Leo tuwakumbuke wanamuziki wa mamtoni waliotamba miaka ya nyuma

Leo tuwakumbuke wanamuziki wa mamtoni waliotamba miaka ya nyuma

Mi nilikua siendagi Fiesta lakini ile Ja Rule nilitimba atleast nimuone mzee wa Unyamwezini. Sema nilivyofika pale na washkaji tukaanza kuzuzuka na mitungi na mademu Ja Rule mwenyewe anaperform tunamuona yuko mbaaali wala hatuna habari nae. Baadae akaanza kuimba New York New York wahuni wakaanza kuleta zengwe wanamwambia f*ck New York hapa tuko Dar
 
Sisqo na kundi lake la dru hill. Jamaa alikuwa bishoo balaa.
Kuna kundi la jagged edge, wale jamaa na ngoma zao fulani za kinyamwezi kuna moja inaitwa where is the party kuna nelly. Halafu walikuwa chini def jam ngoma anazigonja jamaine dupri producer tozi balaa.
**** mwanadada Eve alikuwa anachana balaa akiwa kundi la ruff ryders.
Kuna kundi la the fugees akiwa wycliff na mwanadada jina limenitoka. Yule dada alikuwa konyo aisee. Kuna ngoma fulani inaitwa guantanamela mle kacha vinaya mno.
Kuna fox brown yule dada alikuwa nachana si kidogo.
Kuna cris cross dah hawa jamaa nilikuwa anwaelewa sana

Sisqo Ngoja nipakue Unleash the dragon hiyo ngoma naipenda
 
Watatamba wote lakini nikisikia tu neno mamatoni namkumbuka mwamba mmoja wa kuitwa Curtis James Jackson Ila kama anavojulikana zaidi kama 50 Cent A K.A Ferrari

Picha Linaanza nikiweka we EATV enzi hizo tuinaiita Channel Five Ebana weee! Unakutana na kitu kinaitwa WANKSTAR
Dah hili Pini ni balaa aisee...

Hapo sijakumbuka IN DA CLUB, JUST A LIL BIT, CANDY SHOP [emoji91],21 QUESTIONS, I GET MONEY, WINDOW SHOPPER NA MANY MEN

Aisee 50 Cent alikua nyoqo Sana nyieeee...
Si T-shirt, suruali,viatu, mabegi Hadi chupi zilikua na chata ya 50
 
Dah hayo maisha ya Internet cafe acha kabisa [emoji23][emoji23] cafe ipi hatujaingia daslam mjini [emoji23][emoji23] Ila kuna kituko kimoja sitakaa nisahau. Enzi hizo net cafe saa nzima 500 . hiyo ndo ilikuwa bei elekezi. Labda uende za kishua mitaa ya Ohio serena saa nzima buku 2. Sasa Bwana kuna mshkaji wangu akaleta chimbo jipya liko mnazi mmoja mitaa ya mtendeni na kisutu akadai masaa matatu buku. Basi raia Hao kama wote [emoji23][emoji23] tukatia timu. Computer inaload hatari. Yan kufungua page dakika 5. Kumbe lile saa waliloongeza Ni kufidia loading [emoji23][emoji23][emoji23].
enzi hizo sony ericson, Mototrola L6 ndio simu zinazotamba mixer kuwa na infared kabla ya bluetooth🤣🤣
 
Hahahaha [emoji23][emoji23]Taima umenikumbusha mbali sana mazee. Niko form 2 2001 taima ndo habari ya mjini nikaleta bonge la zengwe home hadi bi mkubwa tukazama nae mitaa ya clock tower kuninunulia [emoji23][emoji23]. Hapo namake make viela vya shule ninunue jeans zile zinawaka waka pale kwa Mkorea ilikuwa 25k acha kabisa. Hapo T-shirts za Phat Farm, Dada Supreme, Roca Wear, sijui SOHK school of hard knocks yan balaa tupu. bado una jezi kibao za basketball Kina Iverson, sijui Jordan yuko Philadelphia 76ers, Kobe ya Lakers etc yan purukushani mtindo mmoja. Headband za kila rangi [emoji23][emoji23]

Ujana bana [emoji23] kama hujapitia hizi Mambo huwezi kujua raha zake
Mimi nilipewa Ada nikaenda kujinunulia Taima pair moja. Sitaki masikhara kabisa. Yaani me univalishe vile viatu vyeusi visivyo na chata. Khaaaaaah [emoji23][emoji23][emoji23]

Taima ni kiboko ya enzi hizo na ukivaa we ndio mtu sasa.
 
Dah hayo maisha ya Internet cafe acha kabisa [emoji23][emoji23] cafe ipi hatujaingia daslam mjini [emoji23][emoji23] Ila kuna kituko kimoja sitakaa nisahau. Enzi hizo net cafe saa nzima 500 . hiyo ndo ilikuwa bei elekezi. Labda uende za kishua mitaa ya Ohio serena saa nzima buku 2. Sasa Bwana kuna mshkaji wangu akaleta chimbo jipya liko mnazi mmoja mitaa ya mtendeni na kisutu akadai masaa matatu buku. Basi raia Hao kama wote [emoji23][emoji23] tukatia timu. Computer inaload hatari. Yan kufungua page dakika 5. Kumbe lile saa waliloongeza Ni kufidia loading [emoji23][emoji23][emoji23].
Mafala wametulia sana hela wale. Me nilikuwa naenda kwa babu wa kihindi pale mitaa ya fire kariakoo. Mzee computers zake alikuwa amewekea zile partitions yaani jirani hawezi ona unatizama nini.

Kwahiyo nilikuwa nina computer yangu hiyo ipo kona kule hakuna mtu anaweza kuona ukikaa huko. Nikijichimbia kule natulia nakula zangu picha za namna gani vipi tu.

Yule mzee alikuwa anatuchora sana nikifikiria saa hii kama alikuwa anacheki browsing history [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom