Leo ukipewa nafasi ya kuwa Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira utafanya nini kuongeza Ajira nchini?

Leo ukipewa nafasi ya kuwa Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira utafanya nini kuongeza Ajira nchini?

Ni kuwekeza kwenye miundombinu ya usafirishaji na nishati na kuweka reform ya Sera za uwekezaji na kuondoa ukiritimba na rushwa.
Watu hawawezi kuja kuwekeza viwanda nchi ya kipumbavu kama hii isiyo na nishati ya uhakika , miundombinu ya usafirishaji na sera duni za uwekezaji zisizomlinda muwekezaji kwa ubabaishaji wa watendaji wa serikali na mifumo ya rushwa.
 
Wiki iliopita niliona kwenye CNN habari yenye caption 'US ECONONY GENERATES 170,000 JOBS IN APRIL' Umeona nini hapo? In short the ECONONY CREATES JOBS' not Waziri wa kazi. Hii inabidi ifanywe na wizara ya fedha,wizara ya kilimo,wizara ya viwanda na biashara. Wizara ya ajira itasimamia Sera na haki za wafanyakazi etc
The Economy Creates JOBS.
Exactly
 
Sioni ni kwa nini Tanzania tushindwe hata kuwa na viwanda vya kuzalisha mitambo midogo midogo wakati malighafi ya chuma , makaa ya mawe na gesi vipo .
Hii ni aibu
 
Jambo la kwanza ntasitisha vibali vya Wahindi na Wachina wote wanaofanya kazi ambazo Mtanzania anaweza kufanya, no matter what na sheria kali dhidi ya yeyote anayevunja.

Baada ya hapo ndio ntaanza kufikiria kuongeza ajira kupitia viwanda na biashara na kilimo. Atakayetaka mkopo wa biashara atapewa in instalmenta badala ya mkopo wa kusoma chuo kikuu.
Leseni zote za biashara ni bure kwa mtu mwenye umri miaka 18 mpaka 35. Kodi (income tax) itawekwa 1/4 ya kiasi kinacholipwa sasa kwa vijana wa umri huo.

Mikopo katika mabanks kwa subsidies.
Ngoja ntarudi
 
Mifuko ya pension yaweza kufa Kwa kuwalipa vijana pension wengi wenye nguvu zao wanaotakiwa kuzalisha sio kulala na kula pension
Miaka 47 bado ni kijana?mifuko ya pensheni haiwezi kufa sababu mtu anachukua alichoweka!
 
Miaka 47 bado ni kijana?mifuko ya pensheni haiwezi kufa sababu mtu anachukua alichoweka!
Hachukui alichoweka huchukua zaidi ya alichoweka Tena chapitiliza hata mara 20 kumbuka hutakiwa alipwe maisha yake yote Hadi siku anakufa

Kuna Fani mfano za madaktari bingwa,Maprofesa,Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na usalama ukiweka miaka 47 umri wa kustaafu uwezekano wa kutokuwapata mkubwa sababu kufikia viwango hivyo Mtu umri Huwa umesonga sana
 
Mara nyingi tumekuwa tukishauri viongozi vitu vya kufaya ili kusaidia maboresho katika Wizara na Serikali kwa ujumla. Sasa leo ukipewa wewe nafasi ya kuwa Waziri wa Kazi na Ajira, utafanya nini cha tofauti ili kusaidia kuongeza Ajira katika nchi yako?
Swala LA kuongeza, kutengeneza ajira sio swala LA kutatuliwa na waziri! Hakuna silver bullet ya kutatua, ni swala mtambuka, cross cutting, multisectorial issue, ni Sera, chanzo,cha ajira ni viwanda(sio, upuuzi, wa, vyereani vitatu), namaanisha manufacturing factories Kama kile cha vital vya umeme kigamboni, viwanda vya huduma Kama hii JF, sio, kupereka vijana Dodoma kulima alizeti! Wakulima inqbidi iwe 20% viwandani kuwe na 80%hapa kwetu ni kinyume, wakulima ni 80%ya, wananchi,umaskini hauwezi, Isha! Tunahitaji viwanda vya magari,bidhaa za, tekinolojia, tv, majiko, friji, electronics nk, kwanza tungeanza na kila tender ndogo za ujenzi, zifanywe na kampuni za wazawa! Hapa bongo, kila Kona yupo mchina,anatujengea madaraja, balabala, viwanja vya mpira,nashukuru tanesco imewapa kampuni binafsi service contract za service line
 
Kama ningepewa nafasi ya kuwa Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira nchini Tanzania, ningezingatia hatua zifuatazo kuongeza ajira:

Kuimarisha Uwezo wa Watu:

Kuwekeza katika elimu na mafunzo ya ujuzi: Ningeongeza ufadhili wa elimu ya ufundi na vyuo vya ufundi ili kuhakikisha vijana wanapata ujuzi unaohitajika na waajiri. Ningeanzisha pia programu za mafunzo ya ustadi kwa watu wazima ili kuwawezesha kubadilika na mahitaji ya soko la ajira.

