Leonardo aache kujiona msomi, kama ni degree kila mtu anayo

Leonardo aache kujiona msomi, kama ni degree kila mtu anayo

Kwani dhambi kujisifu, wako wanajisifu wao wazuri wako wanajisifu wana pesa na wako wanajisifu wamezaliwa Kariakoo sasa kwani Kariakoo kazaliwa peke yake, ni mtu kajisifu sawa tu hakuna kosa wewe msikilizaji ndio utaamua kusikiliza au kupuuza. Asiseme degree yake sio anakufa ndio utasikia ana degree hapo tena itamsaidia nini?
Hakika Jf ni chimbo la Greatthinker
 
Na hiki ndicho nilichokuwa namaanisha kwamba watu wachague sehemu ambayo hufurahii hamna haja kumbeza mtu wewe shika njia nyingine ufanye machaguzi yanayofaa,,,, siku moja pia nilikuwa naongea na rafiki yangu akasema eliudi hajuui kuchekesha anachekesha kitoto! Nikamwambia huyo anayechekesha kitoto Kuna watu wazima wanamsikiliza na wanacheka Cha muhimu Kama hakuchekeshi wewe chagua anayekuchekesha umfurahie...ni simple tu
Kifupi watu wanataka kulazimisha wenzao kwamba wanachokiona wao kinachekesha ndicho kinachochekesha.

Yani ni aina fulani ya kuwaburuza watu na kuwashikia akili.
 
Kifupi watu wanataka kulazimisha wenzao kwamba wanachokiona wao kinachekesha ndicho kinachochekesha.

Yani ni aina fulani ya kuwaburuza watu na kuwashikia akili.
Lakini pia ni kukubali kuwaza kwa ufinyu! Maana ukiwaza kwa mapana unatambua kuwa si kila linalokufurahisha wewe litamfirahisha mwingine na so kila likuchukizalo wewe litamchukiza mwingine wawaache vijana wajitafute ili mradi hawavunji Sheria wasiwavute nyuma
 
Huyu dogo ni limbukeni sana analazimisha vichekesho vinavyohusiana na shule,higher kearning ili aonekane msomi,
Mara ohh mama yangu ni mwalimu,so what???
Wengine mama zetu walikuwa malecturer,

Wengine mavyeti yanajaa sanduku ila tumechill tu.

Aache ushamba kama ni degree kila mtu anayo,tena from reputable universities sio vyuo vya kata kama alichosoma yeye

Kila saa mara ohoo nilipokuwa chuo sijui nini sijui nini,chuo chenyewe TEofili Kisanji TEKU

Hajui kuchekesha,abanimalizia king'amuzi tu.
Mkuu wewe kabila gani, mbona una dharau sana!
 
Punguza hasira kila mtu atajisifia tu, usimkabie kwa juu mwenzio. Tuliza kozazi.
 
Picha iko wapi? wengine hatuangaliagi hivyo vichekesho
 
Lakini pia ni kukubali kuwaza kwa ufinyu! Maana ukiwaza kwa mapana unatambua kuwa si kila linalokufurahisha wewe litamfirahisha mwingine na so kila likuchukizalo wewe litamchukiza mwingine wawaache vijana wajitafute ili mradi hawavunji Sheria wasiwavute nyuma
Naam.

Hususan kwa kitu ambacho hakina formula kama comedy.

Comedy si chemistry useme haya maji tunajua formula yake ni H2O, tunaweza kuyapima tujue yana impurities kwa asilimia ngapi.

It's absurd.
 
Unamuonea wivu mwanaume mwenzyo lol
Mtu mpaka kuanzisha uzi ujue kimemkaa sana kashindwa kujizuia.

Yani kuna watu wangapi wanajinywea mataptap wanayotaka wao wenyewe, kwa raha zao, kwa nini wewe ujione una mamlaka ya kusema haya mataptap mabaya, kunyweni single malt Scotch Whisky au Champagne?

Kama Champagne hawaipendi wanaona ina uchachu je, utawalazimisha wapende Champagne kwa sababu umekaririshwa hiyo ndiyo pombe ya watu wa matawi ya juu?

Kwa nini hatuwaachii watu creative freedom wafanye wanavyotaka, halafu tuachie wanaopenda wapende, na wasiopenda watuoneshe yao bora zaidi tuione tulinganishe wenyewe?
 
Na hiki ndicho nilichokuwa namaanisha kwamba watu wachague sehemu ambayo hufurahii hamna haja kumbeza mtu wewe shika njia nyingine ufanye machaguzi yanayofaa,,,, siku moja pia nilikuwa naongea na rafiki yangu akasema eliudi hajuui kuchekesha anachekesha kitoto! Nikamwambia huyo anayechekesha kitoto Kuna watu wazima wanamsikiliza na wanacheka Cha muhimu Kama hakuchekeshi wewe chagua anayekuchekesha umfurahie...ni simple tu
Una mitizamo na character vya kiswahili sana,
Mbona kwenye siasa, mpira na muziki watu wanachambua wanasiasia, wachezaji, makocha na wanamuzuki na kutoa maoni yao? Kwa nini iwe nongwa mtu akitoa maoni kuhusu hao wanakomedi wenu ambao wengi wanafanya comedy za ubora mdogo??
 
Mimi naona mleta mada una wivu. Alisema Snoop Dog kwamba ukiona kijana mdogo anauza maji juani nunua hata kama huna kiu kwasababu angeweza kuuza madawa ya kulevya akiwa kivulini. Hawa vijana wadogo tuwasapoti kwa kuweza kujiajiri kupitia vipaji vyao. Sanaa ya uchekeshaji ni ngumu kuliko unavyodhani.
Kwa nini comedians wenu wanafanya contents za mapenzi zaidi na vipato vya watu??
 
Yani mtu kujisifu usomi kwenye video za comedy zisizo na viwango watu wamekasirika?
 
Back
Top Bottom