Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

Yaani mfano Mimi niende bank flani.. niombe miamala Yako...
Kwanza watashangaa... Huyu mtu vipi ..unawezaje kuja kuomba miamala ya mtu mwingine?

Mimi ni wakili... Sawa unakibali Cha Mahakama ?
Na kibali lazima kiseme Sababu... Huyu anafanya labda biashara haramu.. au anatakatisha pesa...

Lakini kumbuka wakili haruhusiwi kufanya uchunguzi Bali ni Polisi ...

Kwa hiyo Hawa jamaa ..Mawakili wa Serikali wanabebwa na mfumo
Ok hapo nimekuelewa.
 
Hivi unajua Kwenda bank na kuomba miamala ya mtu Fulani inahitaji kibali na Sababu Maalum...Tena na mwenye account ajulishwe ..mara nyingi wanaofanya hivi ni Polisi kitengo Cha fedha haramu na sio Mawakili wa Serikali l

Ina maana Mawakili wa Serikali wanajua Salio za account zake zote Heche...
Akienda kulalamika CRDB... Na kufungua kesi ...hii ni suala lingine la hatari

Kuhusu magari...akiulizwa kwenye re examination na Lissu... Akisema magari mawili niliuza na mmiliki hajabadili umiliki ?

Toka kesi imeanza mwaka Jana bado Uhaini na viini vyake havijaanza...tuendelee kusubiri
Hayo ya kuishtaki CRDB yatafata. Issue ni kwamba amekana kumfahamu Salman lkn anakiri aliwekewa mzigo na huyo huyo
 
Watu wanasubiri

1789378301996.png
 
Swali la Msingi kwa wenye
Akili
Kama Mwenyekiti mh Lissu yeye mwenyewe kajua
Kuongea yale Maneno ni kosa Kisheria na nitashtakiwa kwa kesi ya Uhaini

SWALI Kwanini mh Lissu kafanya yale
MAKOSA ‼️‼️

nini kusudio lake na hatma ya chama chenyewe cha
CHADEMA ‼️‼️

CHADEMA kitabaki salama mbele ya Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ❓️❓️❓️

Nini faida ya yote aya kafanya ❓️❓️
 
Hayo ya kuishtaki CRDB yatafata. Issue ni kwamba amekana kumfahamu Salman lkn anakiri aliwekewa mzigo na huyo huyo
Sawa.... Huoni hii kesi ni kama kata funua..

Yaani kesi ni Uhaini lakini kinachoendelea ni Tone tone...
Mimi ni mkulima...
Aliyeuwawa mwaka flani ulikuwepo ?

Hapa tusubiri.. Heche iyambie Mahakama una nyumba ngapi ?

Kesi itaendelea... Tuambie vikao vya CHADEMA vina wajumbe wangapi ..
 
Huyo Katuga naona anatafuta kumpotezea credibility heche mbele ya wafuasi wa chadema, kuhusu hizo gari wala sio ajabu mtu kakaa ubunge miaka 5 ndio ashindwe kuwa na hizo gari na tractor?

Issues ya Salman hata km kawekewa pesa je km ni kwa biashara zao binafsi nje ya masuala ya chama? Huyu bichwa cabbage mbona anauliza maswali ya kiwaki, tena nje ya case ya msingi? Huo ndio uhaini?
 
Huyo Katuga naona anatafuta kumpotezea credibility heche mbele ya wafuasi wa chadema, kuhusu hizo gari wala sio ajabu mtu kakaa ubunge miaka 5 ndio ashindwe kuwa na hizo gari na tractor?

Issues ya Salman hata km kawekewa pesa je km ni kwa biashara zao binafsi nje ya masuala ya chama? Huyu bichwa cabbage mbona anauliza maswali ya kiwaki, tena nje ya case ya msingi? Huo ndio uhaini?
Re examination atasawazisha tu
Ni kawaida sana hayo maswali
 
Kuna kitu hakiko sawa hasa kwemye mtazamo wetu juu ya viongozi wa upinzani.

Yes, ni kweli sio wote ni waaminifu, na kweli wengine wanatumika na dola, lakini haimaanishi ukiwa mpinzani, usifanye biashara au usiwe na deals na watu tofauti tofauti. Cha muhimu, je hizo deals ni CLEAN?.

Heche amekuwa diwani na mbunge kwa miaka mingi, hivi kwa level yake Milioni 20 kweli ni hela ya kuanza kuishangaa?

Upinzani sio umasikini.
 
Kwamba wanafata mpaka account zako za bank watu wanaokuingizia pesa!!
Looh.

Ndio kwanza Asubuhi leo Mh Lissu wawepo watu wa kuzuia
kudondoka kwake kama Mzee Warioba ‼️

mana Heche leo wanamwanika kila kitu❗️
kinawekwa wazi kwa Mahakama na kwake
mh Lissu 🤔
Leo Heche
hakunji Uso tena kakutana na wahuni
zaidi yake✍️
 
Kwamba kwa huyo wakili wa Serikali anaona wazi kwamba; kusoma ripoti kwa kiingereza ni jambo linahitaji umahiri katika lugha husika! 😊
Tafsiri yake ni kwamba anajaribu kuieleza mahakama kwamba shahidi (Heche) sio mahiri wa lugha ya kiingereza kusoma na kuelewa ripoti alizoeleza kuzijua mahakamani. 😊

Anajaribu ku "establish" kwamba kwa kuwa ripoti za tume hizo ni za kiingereza: basi zingehitaji mtu kuwa mahiri wa lugha ya kiingereza kuzisoma na kuzielewa. Ni sawa na kusema kusoma habari/makala/ripoti kutoka katika gazeti la kiingereza na kuelewa kunahitaji msomaji awe "mahiri wa lugha" husika.
Vetting ya mtu kuwa wakili mkuu/mwandamizi wa serikali itakuwa ya hovyo sana bila shaka.
Ulishawahi kuhojiwa maswali na mtoto? Huwa unamjibu tu for the sake of it, halafu rohoni unamuombea akili yake ikue na ikomae ili hayo maswali awe anajijibu mwenyewe kichwani.