Kukuza ujasiriamali: Ningetoa msaada wa kifedha na ushauri kwa vijana wanaotaka kuanzisha biashara zao wenyewe.

Ningeboresha pia mazingira ya biashara ili kuifanya iwe rahisi kwa biashara ndogo ndogo kustawi. Kuimarisha Uwezo wa Watu:

Kuwekeza katika elimu na mafunzo ya ujuzi: Ningeongeza ufadhili wa elimu ya ufundi na vyuo vya ufundi ili kuhakikisha vijana wanapata ujuzi unaohitajika na waajiri.

Ningeanzisha pia programu za mafunzo ya ustadi kwa watu wazima ili kuwawezesha kubadilika na mahitaji ya soko la ajira.

Kukuza ujasiriamali: Ningetoa msaada wa kifedha na ushauri kwa vijana wanaotaka kuanzisha biashara zao wenyewe. Ningeboresha pia mazingira ya biashara ili kuifanya iwe rahisi kwa biashara ndogo ndogo kustawi.

Kuunda Fursa za Ajira:

Kuhamasisha uwekezaji: Ningefanya kazi na sekta binafsi kuvutia uwekezaji katika sekta zinazozalisha ajira nyingi, kama vile utalii, kilimo, na viwanda.Kukuza miundombinu:-
Ningewekeza katika miundombinu kama vile barabara, reli, na bandari ili kuboresha ufanisi wa uchumi na kuunda ajira.

Kutekeleza sera za kukuza ajira: Ningeanzisha sera zinazohamasisha uundaji wa ajira, kama vile punguzo la kodi kwa waajiri wanaowaajiri vijana na wanawake.

Kuwasaidia Watafutaji Kazi:

Kuboresha huduma za ajira: Ningeboresha huduma za ajira za serikali ili kuwasaidia watafutaji kazi kupata ajira zinazofaa.

Kuunganisha waajiri na watafutaji kazi: Ningeunda jukwaa la mtandaoni linalounganisha waajiri na watafutaji kazi.

Kutoa msaada kwa watafutaji kazi: Ningetoa msaada kwa watafutaji kazi katika kuandika wasifu wao, kujiandaa kwa mahojiano, na kutafuta ajira.
Ninaamini kuwa kwa kutekeleza hatua hizi, tunaweza kuunda mazingira bora ya ajira nchini Tanzania na kuwawezesha vijana kufikia uwezo wao kamili.

Ni muhimu kutambua kuwa hizi ni baadhi tu ya hatua ninazoweza kuchukua kama Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira. Ningeendelea kushirikiana na wadau wote muhimu kuanzia JF,mashirika ya kiserikali, sekta binafsi na mashirika ya kimataifa, ili kuboresha hali ya ajira nchini.
 
1. Nitapunguza masaa ya kazi kutoka masaa 11 hadi masaa sita yaani kuanzia muda wowote unaoingia kazini iwe saa moja jioni, saa saba mchana, saa kumi na mbili asubuhi, then hesabia kuanzia muda huo then mbele yako ni masaa sita unakuwa umemaliza muda wa kazi na utapisha mtu mwingine aingie shifti yako.

Hii itapunguza kwanza masaa ya kazi na kuwapa wafanyakazi nafasi ya kushiriki shughuli zingine za kijamii kama malezi ya familia, ndoa na biashara.

Lakini pia itapunguza ubwanyenye na umangi meza ambapo mtu anaweza hodhi ofisi na mamlaka na kuyatumia vibaya akijua ofisi yupo pekee yake na hatimae kuleta urasimu na ukiritimba kwenye ofisi za serikali na kuharibu ufanisi.

2. Nitafuta malipo ya mshahara kwa mwezi na kupendekeza taaisisi moja baada ya nyingine kuingizwa katika malipo ya masaa. Yaani masaa sita utalipwa kwa kila lisaa chini ya uangalizi na ukaguzi wa kufa mtu. Hii itapunguza mzigo wa serikali kulipa wafanyakazi hewa, na kulipa watu wasiofanya kazi. Mtu anaingia ofisini na kutoka masaa manne hayupo eneo la kazi ila mwisho wa siku analipwa, kwann analipwa?

