Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
- Thread starter
- #301
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI
SEHEMU YA 19.
KUHOJIWA NA NASSORO KATUGA
Nassoro Katuga: Ulijua au hukujua kuwa kilichofanya wamchukue Bwana Tall ni kwa sababu ni mwanachama wa CHADEMA?
Heche: Ni kweli.
Nassoro Katuga: Unasema aliyemchukua humjui?
Heche: Ni kweli.
Nassoro Katuga: Baadaye ulieleza kuwa ulikamatwa hapa nje?
Heche: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Ukashtakiwa kwa kuvuka mpaka?
Heche: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, ni kweli ulienda Kenya au hukwenda?
Heche: Sikuvuka.
Nassoro Katuga: Ni kweli ulitaka kwenda au hukutaka?
Heche: Nilitaka kwenda.
Nassoro Katuga: Ulieleza katika ushahidi wako kwa nini ulizuiliwa?
Heche: Sikueleza.
Nassoro Katuga: Ni kweli ulisema ulipelekwa hadi Dodoma, ukalazwa Mtumba peke yako?
Heche: Sahihi.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, ulitaka uwekwe selo na nani?
Heche: Sikutaka kuwekwa na mtu.
Nassoro Katuga: Unaogopa kulala peke yako na wewe mwanaume?
Heche: Hapana.
Nassoro Katuga: Hivi shahidi, katika kukamatwa kwako huko unapotuambia, uliwahi kuchukuliwa passport yako?
Heche: Ilichukuliwa.
Nassoro Katuga: Ilichukuliwa lini?
Heche: Nafikiri tarehe 18 Oktoba 2025.
Nassoro Katuga: Ilirudi vipi kwako?
Heche: Chama kiliandika barua kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, nikarudishiwa kwa mtu anayeitwa Kamishna wa Mipaka Jirani.
Nassoro Katuga: Unajua kuwa Ofisi ya DPP kupitia National Service Act ina jukumu la kuratibu kupeleka kesi za jinai?
Heche: Sijui.
Nassoro Katuga: Ni kosa gani kukuta Mawakili wa Serikali kituo cha polisi?
Heche: Sijui.
Nassoro Katuga: Katika ushahidi wako kuna sehemu yoyote ukisema hawa akina Katuga walideal na mimi?
Heche: Sikujua.
Nassoro Katuga: Unajua au hujui kuwa kesi ya jinai haina limit kwamba baada ya miaka mitano unaweza kushtakiwa?
Heche: Sijui.
Nassoro Katuga: Uliulizwa kuhusu kesi ya Oktoba 29, hukuwahi kushtakiwa. Na kuhusu hiyo ya ugaidi ukasema hujawahi kushtakiwa, ni kutisha-tisha tu?
Heche: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Unajua ama hujui kuwa Mawakili uliowaona pale walikuwa wanacoordinate kesi za tarehe 29 Oktoba?
Heche: Sijui.
Nassoro Katuga: Unajua au hujui kama washtakiwa tuliowahoji pale walikutaja wewe kuwatuma Oktoba 29?
Heche: Sijui.
Nassoro Katuga: Unajua ama hujui ushahidi uliokusanywa kwenye hayo mafaili unaeleza mlikaa vikao na jinsi mlivyopanga kuratibu matukio ya tarehe 29 Oktoba?
Heche: Sijui.
Nassoro Katuga: Ni ushahidi wako kwamba ulipohojiwa kuhusu ugaidi ulikataa?
Heche: Nilikataa, maana sikutoa maelezo
Nassoro Katuga: Ulitoa maelezo Polisi au ulikataa?
Heche: Nilikataa ndiyo.
Nassoro Katuga: Sasa shahidi, unasema ulisikiliza hotuba ya Jaji Chande. Je, kwenye hotuba hiyo ulisikia kauli ya kuwa Oktoba 29 ni matukio yaliyopangwa?
Heche: Nilisikia.
Nassoro Katuga: Je, ushahidi mbili za wakati wa coordination kupitia ushahidi wa watuhumiwa kuwa wewe ulihusika katika kupanga na kuratibu, na hotuba ya Chande kwamba matukio yalipangwa, vinafanana au havifanani?
Heche: Kwa hiyo mimi ni mshitakiwa?
Lissu: Jibu swali kaka.

Nassoro Katuga: Shahidi, nilikusikia ukisema hujui au huna kumbukumbu ya viongozi wengine wa CHADEMA kama waliwahi kushtakiwa?
Heche: Ndiyo nilisema.
Nassoro Katuga: Unamfahamu Zitto Zuber Kabwe?
Heche: Namfahamu.
Nassoro Katuga: Unajua kuwa Zitto Zuber Kabwe alishtakiwa kwa kuchapisha taarifa za mauaji ya Kigoma? Alishtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam inayoketi Kisutu na hakukutwa na hatia.
Heche: Sijui. Nilikuwa naongelea viongozi wa CCM.
Nassoro Katuga: Unamfahamu Daniel Yona?
Heche: Simjui.
Nassoro Katuga: Unamfahamu Basil Pesa Mbili Mramba?
Heche: Simfahamu.
Nassoro Katuga: Na bado unajiona wewe ni shahidi?
Heche: Ndiyo.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.