Babu simu haikuwa kitu hata cha kufikiria kumiliki sababu ya uadimu wake. Nakumbuka kuna bwana mdogo m'moja wa kishua sana alikuwa anasoma Loyola, alikuwa tukikutana Bills amejikoki na gears zote yaani mixer ni M'marekani huyu hapa. [emoji23][emoji23][emoji23]
Unakuta kavaa zile vest kubwa za wacheza basketball juu ya flana, cheni kama tatu hivi tena kubwa za silver, jeans hizo za Sean John, chini amepiga buyu la maana (raba ya kibishoo), kichwani kavaa headband na mkononi ana handband pia, miwani, kabandika plaster shavuni kama Nelly, halafu hiyo jeans imevaliwa mlege halafu ndani ana pensi kama then kaning'iniza Motorola ya kuflip imekaa kama kalaptop kadogo, ukitaka kuiona hiyo sim ipo kwenye video ya Nelly na Kelly , Kelly anaonekana ameishika amekaa kweny dirisha. Halafu amening'niza Beeper (siku hizi hazipo tena).
Mradi tu aturushie roho mademu wamuone yeye tu mbwa yule [emoji23][emoji23][emoji23]