WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI
SEHEMU YA 18.
Nassoro Katuga: Kwanza, umemtaja jina hapa Mahakamani?
Heche: Sijamtaja.
Nassoro Katuga: Je, alikueleza kwamba amefanya mauaji haya ili akutishe wewe na uendelee na siasa wako?
Heche: Magufuli alisema kuwa mpaka 2020 upinzani utakuwa umeisha.
Nassoro Katuga: Je, alikwambia kwamba amemuua mdogo wako katika kukutisha wewe katika harakati zako za kisiasa?
Heche: Hakuniambia hivyo.
Nassoro Katuga: Kwa hiyo, sababu za huyo mtuhumiwa kufanya hivyo kwa Suguta Heche zimebaki kwa mtuhumiwa. Hapa Mahakamani hatuna.
Heche: Ni sahihi.
Nassoro Katuga: Unajua au hujui, kwenye jinai, sababu ya kumfanya mtu aachiwe ni ushahidi aidha haujatosheleza?
Heche: Kuna rushwa, upendeleo, sababu ni nyingi.
Nassoro Katuga: Kati ya hayo unayotueleza, wewe ni sababu ipi uliyoeleza ilifanya aachiwe aliyemuua mdogo wako?
Heche: Ni uonevu wa kisiasa na upendeleo.
Nassoro Katuga: Ulisema mtu aliyemuua mdogo wako alikuwa na nia ya kukukomoa na kwamba wanaweza kukufanyia chochote na hatua zisichukuliwe?
Heche: Ni sahihi.
Nassoro Katuga: Huyu mdogo wako anao wazazi?
Heche: Mama yake yupo, ila baba alifariki.
Nassoro Katuga: Ni ukweli, kwa mujibu wa dini na misemo ya Kiswahili, kwamba uchungu wa mwana aujuaye mzazi?
Heche: Ni kweli.
Nassoro Katuga: Kati ya mama yako na wewe, nani anauchungu zaidi?
Heche: Mimi nina uchungu, lakini huyo mama yangu nenda kamuulize yeye.
Nassoro Katuga: Kwa nini walichomfanyia mdogo wako ilikuwa kukukomoa wewe na siyo mzazi wake?
Heche: Mimi najua ni mimi.
Nassoro Katuga: Umeiambia Mahakama huyo polisi aliyemuua alikutishia kwa jambo gani?
Heche: Kunitishia nisiendelee na siasa.
Nassoro Katuga: Ulisema ni mwaka gani ulimpoteza mdogo wako?
Heche: Mwaka 2018.
Nassoro Katuga: Unakumbuka mwaka 2018 masuala ya siasa yalikuwa yamefungwa?
Heche: Mimi nilikuwa Mbunge.
Nassoro Katuga: Ni ushahidi wako hapa kwamba Magufuli alizuia mikutano ya kisiasa?
Heche: Mikutano siyo siasa.
Nassoro Katuga: Umewaambia Waheshimiwa Majaji kuwa huyu polisi aliyemuua mdogo wako alikukusudia kukutishia kufanya aina gani ya siasa?
Heche: Sikueleza aina.
Nassoro Katuga: Ila ni imani yako?
Heche: Sahihi.
Nassoro Katuga: Wewe ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA?
Heche: Ni sahihi.
Nassoro Katuga: Ukiwa Makamu Mwenyekiti, ulihudhuria Kamati Kuu ya tarehe 29 Agosti 2026?
Heche: Sikumbuki mpaka nipitie.
Nassoro Katuga: Unawaambia Waheshimiwa Majaji kwamba unakumbuka vitu vya mwaka 2015, lakini cha tarehe 29 Agosti hukumbuki?
Heche: Sikumbuki.
Nassoro Katuga: Sasa Naibu Katibu Mkuu alituambia kuhusu Kamati Kuu ya tarehe 29 Agosti 2026 kwamba mlizungumzia “Tonetone” zinazoonekana.
Heche: Muulize yeye.
Nassoro Katuga: Waeleze Waheshimiwa Majaji, unakumbuka kikao chochote ambacho Golugwa alisema mpaka sasa mmekusanya milioni 302?
Heche: Taarifa ya fedha huwa inaletwa Kamati Kuu.
Nassoro Katuga: Kwa wakati wowote umewahi kuletewa taarifa ya fedha kwamba kuna milioni 302?
Heche: Kamati Kuu imeletewa.
Nassoro Katuga: Ni lini ambapo Kamati Kuu ilikaa na kuletwa taarifa hiyo ya fedha?
Heche: Sikumbuki.
Nassoro Katuga: Unakumbuka au hukumbuki kuwa siku hiyo hiyo ndiyo mlizungumzia kuhusu kesi hii?
Heche: Siyo kweli.
Nassoro Katuga: Kwa hiyo, taarifa ya Naibu Katibu Mkuu kuwa Kamati Kuu imekaa na kuazimia viongozi waelekeze nguvu zao katika kumtetea Mwenyekiti...
Lissu: Shahidi, usijibu swali. Jibu maswali ya watu.
Heche: Si kweli.
Nassoro Katuga: Kwa hiyo taarifa ya Naibu Katibu Mkuu kuwa Kamati Kuu imekaa na kuazimia viongozi waelekeze nguvu zao katika kumtetea Mwenyekiti, ni taarifa sahihi au siyo sahihi?
Heche: Siikumbuki hiyo taarifa.
Nassoro Katuga: Nilikusikia ukiwaambia Waheshimiwa Majaji Bwana Ezekiah Wenje alinusurika kuuawa, akakimbilia Kenya.
Heche: Kweli.
Nassoro Katuga: Ulikuwepo?
Heche: Sikuwepo alikimbia.
Nassoro Katuga: Kwa hiyo huu ushahidi ni wa Wenje?
Heche: Kweli alikimbia.
Nassoro Katuga: Uliiambia Mahakama alinusurika kuuawa na nini?
Heche: Sikueleza muulize yeye.
Nassoro Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema mzalendo ni mtu anayependa nchi yake?
Heche: Sahihi.
Nassoro Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema mzalendo si mtu anayehimiza kuharibu nchi yake?
Heche: Sahihi.
Nassoro Katuga: Nitakuwa sahihi kusema mzalendo ni mtu anayehimiza ujenzi wa taifa lake?
Heche: Wapo wanaohimiza, lakini si wazalendo.
Nassoro Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema mtu mzalendo, pamoja na uzalendo wake, atahamasisha familia yake kujenga nchi yake?
Heche: Siyo lazima.
Nassoro Katuga: Unajua au hujui Tanzania hatuna uraia pacha?
Heche: Najua.
Nassoro Katuga: Unajua au hujui kuwa Mwenyekiti unayemuita mzalendo, familia yake (watoto wake), Mwenyekiti si raia wa Tanzania?
Heche: Hilo sijui.
Nassoro Katuga: Unajua au hujui mke wa Mwenyekiti unayemuita mzalendo siyo raia wa Tanzania?
Heche: Hilo sijui nachojua ni Mkurya.
Nassoro Katuga: Ni kweli au si kweli uliiambia Mahakama kwamba Sinda Geteba alikuwa mgombea wa Udiwani CCM, kwamba alichukuliwa na RCO mpaka leo haonekani?
Heche: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Ni ushahidi wako?
Heche: Niliambiwa na mdogo wake.
Nassoro Katuga: Ukasema na Tall pia?
Heche: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Uliiambia Mahakama amechukuliwa na nani?
Heche: Sikuiambia.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.