Acheni hizo hicho kitu hatuwezagi, unaanzaje kwa mfano? Mwanamke kaumbiwa aibu. Binafsi siwezi mtamkia kaka neno lolote la kimahusiano kama hajaanza yeye.
kama ingekuwa ni rahisi basi mimi Mungu kanikutanisha na mtoto wa mkubwa no moja hapa mjini cha ajabu sina hata pa kuanzia.
tulikutana kikazi na kazi hiyo naendelea nayo pamoja nae ila ndo hivyo tena.
In short huyu kaka ana status kubwa dah.ila yupo charming. Tunaongelea maswala ya kazi tu. Kwa kweli nimemuelewa sio kwa sababu ya status ya familiya yao bali kaka mwenyewe yuko simple anaongea vizuri, dah akiongea kikiristo ndo utamu wake ulipo.
Jl wewe mtoto wa mama mkwe mmmh.
Nimeamini ukimuona mtu face to face ndo moyo unatoa jibu. Humu jf ya kufichana wacha yabaki hivyo hivyo.
Huyu kaka anakuwa mtu wa pili kumuelewa tangu nizaliwe, wa kwanza, hatukuweza kufikia malengo, sasa hivi anaishi na maisha yake huko mbali.wapili ndo huyu sidhani hata kama nitamsogelea ana status kubwa mno . Anyway nimeshare tuuuuuu.sina maana nyingine.