Leo tunamaliza malumbano kuhusu upangaji wa matokeo katika ligi ya NBC

Leo tunamaliza malumbano kuhusu upangaji wa matokeo katika ligi ya NBC

Coastal katoa sare na Simba katika msimu mgumu kama huu na msimu wa juzi Namungo alitoa sare na Simba katika moja ya mechi za mwisho iliyomaliza ndoto ya Simba ya ubingwa.
Au sio na Tabora alifanyaje?
 
Kwaiyo kmc na yanga ni timu ipi Bora kuliko mwingine
Kwa hiyo Tabora na Yanga ni timu ipo bora kuliko mwingine?

Nimejibu hoja yako ya Coastal na Namungo umeikimbia.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Kwani alifanyaje?
Tabora tokea ipande aijawai kuifunga Simba ata goli la kubahatisha,,inapokaribia mechi na Simba wachezaji muhimu wanakuwa na matatizo,,mara vibali mara majeruhi but mechi ikiisha mambo yanakuwa sawa kwanini
 
Tabora ana misimu mingapi ligi kuu? KMC kabla ya mechi ya juzi ilikuwa haijaifunga uto hata goli la kuotea kwa mechi 8 mfululizo. Niambie hiyo ni misimu mingapi? Umeona nimesema lolote kuhusu hilo?
 
Tabora ana misimu mingapi ligi kuu? KMC kabla ya mechi ya juzi ilikuwa haijaifunga uto hata goli la kuotea kwa mechi 8 mfululizo. Niambie hiyo ni misimu mingapi? Umeona nimesema lolote kuhusu hilo?
Basi Kaa kimya akuna tutakachokusaidia hapa Msemaji wenu alinukuliwa akisema pale tff Kuna sanduku la maoni uyapeleke uko baada ya kolo kudhulumu point za Dodoma Jiji,,sasa na wewe elekea uko mapema!
 
Wachezaji wao kibao akiwemo yule duka Kennedy wanamiss. Hata aibu hawaoni. Ila waache wabebane, sisi tunapita nao wote na kimataifa tunaendelea kushaini. Siku wakija kushtuka upuuzi wanaofanya watakuwa wamechelewa saana.
Kimataifa unashaini na robo fainali ama una ziada?
 
Yanga waliangalia ratiba ya ligi wakaona muda sahihi wa harusi ya Aziz Ki na Hamisa Mobetto ni huu ndiyo wakabariki hili zoezi zima linaloendelea.

Wachezaji wa Yanga wamekuwa kwenye pilikapilika za shughuli za hii harusi zaidi ya wiki moja sasa ila cha ajabu wakiingia uwanjani wao ndiyo wana dominate mchezo na kuondoka na goli 6. Tukumbuke pia ni juzi juzi tu hapa tuliambiwa fitness ya wachezaji iko chini!

Leo wanaenda kucheza na timu ambayo inaongoza kwa kusajili wachezaji wa kigeni, yaani imesajili wengi hadi wengine imebidi iwabadili uraia na wengine iwatoe kwa mkopo. Singida ni timu ambayo mwanzoni mwa msimu iliwekwa kama moja ya wanaowania ubingwa na mpaka sasa ipo katika mbio hizo na pia kuwania nafasi ya kushiriki kimataifa. Kwa hiyo katika makaratasi haitakiwi kuwa mechi ndogo.

Cha ajabu Yanga inaenda katika mchezo huu bila wasiwasi wa kukabiliana na upinzani wowote.

Tuache unafki. Haya mambo hayana faida kwa mpira wa Tanzania.

Za ndaaani, Bwana Fedha aliulizwa anatoa mchango gani kwa harusi, akakumbushia pesa ya usajili iliyombakisha Ki, akaahidi kibunda kingine kizito ila pia akaahidi pwenti 3 za leo.
Siku hizi wachawi mnawanga mcha kweupeee bila hofu. Haya
 
Back
Top Bottom