Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 8

Nassoro Katuga: Kama nimekusikia na nikakuelewa, hapa Mahakamani umetaja majina mengi na watu wengi sana.

Uki-relate watu hao kupotea na mambo ya uchaguzi?

Heche: Nakumbuka.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, kwa nature ya ushahidi wako kwamba haya yanatokea sababu ya uchaguzi, je, umewahi kusema namna gani watu wanapotea kwa mapungufu yapi ya sheria ya uchaguzi?

Heche: Sikusema.

Nassoro Katuga: Umewahi kuona familia zinamtafuta mtu wao?

Heche: Nimeona.

Nassoro Katuga: Kila ambaye haonekani ametekwa? Kila ambaye ametoweka ametekwa?

Heche: Familia gani?

Nassoro Katuga: Siyo lazima yako kuniuliza swali.

Nassoro Katuga: Ni nani katika familia aliyekwambia Bwana Simon katoweka?

Heche: Mke wake.

Nassoro Katuga: Mke wake anaitwa nani?

Heche: Siku nyingi, nimemsahau.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba ushahidi wa Simon kutekwa siyo wako, ni wa mke wake.

Heche: Sahihi.

Nassoro Katuga: Nimeusema hapa Mahakamani kwa kuambiwa?

Heche: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama unafahamu kwamba ushahidi wa kuambiwa hautakiwi Mahakamani.

Heche: Sahihi.

Nassoro Katuga: Unajua au hujui hata ushahidi wanaousoma kwenye vyombo vya habari ni ushahidi wa kuambiwa?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Unajua ama hujui ushahidi wako wa msingi lazima uendane na hoja iliyopo Mahakamani?

Heche: Najua.

SUALA LA MZEE SASI

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama katika ushahidi wako ulisema Mzee Sasi baada ya kutoka gerezani alijiunga na Chama chetu, CHADEMA.

Kama suala la Mzee Sasi kutoka gerezani na kuchaguliwa kuwa Diwani lina-relate vipi na kesi?

Heche: Sikueleza.

Nassoro Katuga: Unajua ama hujui unaporejea shauri lolote halihusiki kuthibitishwa, lakini Mahakama ina-take judicial notice?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ulitaja namba za kesi za Mzee Sasi na wenzake.

Heche: Sikuzitaja.

JEZI YA ARSENAL

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, ni nani au rafiki gani wa Chama aliyekupa jezi ya Arsenal original yenye jina la Heche?

Heche: Nimenunua mwenyewe.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, hiyo jezi umenunua lini na wapi?

Heche: Ya mwaka gani?

Nassoro Katuga: Uliyonunua kwa Pound 500?

Heche: Tuone.

Nassoro Katuga: Hii hapa, unaweza kuona.

Heche: Waheshimiwa, tupo wengi.

SUALA LA SALMAN NA AKAUNTI

Nassoro Katuga: Unajua mtu anaitwa Salman?

Heche: Simfahamu mtu anaitwa Salman.

Nassoro Katuga: Baada ya Salman kukuchangia pesa, ulipeleka wapi?

Heche: Simfahamu Salman.

Nassoro Katuga: Ni kweli hizi namba za akaunti za CRDB 015222005XXX ni za kwako?

Heche: Ni za kwangu.

Nassoro Katuga: Ni kweli, kwa mujibu wa risiti hii, huyo Salman ameweka milioni 20 katika akaunti yako?

Heche: Ni kweli.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.

..Benki / CRDB wana ruhusa ya kutoa taarifa za akauti ya John Heche bila kuwepo shauri mahakamani na kupata ruhusa ya Jaji?
 
Mimi sio kiongozi wa Chadema, i think tunafanana tu, wote tunaishia kelele zetu humu humu.

Nachotaka atoe taarifa public ni kwasababu, Chadema kinaitwa chana cha watanzania.

Hata michango wanayopokea inatoka kwao, sasa kuna ubaya gani kiongozi wao akijitokeza mbele yao akajibu yale anayotuhumiwa nayo?

Tena kama ikitokea akajibu wazi kwa public, naamini hapa ndio atakuwa amekata mzizi wa fitna, watu tayari tutakuwa na majibu yetu, sio rahisi kuja kuvurugwa tena mbele ya safari.

Lakini madhara ya kujibia kwenye vikao, ikitokea upande mmoja haujaridhika, basi naamini hizi kelele zitaibuka tena mbele ya safari, hivyo mwaka wote huu tuwe tunaishi kwa malalamiko yao tu.
Kwahiyo unataka kiongozi aite press conference kujibu kila tuhuma?

Tuhuma za tone tone zilijibiwa na mnyika, kwasasa Tuhuma gani za msingi ambazo anatakiwa kuzijibu Heche?

Kwa mazingira ya siasa za sasa dhidi ya Heche, chama kisipokuwa na msimamo kila siku kitakuwa kinaita press kujibu tuhuma zilizoanzishwa na waliotorokea Chauma, timu abduli na CCM yote.

Target hapa ni Heche, let’s not pretend we do not see. Btw maswali ya Katuga kwa Heche yote ameyajibu, mtu aniambie kama kuna swali halijajibiwa.
 
