ExactlyWiki iliopita niliona kwenye CNN habari yenye caption 'US ECONONY GENERATES 170,000 JOBS IN APRIL' Umeona nini hapo? In short the ECONONY CREATES JOBS' not Waziri wa kazi. Hii inabidi ifanywe na wizara ya fedha,wizara ya kilimo,wizara ya viwanda na biashara. Wizara ya ajira itasimamia Sera na haki za wafanyakazi etc
The Economy Creates JOBS.
Mifuko ya pension yaweza kufa Kwa kuwalipa vijana pension wengi wenye nguvu zao wanaotakiwa kuzalisha sio kulala na kula pensionUmri wa kustaafu utakuwa miaka 47....ili na wengine wapate ajira!
Miaka 47 bado ni kijana?mifuko ya pensheni haiwezi kufa sababu mtu anachukua alichoweka!Mifuko ya pension yaweza kufa Kwa kuwalipa vijana pension wengi wenye nguvu zao wanaotakiwa kuzalisha sio kulala na kula pension
Hachukui alichoweka huchukua zaidi ya alichoweka Tena chapitiliza hata mara 20 kumbuka hutakiwa alipwe maisha yake yote Hadi siku anakufaMiaka 47 bado ni kijana?mifuko ya pensheni haiwezi kufa sababu mtu anachukua alichoweka!
Swala LA kuongeza, kutengeneza ajira sio swala LA kutatuliwa na waziri! Hakuna silver bullet ya kutatua, ni swala mtambuka, cross cutting, multisectorial issue, ni Sera, chanzo,cha ajira ni viwanda(sio, upuuzi, wa, vyereani vitatu), namaanisha manufacturing factories Kama kile cha vital vya umeme kigamboni, viwanda vya huduma Kama hii JF, sio, kupereka vijana Dodoma kulima alizeti! Wakulima inqbidi iwe 20% viwandani kuwe na 80%hapa kwetu ni kinyume, wakulima ni 80%ya, wananchi,umaskini hauwezi, Isha! Tunahitaji viwanda vya magari,bidhaa za, tekinolojia, tv, majiko, friji, electronics nk, kwanza tungeanza na kila tender ndogo za ujenzi, zifanywe na kampuni za wazawa! Hapa bongo, kila Kona yupo mchina,anatujengea madaraja, balabala, viwanja vya mpira,nashukuru tanesco imewapa kampuni binafsi service contract za service lineMara nyingi tumekuwa tukishauri viongozi vitu vya kufaya ili kusaidia maboresho katika Wizara na Serikali kwa ujumla. Sasa leo ukipewa wewe nafasi ya kuwa Waziri wa Kazi na Ajira, utafanya nini cha tofauti ili kusaidia kuongeza Ajira katika nchi yako?
Hoja zako Zina mashiko sana nimekuelewa Vizuri sana brother1. Nitapunguza masaa ya kazi kutoka masaa 11 hadi masaa sita yaani kuanzia muda wowote unaoingia kazini iwe saa moja jioni, saa saba mchana, saa kumi na mbili asubuhi, then hesabia kuanzia muda huo then mbele yako ni masaa sita unakuwa umemaliza muda wa kazi na utapisha mtu mwingine aingie shifti yako.
Hii itapunguza kwanza masaa ya kazi na kuwapa wafanyakazi nafasi ya kushiriki shughuli zingine za kijamii kama malezi ya familia, ndoa na biashara.
Lakini pia itapunguza ubwanyenye na umangi meza ambapo mtu anaweza hodhi ofisi na mamlaka na kuyatumia vibaya akijua ofisi yupo pekee yake na hatimae kuleta urasimu na ukiritimba kwenye ofisi za serikali na kuharibu ufanisi.
2. Nitafuta malipo ya mshahara kwa mwezi na kupendekeza taaisisi moja baada ya nyingine kuingizwa katika malipo ya masaa. Yaani masaa sita utalipwa kwa kila lisaa chini ya uangalizi na ukaguzi wa kufa mtu. Hii itapunguza mzigo wa serikali kulipa wafanyakazi hewa, na kulipa watu wasiofanya kazi. Mtu anaingia ofisini na kutoka masaa manne hayupo eneo la kazi ila mwisho wa siku analipwa, kwann analipwa?
3. Watu wataweza kuajiriwa na kuwa na mikataba zaidi ya mitatu. Yaani mfano mtu anaajiriwa CRDB, NMB na Exim, na kote huko anafanya kazi kwa masaa kulingana na uwezo wake. Au anaweza fanya kazi NMB, shirika la posta, na Hotelini kama Serena. Na kazi zote analipwa kwa masaa yake ya utendaji.
4. Nitabadilisha mfumo wa malipo badala ya mwezi waajiriwa watalipwa stahiki zao kwa wiki ili kupunguza msongamano wa malipo mwisho wa mwezi na pia kuwaondolea kadhia raia ya kupata malipo baada ya siku 30.
5. Nitashawishi mitaala ya vyuo vikuu kubadili masomo yasiwe notisi nyingi na mitihani mingi bali yawe ni lecture wastani, presentation za group na individual za kuongea ziongezwe, na seminars sessions,ziwe za kutosha ili kuwapa wanavyuo uwezo wa kitaaluma wa kuchanganua mambo, lakini pia nitashawishi serikali wanavyuo kutumia semester ya kwanza ya kila mwaka wa masomo kufanya field practice kwenye taaisisi mbali mbali popote walipo. Sio tu hadi kusubiri mwaka wa tatu.
