Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Tunahitimisha mwaka 2024.. Kiuhalisia hakuna kinachobadilika zaidi ya tarakimu.. Maisha yetu yametawaliwa na tarakimu.. Na hizi ndio zinaendesha dunia ya kimwili na ya kiroho pia
Tarakimu hazina kinyume(rivasi).. Muda haurudi nyuma.. Hivyo basi siku hii ya huu mwaka haitakaa irudi tena maishani mwetu.. Hivyo ni vema tukaipa umuhimu mkubwa na wa kipekee
Tulianza salama huu mwaka pamoja na tukiwa na matarajio mengi.. Wenzetu baadhi hawakuweza kumaliza nasi.. Tuwaombee sana!
Kipekee kabisa naomba kuchukua nafasi hii kwa wale wote kwa njia moja ama nyingine waliumizwa na maandishi na maandiko yangu
Kuna wale ambao pia sikuweza kukidhi haja ya matarajio yao katika changamoto mbali mbali walizopitia mwaka huu..
Wengi tuliwasiliana PM na baadhi baadae kwenye mawasiliano ya simu lakini harakati na ubize wa maisha vikanifanya niwe na maahirisho mengi
Kikubwa ninachoweza kusema ni kwamba najali shida ya kila mmoja wenu na daima sikuacha kuwaombea kila nilipopata walau sekunde chache ama dakika chache za kufanya hivyo
Mimi ni binadamu nisiye mkamilifu, nina mapungufu yangu pia mengi tu.. Mniwie radhi kwa wale ambao tulikwazana hapa na pale.. Sina kinyongo wala sina kisasi kwa yeyote yule
Naumaliza mwaka 2024 nikiwa msafi wa roho na mwili na amani tele.. Nimeitafuta njia ya ukamilifu wa kiroho na wokovu wa ndani kwa utulivu na unyenyekevu mkubwa na matokeo yake mazuri nimeyaona
Kwa uzi huu niwatakie heri ya mwaka mpya 2025 masaa si mengi yajayo.. Na tukipewa kibali cha kiroho basi sote tuweze kuumaliza mwaka 2024 kwa amani na furaha na kuuingia mwaka 2025 kwa viwango vilevile
Nawaombea sana!