3. Watu wataweza kuajiriwa na kuwa na mikataba zaidi ya mitatu. Yaani mfano mtu anaajiriwa CRDB, NMB na Exim, na kote huko anafanya kazi kwa masaa kulingana na uwezo wake. Au anaweza fanya kazi NMB, shirika la posta, na Hotelini kama Serena. Na kazi zote analipwa kwa masaa yake ya utendaji.

4. Nitabadilisha mfumo wa malipo badala ya mwezi waajiriwa watalipwa stahiki zao kwa wiki ili kupunguza msongamano wa malipo mwisho wa mwezi na pia kuwaondolea kadhia raia ya kupata malipo baada ya siku 30.

5. Nitashawishi mitaala ya vyuo vikuu kubadili masomo yasiwe notisi nyingi na mitihani mingi bali yawe ni lecture wastani, presentation za group na individual za kuongea ziongezwe, na seminars sessions,ziwe za kutosha ili kuwapa wanavyuo uwezo wa kitaaluma wa kuchanganua mambo, lakini pia nitashawishi serikali wanavyuo kutumia semester ya kwanza ya kila mwaka wa masomo kufanya field practice kwenye taaisisi mbali mbali popote walipo. Sio tu hadi kusubiri mwaka wa tatu.

Performance zao zikuwa nzuri zitawaruhusu kupata post za internships za kujitolea kwenye makampuni lengwa kulingana na taaluma zao, ili kuwasaidia kupata ujuzi na uzoefu wa kitaasisi na kuweza kutambua uhalisia na changamoto halisi na sio story za vijiweni au hadithi za matutorial na lecturers.

Pia vijana hawa nitashawishi serikali kutenga fungu maalumu waweze kupata vitu basic kama vifurishi vya simu kwaajiri ya mawasiliano, pesa ya chakula na nauli, na posho ya kujikimu kimaisha ili kuweza kuwasaidia kujihudumia kipindi wakiwa wanasubiria kupata mikataba kamili yenye stahiki zote. Watalipwa pia kwa masaa ila kwa 60% ya kiwango anacholipwa mfanyakazi wa kawaida kama basic salary.

6. Nitahakikisha kila taaisisi ya serikali ndani ya departments zake inakuwa na kitengo cha internships na kunakuwa na maofisa wake ambao wata act kama supervisors wa kurepoti kwenye taasisi yenyewe, vyuo, na wizarani kutoa ripoti za kimwenendo za hawa wahusika wataopewa nafasi aidha za trainings au internships.

Nitaongeza points nyingine baadae.
Hoja zako Zina mashiko sana nimekuelewa Vizuri sana brother
 
Nitafuta malipo ya mshahara kwa mwezi na kupendekeza taaisisi moja baada ya nyingine kuingizwa katika malipo ya masaa ( kama USA). Yaani masaa sita utalipwa kwa kila lisaa chini ya uangalizi na ukaguzi wa kufa mtu. Hii itapunguza mzigo wa serikali kulipa wafanyakazi hewa, na kulipa watu wasiofanya kazi. Mtu anaingia ofisini na kutoka masaa manne hayupo eneo la kazi ila mwisho wa siku analipwa, kwanin analipwa wakati hajafanya Kazi siku nzima au amefanya siku zinazo pungua 24 Kwa mwezi .
 
Mara nyingi tumekuwa tukishauri viongozi vitu vya kufaya ili kusaidia maboresho katika Wizara na Serikali kwa ujumla. Sasa leo ukipewa wewe nafasi ya kuwa Waziri wa Kazi na Ajira, utafanya nini cha tofauti ili kusaidia kuongeza Ajira katika nchi yako?
Suala la kupatikana kazi au kinyume chake, halitegemei wizara moja, tena yenye jina la 'kazi na ajira'. Ni mfumo mzima wa kiuchumi, utakaowezesha kushamiri kwa viwanda/vipuri, kilimo/pembejeo/soko, sera nzuri za uwekezaji, Kodi, elimu/ujuzi/mafunzo na vitendea/dhana kazi.
Kama hayo mambo hayajawekwa vizuri kiufanisi, waziri haitakuwa na njia yoyote ya kuwezesha upatikanaji wa kazi wala ajira.
 
Huwa nashindwa kuelewa mnaposema mnazingatia wage load kuajiri wakati huo huo mna pesa za kutupa tupa kwenye miradi hewa Mnagharamia mashirika ya umma yanayojiendesha kwaHasara lakini kuajiri damu changa za Ardhi ya Hii nchi mnajibu haraka hakuna hela na kwamba hili tatizo ni la dunia nakutupa hela ovyo nalo ni tatizo la dunia?
 