Performance zao zikuwa nzuri zitawaruhusu kupata post za internships za kujitolea kwenye makampuni lengwa kulingana na taaluma zao, ili kuwasaidia kupata ujuzi na uzoefu wa kitaasisi na kuweza kutambua uhalisia na changamoto halisi na sio story za vijiweni au hadithi za matutorial na lecturers.
Pia vijana hawa nitashawishi serikali kutenga fungu maalumu waweze kupata vitu basic kama vifurishi vya simu kwaajiri ya mawasiliano, pesa ya chakula na nauli, na posho ya kujikimu kimaisha ili kuweza kuwasaidia kujihudumia kipindi wakiwa wanasubiria kupata mikataba kamili yenye stahiki zote. Watalipwa pia kwa masaa ila kwa 60% ya kiwango anacholipwa mfanyakazi wa kawaida kama basic salary.
6. Nitahakikisha kila taaisisi ya serikali ndani ya departments zake inakuwa na kitengo cha internships na kunakuwa na maofisa wake ambao wata act kama supervisors wa kurepoti kwenye taasisi yenyewe, vyuo, na wizarani kutoa ripoti za kimwenendo za hawa wahusika wataopewa nafasi aidha za trainings au internships.
Nitaongeza points nyingine baadae.
Suala la kupatikana kazi au kinyume chake, halitegemei wizara moja, tena yenye jina la 'kazi na ajira'. Ni mfumo mzima wa kiuchumi, utakaowezesha kushamiri kwa viwanda/vipuri, kilimo/pembejeo/soko, sera nzuri za uwekezaji, Kodi, elimu/ujuzi/mafunzo na vitendea/dhana kazi.Mara nyingi tumekuwa tukishauri viongozi vitu vya kufaya ili kusaidia maboresho katika Wizara na Serikali kwa ujumla. Sasa leo ukipewa wewe nafasi ya kuwa Waziri wa Kazi na Ajira, utafanya nini cha tofauti ili kusaidia kuongeza Ajira katika nchi yako?
Mara nyingi tumekuwa tukishauri viongozi vitu vya kufaya ili kusaidia maboresho katika Wizara na Serikali kwa ujumla. Sasa leo ukipewa wewe nafasi ya kuwa Waziri wa Kazi na Ajira, utafanya nini cha tofauti ili kusaidia
Moja nitabadilosha mtazamo wa soma uajiliwe nitakuja na matzamo somo uje ujiajili mwenyew na kutengeneza ajira Kwa wenzako ulio waacha shuleni.pia nitaongezashule za kujifunza stadi za maisha zaidi ili watu wawe wabobevu wa utengenezaji wa vitendo na sio utengenezaji wa vitu Kwa maneno maana yangu vyeta zitaongezewa nguvu Kwa watu wnao hitaji kupata stadi za maisha ili waweze kujiajili.kuongeza Ajira katika nchi yako?
Usemacho ni sahihi ila sekta pekee inayo weza kuchukua vijana wengi Kwa wingi ni sekta ya kilimo hasa ukizingatia Tanzania tuna ardhi kubwa yenye rutuba ni wajibu wa serikali kukifanya kilimo ni eneo la ajila Kwa msomi hata wa chuo kikuu Kwa kuwezesha pembe jeo kupatikana Kwa urahisi na kutafuta masoko yenye uhakika mkubwa Kwa hao vijana watakao jiwekeza kwenye kilimo humo vijijini wanakotoka kusiwepo na ubabaishaji.pia hata sekta za ufugaji Nako Kuna ajira nyingi kama tuta base huko katika mifugo hata uvuvi nijukumubla wenye zamana kupata mawazo yetu na kutengeneza muundo Bora wa miaka 20 ijayoSerikali inaajiri watu wachache sana hasa wanaomaliza vyuo vikuu na kwasasa wapo weeeengi mitaani . Waliosoma ualimu, afya, na kozi nyingine nyingi sana wapo na digrii mitaani.
Kuna baadhi ya sekta zinatakiwa kuongezwa waajiriwa , mfano kuongeza walimu mashuleni, kuongeza wataalamu afya na sekta nyingine hivyo hivyo.
Hatuwezi kuepuka kuboresha SEKTA BINAFSI AU PRIVATE SECTOR AMBAYO NDIO SEHEMU YA MWISHO KABISA AMBAYO WATU WOOOTE TENA KWA ASILIMIA KUBWA WAPO HUKO. Mazingira ya fursa za ajiria yatengenezwe.
Mitaala ya elimu iendane na ulimwengu wa Leo ili watu wajue kukabiliana nayo.
Lugha ya kusema wahitimu vyuo vikuu mkajiari ina maswali mengi sana hasa inapotamkwa na MTU aliyeajiriwa au mwanasiasa .Hii lugha ibadilishwe au isemwe na watu ambao wanajua uhalisia na ugumu wake ili inapoongelewa itaje na ugumu wake na sio KUROPOKA TU MKAJIARI NKNK.