Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 10

Nassoro Katuga: Shahidi, tuhame kidogo huko.

Je, unajua ama hujui Tanzania ni nchi huru?

Heche: Najua.

Nassoro Katuga: Unajua ama hujui, kwa kuwa Tanzania ni nchi huru, kwa Katiba ya 1977 (uliyokuwa unairefer), Ibara ya 107(A), kwamba Mahakama ndiyo chombo chenye kutoa haki?

Heche: Mahakama za ndani na za kimataifa.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, kwa mujibu wa Ibara ya 107(A) ya Katiba, Mahakama ndiyo itakuwa inatoa haki kwenye mgogoro wowote.

Heche: Naelewa.

Nassoro Katuga: Unajua ama hujui kwa mujibu wa Katiba, inapotoa hizo haki, kwamba haitakiwi kuingiliwa?

Heche: Najua.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, kuwa Mahakama hii ya Jopo la Majaji watatu unaiamini au huiamini kuhusu kesi hii ya uhaini?

Heche: Hii kesi haijaamuliwa, siwezi kusema.

Nassoro Katuga: Unaiamini hii Mahakama au huiamini?

Heche: Naamini.

Nassoro Katuga: Sasa hebu waambie Waheshimiwa Majaji, kwenye kesi kati ya Mahakama na raia, nani anaangalia demeanor ya shahidi?

Heche: Ni Majaji.

Nassoro Katuga: Ni sahihi au siyo sahihi kwa shahidi kupima demeanor ya Waheshimiwa Majaji?

Heche: Sijui.

MASUALA YA USHAHIDI NA MASOMO YA SHERIA

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, unajua au hujui unafika kutoa ushahidi baada ya Mheshimiwa Lissu kuonekana ana kesi ya kujibu?

Heche: Najua.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, unajua au hujui ushahidi wa kielektroniki ni sawa na ushahidi wa nyaraka?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Unasoma Sheria, mwaka wa kwanza, Open University, mwaka wa kwanza?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Ya mkoa gani?

Heche: Mkoa wa Mara.

Nassoro Katuga: Umesoma kwa miezi mingapi?

Heche: Miezi 6, ila sisomi sasa hivi, nimesitisha.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.

Hatuweki Emoji
tumegomea!!!
 
Unajua mpaka saivi hawa mawakili wa serikali nawaona wajinga Sana vile vifo siku ya uchaguzi wao wanaona ni kawaida eeh mbona hajawajibishwa mtu yeyote kuhusu vile vifo au ndio Lissu ndio kauwa Watanzania siku ya uchaguzi na alikua gerezani😂😂
 
Issues ya Salman hata km kawekewa pesa je km ni kwa biashara zao binafsi nje ya masuala ya chama? Huyu bichwa cabbage mbona anauliza maswali ya kiwaki, tena nje ya case ya msingi? Huo ndio uhaini?
Heche mwenyewe keshasema hamfahamu huyo Salman. Angalau ht angesema huwa anawasiliana nae tu kwa mtandao kibiashara
 
Yaani maswali ya katuga anauliza kuhusu maisha binafsi hao wabunge wameingia juzi tuh apa bungeni wengine Wana magari ma 3 tayari yaani unaona kabisa ni ujinga mtupu
 
Inshu ni moja tu uyo Tundu Lissu kafanya fanya vipo uhaini pekeyake sisi tunataka kujua unawezaje mtu mmoja kufanya uhaini pekeyake Nchi nzima
Ivi Mimi najiuliza Kati ya kesi ya mauaji ya raia na kesi ya uhaini ipi ina uzito,mbona hawafikilii kuhusu aliyetoa order ya kuua raia wakati WA uchaguzi, Natamani Sana IGP Wambura na CDF mkunda watakapofika mahakamani
 
Hivi unajua Kwenda bank na kuomba miamala ya mtu Fulani inahitaji kibali na Sababu Maalum...Tena na mwenye account ajulishwe ..mara nyingi wanaofanya hivi ni Polisi kitengo Cha fedha haramu na sio Mawakili wa Serikali l

Ina maana Mawakili wa Serikali wanajua Salio za account zake zote Heche...
Akienda kulalamika CRDB... Na kufungua kesi ...hii ni suala lingine la hatari

Kuhusu magari...akiulizwa kwenye re examination na Lissu... Akisema magari mawili niliuza na mmiliki hajabadili umiliki ?

Toka kesi imeanza mwaka Jana bado Uhaini na viini vyake havijaanza...tuendelee kusubiri
Kwenye hili nimeshangaa mpaka hii Serikali inafanya mambo mengi ya ovyo kwa style inatuthibitishia taarifa za Polepole zilitolewa na hao hao Serikali na ndio wanafanya utekaji
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 11

Nassoro Katuga: Unajua au hujui hotuba zako mbalimbali/nyingi zipo mitandaoni?

Heche: Najua.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa kama uliwahi kuongelea kesi hii kuhusu Mshtakiwa kuonekana ana kesi ya kujibu.

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba katika hotuba hiyo ulisema hata ukiangalia demeanor ya Jaji wakati anasoma hukumu, hayupo sawa.

Heche: Sikumbuki.

Nassoro Katuga: Unajua kwamba Mahakamani unaruhusiwa kujikumbusha?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Unajua kwamba unaweza kuonyeshwa video, ujisikilize, halafu nikuulize maswali?

Heche: Sina uhakika nayo. Naamini unaweza kuchakachua au AI.

Nassoro Katuga: Sasa naiomba Mahakama nikuonyeshe video yake kama ushahidi wa nyaraka tuliokuonyesha.

(Wameanza ku-pray.)

Lissu: Waheshimiwa Majaji, huu ni utaratibu gani? Sijauelewa.

Jaji Ndunguru: Jirejeshe kwenye utaratibu wa cross-examination.

(Lissu anakaa.)

Nassoro Katuga: Wewe Shahidi, sikiliza kwanza.

(Wana-pray.)

(Maneno yanasikika.)

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa, kama wewe ni Shahidi wa kweli, hii hotuba unaikumbuka au huikumbuki?

Heche: Sauti imetengenezwa, ni kama ya kwangu.

Nassoro Katuga: Hii hotuba unaikumbuka au huikumbuki?

Heche: Siikumbuki.

Nassoro Katuga: Ulisema kwamba Shahidi wa 17 ndiye alipublish?

Heche: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Hayo uliyoyasema wewe katika hiyo video yapo au hayapo?

Heche: Hiyo video siyo ya kwangu.

Nassoro Katuga: Walau jibu kidogo. Hayo maneno kwamba P17 ndiye aliyepublish yanafanana au hayafanani na yale uliyosema?

Heche: Nimesikia yanafanana.

Nassoro Katuga: Kama nimekuelewa, Shahidi, tusaidie kwa uelewa wako, ku-establish prima facie case na kuthibitisha kesi, nini tofauti yake?

Heche: Sijui.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.

Leo Heche wamemkamata.

Katuga kashamlegeza hapo sijui kama Heche anaujanja tena.

Ukishamtoa mtu uaminifu, na kumfichua mafichoni kwa kumvua nguo. Kinachofuata ni kujipigia.
 
Sasa kama katuga kapray video mahakamani kwanini hiyo video ya Lissu isipelekwe apo mahakamani Kila mtu aone na asikie Lissu aliongea mambo gani siku hiyo
Anza kusoma upya kesi tokea mwanzo ndo utaelewa na kujua ni nini jamaa anajaribu kufanya/jenga kupitia huyu shaidi
 
Back
Top Bottom