Mara nyingi tumekuwa tukishauri viongozi vitu vya kufaya ili kusaidia maboresho katika Wizara na Serikali kwa ujumla. Sasa leo ukipewa wewe nafasi ya kuwa Waziri wa Kazi na Ajira, utafanya nini cha tofauti ili kusaidia

kuongeza Ajira katika nchi yako?
Moja nitabadilosha mtazamo wa soma uajiliwe nitakuja na matzamo somo uje ujiajili mwenyew na kutengeneza ajira Kwa wenzako ulio waacha shuleni.pia nitaongezashule za kujifunza stadi za maisha zaidi ili watu wawe wabobevu wa utengenezaji wa vitendo na sio utengenezaji wa vitu Kwa maneno maana yangu vyeta zitaongezewa nguvu Kwa watu wnao hitaji kupata stadi za maisha ili waweze kujiajili.

Pia Nita anzisha viwanda vidogo vidogo na masoko madogo madogo huko kwenye kila wilaya tunazo tokea ili kila mwenye utayali wa kuuza kitu aweze kufika eneo lile na kuuza bidhaa zake bila pingamizi lakini nitaji taidi kuipa kipaombele michezo yote na sio soka pekee kama ilivyo Sasa kila mchezo wenye kuwa kama anila utapewa kipaombele Kwa watu wanao ingia humo kucheza.
 
Serikali inaajiri watu wachache sana hasa wanaomaliza vyuo vikuu na kwasasa wapo weeeengi mitaani . Waliosoma ualimu, afya, na kozi nyingine nyingi sana wapo na digrii mitaani.
Kuna baadhi ya sekta zinatakiwa kuongezwa waajiriwa , mfano kuongeza walimu mashuleni, kuongeza wataalamu afya na sekta nyingine hivyo hivyo.
Hatuwezi kuepuka kuboresha SEKTA BINAFSI AU PRIVATE SECTOR AMBAYO NDIO SEHEMU YA MWISHO KABISA AMBAYO WATU WOOOTE TENA KWA ASILIMIA KUBWA WAPO HUKO. Mazingira ya fursa za ajiria yatengenezwe.
Mitaala ya elimu iendane na ulimwengu wa Leo ili watu wajue kukabiliana nayo.
Lugha ya kusema wahitimu vyuo vikuu mkajiari ina maswali mengi sana hasa inapotamkwa na MTU aliyeajiriwa au mwanasiasa .Hii lugha ibadilishwe au isemwe na watu ambao wanajua uhalisia na ugumu wake ili inapoongelewa itaje na ugumu wake na sio KUROPOKA TU MKAJIARI NKNK.
 
Serikali inaajiri watu wachache sana hasa wanaomaliza vyuo vikuu na kwasasa wapo weeeengi mitaani . Waliosoma ualimu, afya, na kozi nyingine nyingi sana wapo na digrii mitaani.
Kuna baadhi ya sekta zinatakiwa kuongezwa waajiriwa , mfano kuongeza walimu mashuleni, kuongeza wataalamu afya na sekta nyingine hivyo hivyo.
Hatuwezi kuepuka kuboresha SEKTA BINAFSI AU PRIVATE SECTOR AMBAYO NDIO SEHEMU YA MWISHO KABISA AMBAYO WATU WOOOTE TENA KWA ASILIMIA KUBWA WAPO HUKO. Mazingira ya fursa za ajiria yatengenezwe.
Mitaala ya elimu iendane na ulimwengu wa Leo ili watu wajue kukabiliana nayo.
Lugha ya kusema wahitimu vyuo vikuu mkajiari ina maswali mengi sana hasa inapotamkwa na MTU aliyeajiriwa au mwanasiasa .Hii lugha ibadilishwe au isemwe na watu ambao wanajua uhalisia na ugumu wake ili inapoongelewa itaje na ugumu wake na sio KUROPOKA TU MKAJIARI NKNK.
Usemacho ni sahihi ila sekta pekee inayo weza kuchukua vijana wengi Kwa wingi ni sekta ya kilimo hasa ukizingatia Tanzania tuna ardhi kubwa yenye rutuba ni wajibu wa serikali kukifanya kilimo ni eneo la ajila Kwa msomi hata wa chuo kikuu Kwa kuwezesha pembe jeo kupatikana Kwa urahisi na kutafuta masoko yenye uhakika mkubwa Kwa hao vijana watakao jiwekeza kwenye kilimo humo vijijini wanakotoka kusiwepo na ubabaishaji.pia hata sekta za ufugaji Nako Kuna ajira nyingi kama tuta base huko katika mifugo hata uvuvi nijukumubla wenye zamana kupata mawazo yetu na kutengeneza muundo Bora wa miaka 20 ijayo
 
Back
Top Bottom