SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Yanga waliangalia ratiba ya ligi wakaona muda sahihi wa harusi ya Aziz Ki na Hamisa Mobetto ni huu ndiyo wakabariki hili zoezi zima linaloendelea.
Wachezaji wa Yanga wamekuwa kwenye pilikapilika za shughuli za hii harusi zaidi ya wiki moja sasa ila cha ajabu wakiingia uwanjani wao ndiyo wana dominate mchezo na kuondoka na goli 6. Tukumbuke pia ni juzi juzi tu hapa tuliambiwa fitness ya wachezaji iko chini!
Leo wanaenda kucheza na timu ambayo inaongoza kwa kusajili wachezaji wa kigeni, yaani imesajili wengi hadi wengine imebidi iwabadili uraia na wengine iwatoe kwa mkopo. Singida ni timu ambayo mwanzoni mwa msimu iliwekwa kama moja ya wanaowania ubingwa na mpaka sasa ipo katika mbio hizo na pia kuwania nafasi ya kushiriki kimataifa. Kwa hiyo katika makaratasi haitakiwi kuwa mechi ndogo.
Cha ajabu Yanga inaenda katika mchezo huu bila wasiwasi wa kukabiliana na upinzani wowote.
Tuache unafki. Haya mambo hayana faida kwa mpira wa Tanzania.
Za ndaaani, Bwana Fedha aliulizwa anatoa mchango gani kwa harusi, akakumbushia pesa ya usajili iliyombakisha Ki, akaahidi kibunda kingine kizito ila pia akaahidi pwenti 3 za leo.