😅😅
 
MACHADEMA kwasasa nq Wafuasi wao yanafundishana kusema Uwongo tu

Sasa Heche kusema Uwongo wanamsifia🫎🫎🫎😂

Chama cha Wahuni Wahuni kabisa
Ndio wanataka tuwaamini kuwapa Nchi waendeshe wao🫎🫎🫎🫎🫎🫎🫎

Mwacheni Mungu haitwe Mungu wanaumbuka mbele yetu mchana kweupe

MAKAMU MWENYEKITI MUONGO KIASI ICHI CHINI YA KIAPO 😂😂😂 MWENYEKITI MWENYEWE NAYEYE MUONGO
CHINI YA KIAPO🤠🤠

CHADEMA KWISHAAA
Nenda katoe ushahidi wewe ***** mahakamani.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 10

Nassoro Katuga: Shahidi, tuhame kidogo huko.

Je, unajua ama hujui Tanzania ni nchi huru?

Heche: Najua.

Nassoro Katuga: Unajua ama hujui, kwa kuwa Tanzania ni nchi huru, kwa Katiba ya 1977 (uliyokuwa unairefer), Ibara ya 107(A), kwamba Mahakama ndiyo chombo chenye kutoa haki?

Heche: Mahakama za ndani na za kimataifa.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, kwa mujibu wa Ibara ya 107(A) ya Katiba, Mahakama ndiyo itakuwa inatoa haki kwenye mgogoro wowote.

Heche: Naelewa.

Nassoro Katuga: Unajua ama hujui kwa mujibu wa Katiba, inapotoa hizo haki, kwamba haitakiwi kuingiliwa?

Heche: Najua.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, kuwa Mahakama hii ya Jopo la Majaji watatu unaiamini au huiamini kuhusu kesi hii ya uhaini?

Heche: Hii kesi haijaamuliwa, siwezi kusema.

Nassoro Katuga: Unaiamini hii Mahakama au huiamini?

Heche: Naamini.

Nassoro Katuga: Sasa hebu waambie Waheshimiwa Majaji, kwenye kesi kati ya Mahakama na raia, nani anaangalia demeanor ya shahidi?

Heche: Ni Majaji.

Nassoro Katuga: Ni sahihi au siyo sahihi kwa shahidi kupima demeanor ya Waheshimiwa Majaji?

Heche: Sijui.

MASUALA YA USHAHIDI NA MASOMO YA SHERIA

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, unajua au hujui unafika kutoa ushahidi baada ya Mheshimiwa Lissu kuonekana ana kesi ya kujibu?

Heche: Najua.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, unajua au hujui ushahidi wa kielektroniki ni sawa na ushahidi wa nyaraka?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Unasoma Sheria, mwaka wa kwanza, Open University, mwaka wa kwanza?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Ya mkoa gani?

Heche: Mkoa wa Mara.

Nassoro Katuga: Umesoma kwa miezi mingapi?

Heche: Miezi 6, ila sisomi sasa hivi, nimesitisha.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 11

Nassoro Katuga: Unajua au hujui hotuba zako mbalimbali/nyingi zipo mitandaoni?

Heche: Najua.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa kama uliwahi kuongelea kesi hii kuhusu Mshtakiwa kuonekana ana kesi ya kujibu.

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba katika hotuba hiyo ulisema hata ukiangalia demeanor ya Jaji wakati anasoma hukumu, hayupo sawa.

Heche: Sikumbuki.

Nassoro Katuga: Unajua kwamba Mahakamani unaruhusiwa kujikumbusha?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Unajua kwamba unaweza kuonyeshwa video, ujisikilize, halafu nikuulize maswali?

Heche: Sina uhakika nayo. Naamini unaweza kuchakachua au AI.

Nassoro Katuga: Sasa naiomba Mahakama nikuonyeshe video yake kama ushahidi wa nyaraka tuliokuonyesha.

(Wameanza ku-pray.)

Lissu: Waheshimiwa Majaji, huu ni utaratibu gani? Sijauelewa.

Jaji Ndunguru: Jirejeshe kwenye utaratibu wa cross-examination.

(Lissu anakaa.)

Nassoro Katuga: Wewe Shahidi, sikiliza kwanza.

(Wana-pray.)

(Maneno yanasikika.)

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa, kama wewe ni Shahidi wa kweli, hii hotuba unaikumbuka au huikumbuki?

Heche: Sauti imetengenezwa, ni kama ya kwangu.

Nassoro Katuga: Hii hotuba unaikumbuka au huikumbuki?

Heche: Siikumbuki.

Nassoro Katuga: Ulisema kwamba Shahidi wa 17 ndiye alipublish?

Heche: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Hayo uliyoyasema wewe katika hiyo video yapo au hayapo?

Heche: Hiyo video siyo ya kwangu.

Nassoro Katuga: Walau jibu kidogo. Hayo maneno kwamba P17 ndiye aliyepublish yanafanana au hayafanani na yale uliyosema?

Heche: Nimesikia yanafanana.

Nassoro Katuga: Kama nimekuelewa, Shahidi, tusaidie kwa uelewa wako, ku-establish prima facie case na kuthibitisha kesi, nini tofauti yake?

Heche: Sijui.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Back
Top Bottom