Unayajua maisha wanayoishi waliowahi kuwa Wabunge wa Chadema Mh. Ainess Kiwia (Ilemela) na Machemlo (Ukerewe)? Kawauliza kama wana hata baiskeli! Ahahahahaha!!
Mtu kushindwa kuzalisha kipato chake kizae faida sio kosa la Heche.

Hata hapo kwenye ualimu mnakolipwa laki 3 na nusu wengine wana pikipiki wengine hawana.

Hoja yako ni takataka weka humu 🚮 (Kwa sauti ya Mbaga Jr
 
Kwahiyo mfano
Nina magari 4
Mimi nikasema nina 2
Maanake nimesema uongo si ndio!
Kwahiyo nitaonekana shahidi muongo au?

..sio jambo zuri kwa shahidi.

..hapo Heche ameharibu.

..lakini kusema uongo kuhusu mali zake, hakumaanishi kwamba ni muongo kwa kila jambo aliloieleza mahakama.


..Na mambo mengi aliyoyasema Heche ni mambo yanayojulikana yeye ameyarudia tu mahakamani.

..kwamba Heche amedanganya kuhusu mali zake hakuondoi ukweli kuhusu ushahidi wake unaohusu mauaji kama ya Alphonce Mawazo, Azory Gwanda, ....
 
..sio jambo zuri kwa shahidi.

..hapo Heche ameharibu.

..lakini kusema uongo kuhusu mali zake, hakumaanishi kwamba ni muongo kwa kila jambo aliloieleza mahakama.


..Na mambo mengi aliyoyasema Heche ni mambo yanayojulikana yeye ameyarudia tu mahakamani.

..kwamba Heche amedanganya kuhusu mali zake hakuondoi ukweli kuhusu ushahidi wake unaohusu mauaji kama ya Alphonce Mawazo, Azory Gwanda, ....
Ok mkuu.
 
Ukiwa unajibu kila kitu utajibu mangapi?
Usijali, nawachagua wachache wanaoeleweka
Kwahiyo unataka kiongozi aite press conference kujibu tuhuma?

Tuhuma za tone tone zilijibiwa na mnyika, kwasasa Tuhuma gani za msingi ambazo anatakiwa kuzijibu Heche?

Kwa mazingira ya siasa za sasa dhidi ya Heche, chama kisipokuwa na msimamo kila siku kitakuwa kinaita press kujibu tuhuma zilizoanzishwa na waliotorokea Chauma, timu abduli na CCM yote.

Target hapa ni Heche, let’s not pretend we do not see. Btw maswali ya Katuga kwa Heche yote ameyajibu, mtu aniambie kama kuna swali halijajibiwa.
Tatizo ndio hili, kujigeuza msemaji wake.

Hapa suala sio kujibu kila siku, anatakiwa aje na majibu ya kujitosheleza ajibu biashara iishe, sio kumjibia kama hivi mnavyofanya yule ni kiongozi wa chama cha umma ana wajibu wa kufanya hivyo.

Haya mambo hayataki kupelekana kwa huruma huruma, hiyo huruma yako kwake inaweza kumuumiza mwingine, haya yaachwe yaende kwa uwazi kila mtu aone na ajue.

Na hata kama akitakiwa kurudi tena kurudi kwa public kutoa clarification ana wajibu wa kufanya hivyo mpaka hili jambo liishe.

Hakuna haja ya kumtetea, wakati akichukua form kugombea alijua wajibu wake kwa public, na sasa ndio wakati wake kutimiza wajibu wake.
 
Huyu anafanya hisani, wajibu wa kurusha hiyo kesi mubashara ni wa serekali, na serekali imeona aibu ikagoma kuirusha. Usimpangie mwanaume jinsi ya kuripoti wakati wenye wajibu wamegoma.
Umekuja mbio mbio ku quote comment yangu!! Umelimwa nini?
 
Mahakamani inatumika Logic na ushahidi usiyo acha shaka zaidi badala ya maneno ya kusikia au kuambiwa. Ndo maana kuna watu huwa wanamakosa lakini ushahidi huwa unashindwa kujitoleza.

Anachosema hapo jamaa ni kwamba Heche kwenye upande wa Logic keshawekwa kwenye kona. Na kila swali linaloulizwa lina umuhimu wake wewe usifikiri hayo maswali hayana maana hata kama yanaonekana ya kitoto.

Heche anaonesha hali halisi ya viongozi wa Chadema na wafuasi wao kwamba huwa wanafikiri kitu kikisemwa na Taasisi ya Kimataifa, au mtu maarufu au chombo cha habari maarufu basi wanaweza kukitumia bila kujiridhisha.

Wafuasi wa Chadema tumieni hii kesi kujifunza namna mahakama zinavyofanya na siyo kutumia mihemko na maneno ya kutiana moyo. Kuna mwanamke huko marekaji kesi yake imeshindwa kuamriwa pamoja na kwamba aliaua watoto wake watatu.

Wafuasi wa Chadema na Watanzania tutumie hizi kesi kujifunza. Itatusaidia kutofanya vitu kwa mihemko kwani mahakamani au kwenye kudai haki hakuna mihemko
Exactly 💯
 
Back
Top Bottom