Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
- Thread starter
- #141
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI
SEHEMU YA 12.
Nassoro Katuga: Wewe kama wewe, uliridhika au hukuridhika na uamuzi wa Lissu kuwa na kesi ya kujibu?
Heche: Mimi sikuridhika.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ukiwahi, uliwahi kuzungumzia ushahidi wa Prosecution kuhusiana na hii kesi?
Heche: Sijawahi kuzungumzia mwenendo wa kesi.
Nassoro Katuga: Tukikuonyesha tena, utaiita AI au utaikubali?
Heche: Kama siyo yangu, nitaikataa.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa, Lissu ana chombo cha habari?
Heche: Hana.
Nassoro Katuga: Yule pale Tundu Lissu akitaka kutoa ujumbe wake kwa hadhara, anatoaje?
Heche: Kwa mikutano ya hadhara.
Nassoro Katuga: Sikiliza swali vizuri.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa, that's nonsense. Shahidi ameshajibu, kwa mikutano ya hadhara.
Nassoro Katuga: Kuna siku Lissu amewaita Watanzania wote sehemu moja?
Heche: Hajawahi.
Nassoro Katuga: Ni kweli ama si kweli, Bwana Lissu akitaka kuongea na Watanzania anaongea na Waandishi wa Habari?
Heche: Si kweli.
Nassoro Katuga: Ni kweli kwamba Lissu mwenyewe katika ushahidi wake kwamba alizungumza na Waandishi wa Habari ili umma umsikie ni wa uongo?
Heche: Si kweli.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba ushahidi mbili hizi zinafanana, kwamba Lissu anasema akitaka deliver message anaongea na Waandishi wa Habari na wewe kusema si kweli. Zinafanana au hazifanani?
Heche: Sijui.
Nassoro Katuga: Shahidi, nilikusikia unasema Polisi walikuwa wanaingiza kura feki katika vibegi vyao?
Heche: Sahihi.
Nassoro Katuga: Uliwahi kumuona askari anaingia na kura feki? Ukamkamata?
Heche: Sikumkamata, ila niliwahi kumuona katika Shule ya Msingi Nyanungu akiingiza kura feki.
Nassoro Katuga: Ni sahihi kwamba ulimtaja huyo askari wa Shule ya Msingi Nyanungu?
Heche: Sikumtaja.
Nassoro Katuga: Unafahamu kuwa kwa Tanzania hii kuna mauaji ya vyanzo mbalimbali, kama vile mivu, mapenzi, biashara?
Heche: Najua.
Nassoro Katuga: Na unajua masuala ya mauaji siyo ya uchaguzi, ni jinai?
Heche: Najua.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.