wa " hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi. "
 
Lissu: Muda, Waheshimiwa Majaji. Shahidi wangu amechoka, anahitaji break.

Jaji Ndunguru: Shahidi, hajisema kama amechoka.

Lissu: Mimi mwenyewe nimechoka. We all need a break.
 
Kazi nzuri mkuu
Hope kesho pia tutaamka salama tuendelee kusikiliza mkuu Heche anavyo kichafua hapo.
 
Ukihitaji taarifa za mtu za bank unapewa kisheria kwa kificho ama? Maana nataka kujua wakili yoyote akiwa na shaka na miamala ya mtu anaweza kwenda kupewa tu? Kama ni kisheria akina Katuga wamepata hizo taarifa kisheria?
Bado ni kama tunazunguka mbuyu kwa speed sawa means hatuwezi kukutana...

Hakuna kificho kwenye suala la sheria
"Akina Katuga wamepata hizo taarifa kisheria?"

Hili swali ndilo lilitakiwa lifanyiwe kazi na majibu yapatikane kabla ya kufikia conclusion ya kutoa hukumu kwamba akina Katuga wamefanya makosa bila kujua wamefanya kisheria ama laa na ni sheria ipi imewapa mamlaka
 
Mkuu kwenye ushahidi huo huo ndio utajua kwenye vyombo vya dola hakuna watumishi bali uchafu wa hali ya juu.

..hili suala inabidi tuliangalie kwa pande zote yaani Shahidi[ Heche] vs Muendesha Mashtaka [ Katuga].

..wako wanaoamini kwamba credibility ya Heche imeharibika kwa majibu aliyoyatoa kuhusu magari na miamala yake.

..Je, tumejiuliza kuhusu credibility ya Muendesha Mashtaka, Nasoro Katuga, kama haikuharibika kutokana na maswali aliyouliza?

..Je, Majaji hawawezi kujiuliza kama Katuga amefuata mkondo wa sheria kupata taarifa binafsi za miamala ya benki ya John Heche? Je, watakuwa wameridhika?

..Ni kweli kwamba Heche ameharibu ktk majibu yake, lakini ni ukweli vilevile kwamba Katuga ameharibu ktk maswali aliyouliza.

..Kitendawili ni Majaji watatoa uzito kwa upande upi?

Cc Nguruvi3
 
Mimi nilijua unajua kisheria, lakini nijuavyo taarifa za kibenki za mteja ni Siri, sasa ulipoleta hili swala nikadhani unajua kisheria likoje. Kumbe na ww ni kama mimi kwenye hili.
 
Noted
 
Hiyo kesi ilikuwa inarushwa na serekali mubashara, gafla wakaacha. Sasa unadai wajibu kwa aliyejitolea huku ukiwaacha wenye wajibu! Serekali ingerusha live tuonr kila kitu bila kusubiri hisani ya yoyote
Huyo aliyejitolea Manyanda sijui alijipa hatimiliki ya kuripoti hapa kiasi ilikuwa akianza mwingine anamaindi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…