Lete hoja au swali lolote kuhusu CCM ujibiwe hapa

Lete hoja au swali lolote kuhusu CCM ujibiwe hapa

Brother narudia tena, sizungumzii ukubwa au udogo wa mlichokifanya, nazungumzia 50m ambayo mliahidi na hamkuitoa! Anything nje na 50m ni utapeli! Mlilaghai wapiga kura, walipiga kura kwasababu ya ahadi ya 50m sio ya hayo mambo mengine
Kwa hiyo hao wapiga kura wanataka hizo pesa tu hawataki maendeleo mengine? Sawa nimekuelewa ndugu...kero zote zitaisha awamu inayofata.
 
uteuzi wa wagombea wa ccm, rushwa imetawala ( na jana Warioba alisemea sana hili) na bado mwenyekiti wenu hajalikemea hili. swali kwa hiyo sera ya ccm kupata ushindi inabariki rushwa? tutegemee rushwa zaidi kwa wagombea wenu dhidi ya wagombea wa upinzani?
 
Kwanini maeneo ambayo wananchi wamechagua viongozi wao wa kisiasa yanabaguliwa kwa maendeleo na kuambiwa wanachagua vibaya?
 
Nyie ccm wapiga kura wenu ni Wajumbe mio wahonga wananchi tutampigia kura ambaye hajahonga
 
Baba wa Taifa alituambia tuna maadui watatu.

Umasikini.
Ujinga.
Maradhi.

Vipi toka tupate uhuru 1961 adui yupi kati ya huyo mmeshammaliza.?
 
Katibu mkuu wa CCM alisema hadharani, bila hata kupepesa macho kuwa wanalitumia jeshi la polisi kubaki madarakani, aendelea kusema kuwa Kenya KANU ilishindwa kutumia polisi, sasa wamepotea katika uwanja wa siasa. alikuwa na maana gani? kwa uchaguzi wa mwaka huu mtatumia jeshi la polisi kubaki madarakani?
 
Hiyo kazi imefanyika kiustadi kwenye maeneo mengi tu ila si yote, na viongozi wetu wameliona hilo na utekelezaji wake unaandaliwa...

Karibu ccm ndugu.

Unaweza kutaja hayo "maeneo mengi" yaliyopata hizo milioni 50?

Kuhusu "utekelezaji wake kuandaliwa", unaweza kutuambia hatua iliyofikiwa na lini hizo milioni 50 zitafikia kila kijiji?
 
Habari zenu watanzania!

Huu ni mwaka wa uchaguzi ambapo zimebaki miezi michache chama chetu pendwa ccm kwenda kujinyakulia ushindi wake wa kishindo kuanzia kuanzia ngazi ya za chini kabisa hadi urais...


Jitokezeni kwa wingi kusapoti chama chenye uhakika wa kushinda ili mpendwa wetu Jpm aendelee kulinyoosha taifa.

Chama cha makumbafu...!!
 
Naondoka zangu naona umeshindwa kunipatia ufumbuzi wa maslahi ya wafanyakazi na kutoa ajira kwa vijana.
 
Kwanini maeneo ambayo wananchi wamechagua viongozi wao wa kisiasa yanabaguliwa kwa maendeleo na kuambiwa wanachagua vibaya?
Hakuna maeneo yanayobaguliwa ndugu, maendeleo hayana chama
 
Kwa hiyo hao wapiga kura wanataka hizo pesa tu hawataki maendeleo mengine? Sawa nimekuelewa ndugu...kero zote zitaisha awamu inayofata.
Hapana, don't get me wrong! Ninachoamini ni kwamba, hadi kufikia kuahidi publicly ni kwamba kuna taarifa zimeshafanywa na kukusanywa! Sasa kuja kubadili bila taarifa kwa kisingizio cha maendeleo ni uhuni na uzandiki! I stand to be corrected
 
Naondoka zangu naona umeshindwa kunipatia ufumbuzi wa maslahi ya wafanyakazi na kutoa ajira kwa vijana.
Ajira zinatolewa ila sio rahisi kwa vijana wote kupata ajira, hakuna kabisa nchi inayoweza kufanya hivo...sisi tunajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu ili angalau % kubwa ya vijana wapate ajira
 
Hakuna maeneo yanayobaguliwa ndugu, maendeleo hayana chama
Sasa wewe unaharibu mjadala! Video clips zipo kuanzia za Ma-DC hadi Mwenyekiti wako na most recent akiwa kwenye jumbo la Mheshimiwa Bwege aliongea pia ina akiwa Morogoro aliongea hadi akaambiwa kuwa ni jimbo linaloongozwa na CCM. Brother usitufanye wote vilaza
 
Baba wa Taifa alituambia tuna maadui watatu.

Umasikini.
Ujinga.
Maradhi.

Vipi toka tupate uhuru 1961 adui yupi kati ya huyo mmeshammaliza.?
Asante kwa swali zuri, ni kwamba hakuna adui yeyote kati ya hao ambaye anaweza kutokomezwa kabisa ila tunachokifanya ni kumpunguza makali adui yetu.
 
Back
Top Bottom