Leo tuwakumbuke wanamuziki wa mamtoni waliotamba miaka ya nyuma

Mi nilikua siendagi Fiesta lakini ile Ja Rule nilitimba atleast nimuone mzee wa Unyamwezini. Sema nilivyofika pale na washkaji tukaanza kuzuzuka na mitungi na mademu Ja Rule mwenyewe anaperform tunamuona yuko mbaaali wala hatuna habari nae. Baadae akaanza kuimba New York New York wahuni wakaanza kuleta zengwe wanamwambia f*ck New York hapa tuko Dar
 

Sisqo Ngoja nipakue Unleash the dragon hiyo ngoma naipenda
 
Watatamba wote lakini nikisikia tu neno mamatoni namkumbuka mwamba mmoja wa kuitwa Curtis James Jackson Ila kama anavojulikana zaidi kama 50 Cent A K.A Ferrari

Picha Linaanza nikiweka we EATV enzi hizo tuinaiita Channel Five Ebana weee! Unakutana na kitu kinaitwa WANKSTAR
Dah hili Pini ni balaa aisee...

Hapo sijakumbuka IN DA CLUB, JUST A LIL BIT, CANDY SHOP [emoji91],21 QUESTIONS, I GET MONEY, WINDOW SHOPPER NA MANY MEN

Aisee 50 Cent alikua nyoqo Sana nyieeee...
Si T-shirt, suruali,viatu, mabegi Hadi chupi zilikua na chata ya 50
 
enzi hizo sony ericson, Mototrola L6 ndio simu zinazotamba mixer kuwa na infared kabla ya bluetooth🤣🤣
 
Kula chuma hicho Early 2000s
Your browser is not able to display this video.
 
Mimi nilipewa Ada nikaenda kujinunulia Taima pair moja. Sitaki masikhara kabisa. Yaani me univalishe vile viatu vyeusi visivyo na chata. Khaaaaaah [emoji23][emoji23][emoji23]

Taima ni kiboko ya enzi hizo na ukivaa we ndio mtu sasa.
 
Mafala wametulia sana hela wale. Me nilikuwa naenda kwa babu wa kihindi pale mitaa ya fire kariakoo. Mzee computers zake alikuwa amewekea zile partitions yaani jirani hawezi ona unatizama nini.

Kwahiyo nilikuwa nina computer yangu hiyo ipo kona kule hakuna mtu anaweza kuona ukikaa huko. Nikijichimbia kule natulia nakula zangu picha za namna gani vipi tu.

Yule mzee alikuwa anatuchora sana nikifikiria saa hii kama alikuwa anacheki browsing history [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…